Translate
Jumanne, 30 Aprili 2019
Fadhila za Kusuluhisha Waliogombana
Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh
BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa ba’ad.
Naam, Ndugu zangu katika Imaani Muda huu napenda kuchukua Fursa hii kufikisha kwenu japo kwa Uchache Darsa letu lenye anuani isemeyo Fadhila za Kusuluhisha Waliogombana
➡Anasema Allaah سبحانه وتعالى Kwamba⤵
((لاَّ خَيْرَ فِي كَثِيرٍ مِّن نَّجْوَاهُمْ إِلاَّ مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلاَحٍ بَيْنَ النَّاسِ وَمَن يَفْعَلْ ذَلِكَ ابْتَغَاء مَرْضَاتِ اللّهِ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمً ))
((Hakuna kheri katika mengi ya wanayoshauriana kwa siri, isipokuwa kwa yule anayeamrisha kutoa sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi ya Allaah basi Tutakuja mpa ujira mkubwa))
↪Suratul An-Nisaa Aya ya 114.
➡Na kasema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kwamba⤵
((ألا أخبركم بأفضل من درجة الصيام والصلاة والصدقة ؟ إصلاح ذات البين وفساد ذات البين هي الحالقة)) رواه أحمد وأبو داود والترمذي صحيح الجامع
((Je, nikujulisheni lililo na daraja bora kuliko Swawm na Swalah na Sadaqah? Ni kusuluhisha baina ya watu. Na ama kuharibu uhusiano (baina ya watu) ni uharibifu.
↪Imepokelewa na Imaam Ahmad na Abu Daawuud na At-Tirmidhy katika Swahiyhul-Jaami'i
Ndugu zangu katika Imaani, Katika mambo ya kheri Aliyoyataja Allaah سبحانه وتعالى watu wanapozungumza kwa siri ni kuamrishana kutoa sadaka au kutenda mema. Kisha Ametaja kuhusu kupatanisha watu, jambo ambalo mara kwa mara hutokea katika jamii na khaswa jamii yetu.
➡Na bila ya shaka ugomvi na ikhtilaaf ni katika silaha ya hatari kabisa anayopenda kuitumia Shaytwaan kufarikisha watu watengane na kuchukiana baada ya kuwa ni ndugu au marafiki au majirani au baina ya mume na mke.
➡Lakini Uislamu haukuacha kutilia hima jambo la kusuluhisha ugomvi kwa kutukumbusha fadhila zake kubwa katika Qur-aan na Sunnah kama tunavyoona katika Aayah na Hadiyth hapo juu.
➡Lakini inasikitisha kuona kwamba jambo hili la kusuluhisha halikutiliwa mkazo sana katika jamii yetu, kwani wangapi tunasikia miongoni mwetu kuwa *'fulani kagombana na fulani na hawasemeshani',* kisha zikapita siku na miezi na miaka hawa watu wako katika hali hii jambo ambalo Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amekataza kabisa zisipite zaidi ya siku tatu ndugu wa Kiislamu kuwa katika hali kama hiyo⤵
عن أبي أيوب الأنصاري رضي الله عنه قال : قال النبي صلى الله عليه وسلم : (( لا يَحِلُّ لِمُسْلِمٍ أَنْ يَهْجُرَ أَخَاهُ فَوْقَ ثَلَاثِ لَيَالٍ ، يَلْتَقِيَانِ فَيُعْرِضُ هَذَا وَيُعْرِضُ هَذَا ، وَخَيْرُهُمَا الَّذِي يَبْدَأُ بِالسَّلامِ .(( رواه البخاري ومسلم و في رواية أبو داود بإسناد على شرط البخاري ومسلم
((فَمَنْ هَجَرَ فَوْقَ ثَلاَثٍ فَمَاتَ دَخَلَ النَارَ ))
Imetoka kwa Abu Ayyuub Al-Answariy رضي الله عنه ambaye alisema: Kasema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم: ((Haimpasi Muislamu amhame ndugu yake zaidi ya siku tatu hata wanapokutana huyu anamgeuzia (uso) huyu na huyu anamgeuzia (uso) huyu. Na aliye mbora wao ni yule anayeanza kutoa salaam))
↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhariy na Muslim na katika Riwayaah ya Abu Daawuud
Na nyingine...
((Atakayemhama (mwenzake) zaidi ya siku tatu akafariki basi ataingia motoni))
Ndugu zangu katika Imaani,na huenda ikawa kila mmoja anataka kupatana na mwenziwe lakini Shaytwaan amewatia ari kuwa vipi aanze yeye?
➡Na pia pengine huenda wakawa ni ndugu, au jamaa au jirani lakini hakuna mmoja wetu anayekimbilia kusuluhisha, sababu ni kwamba kila mmoja ameshughulika na kazi zake na maisha yake.
➡Kwa hiyo tulichukulie hima jambo hili bila ya kuchelewesha kila inapotokea ugomvi baina ya ndugu wa Kiislamu na kufanya hivyo ni kumcha Allaah سبحانه وتعالى, kumtii Allaah سبحانه وتعالى na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na ndio sifa ya Waumini kama Anavyosema Allaah سبحانه وتعالى kwamba⤵
((فَاتَّقُواْ اللّهَ وَأَصْلِحُواْ ذَاتَ بِيْنِكُمْ وَأَطِيعُواْ اللّهَ وَرَسُولَهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ))
((Basi mcheni Allaah na suluhisheni mambo baina yenu, na mtiini Allaah na Mtume Wake ikiwa nyinyi ni Waumini))
↪Surat Al-Anfaal Aya ya 1
Ndugu zangu katika Imaani, Tukiendelea na fadhila za kusuluhisha waliogombana wakakhasimiana, na iwapo baada ya kusoma mada hii tutazithamini fadhila hizi, basi kila mmoja wetu atakimbilia kufanya hima ya kupatanisha ndugu zetu wa Kiislamu waliogombana /waliokhasimiana.
➡Allaah سبحانه وتعالى Amelichukia jambo hili kwani linavunja asili ya undugu wa Kiislamu kama Anavyosema⤵
((إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ))
((Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu))
↪Surat Al-Hujuraat Aya ya 10.
➡Na kwa jinsi jambo hili lilivyochukiza hadi kwamba Allaah سبحانه وتعالى Anakataa kupokea amali za watu Waliogombana /waliokhasimiana mpaka wapatane, na hawasamehe watu hao⤵
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((تُعرض الأعمال في كل أثنين وخميس فيغفر الله لكل أمريء لايشرك بالله شيئاً، إلا إمرءاً بينه وبين أخيه شحناء فيقول: اتركوا هذين حتى يصطلحا)) رواه مسلم
Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه kwamba kasema Mtume صلى الله عليه وسلم: Amali njema (vitendo vyema) hutandazwa kila Jumatatu na Alkhamiys, kisha Allaah Humghufuria kila mtu asiyemshiriki kitu Allaah, isipokuwa mtu aliyekuwa baina yake na baina ya ndugu yake uhasama, Husema: Waacheni hawa wawili mpaka wapatane))
↪Imepokelewa na Imaam Muslim
Kwa hiyo ni hatari kubwa kwa waliogombana na hawataki kusameheana watambue kuwa wanapoteza umri wao bure kutenda Mema na hali kumbe havipokelewi vitendo hivyo hadi wapatane. Kwahiyo ni Wajibu kusameheana kwanza ili utaraji Malipo kwa Allaah.
Njia za kupatanisha Waliogombana
1⃣Kwanza tia nia kuwa unafanya kupata Radhi na ujira mkubwa kutoka kwa Allaah سبحانه وتعالى, na muombe Allaah سبحانه وتعالى Akuwafikie jambo hili.
2⃣Msikilize kila mmoja malalamiko yake.
3⃣Ukishajua sababu ya ugomvi, watajie hatari ya kuhasimikiana kama Anavyosema Allaah سبحانه وتعالى na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم .
4⃣Tafuta wakati na sehemu munaasib kwa wote wawili.
5⃣Ikibidi kusema uongo, inafaa katika jambo hili kwa kutaka kumridhisha mmojawao ili kuleta suluhisho kama alivyoruhusu Mtume صلى الله عليه وآله وسلم katika Hadiythi⤵
((لَيْسَ الْكَذابُ الَّذِي يُصْلِحُ بَيْنَ النَّاسِ فَيَنْمِي خيرا أو يقول خيرا)) رواه البخاري ومسلم
((Si muongo yule anayesuluhusha watu kwa kusema uongo, kwani anaarifu mema au anasema mema [kwa lengo la kusuluhisha]))
↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhariy na Muslim
6⃣Fanya uadilifu, usipendelee hata kama mmoja ni jamaa yako wa karibu au unampenda zaidi.
➡Amesema Allaah سبحانه وتعالى⤵
((...فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا بِالْعَدْلِ وَأَقْسِطُوا إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ))
((…basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Allaah Anawapenda wanaohukumu kwa haki))
↪Surat Al-Hujuraat Aya ya 9.
➡Na Anasema tena Allaah سبحانه وتعالى ⤵
((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ كُونُواْ قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاء لِلّهِ وَلَوْ عَلَى أَنفُسِكُمْ أَوِ الْوَالِدَيْن وَالأَقْرَبِينَ إِِن يَكُنْ غَنِيًّا أَوْ فَقَيرًا فَاللّهُ أَوْلَى بِهِمَا فَلاَ تَتَّبِعُواْ الْهَوَى أَن تَعْدِلُواْ وَإِن تَلْوُواْ أَوْ تُعْرِضُوا فَإِنَّ اللّهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ))
((Enyi mlioamini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu, mtowao ushahidi kwa ajili ya Allaah, ijapokuwa ni juu ya nafsi zenu, au wazazi wawili na jamaa zenu. Akiwa tajiri au masikini Allaah Anawastahikia zaidi. Basi msifuate matamanio, mkaacha kufanya uadilifu. Na mkiupotoa au mkajitenga nao basi Allaah anajua vyema mnayoyatenda))
↪Surat An-Nisaa Aya ya 135
7⃣Wakishapatana In shaa Allaah omba du'aa Allaah سبحانه وتعالى Awaendeleze masikilizano na mapenzi baina yao na muombe pia Akutakabalie juhudi yako.
Mwisho tunamuomba Allaah سبحانه وتعالى Atunufaishe kwa yale tunayojifunza na Atuajaalie miongoni mwa wale wanaosikiliza kauli (nyingi) wakafuata zile zilizo njema.
Aamiyn.
Na Allaah anajua zaidi
http://bit.ly/2USSrfb i live islam
Hukmu ya Wanaume kupiga Makofi katika Mihadhala
Swali
Nini hukumu ya kupiga makofi wanaume wanapokuwa wanapongeza mtu au kushangilia jambo kama tunavoona ktk mihadhara, makongomano, semina, mijadala na midahalo ya dini? Hili limekuwa jambo la kawaida hata ktk TV za Kiislamu tunazoona.
Jibu
Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema:
وَمَا كَانَ صَلَاتُهُمْ عِندَ الْبَيْتِ إِلَّا مُكَاءً وَتَصْدِيَةً
((Na haikuwa Swalaah [‘ibaadah] zao [makafiri] kwenye Nyumba [Tukufu yaani Ka’bah] isipokuwa ni miruzi [mbinja] na kupiga makofi)). [Al-Anfaal: 8: 35].
قال الرسول صلى الله عليه وسلم: (مَنْ نَابَهُ شَيْءٌ فِي صَلَاتِهِ فَلْيُسَبِّحْفَإِنَّهُ إِذَا سَبَّحَ الْتُفِتَ،، و إِنَّمَا التَّصْفِيقُ لِلنِّسَاءِ). رواه البخاري (684) ومسلم (421)
“Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayetanabahi kitu katika Swalah yake, alete tasbiyh [Aseme Subhaana-Allaah] kwani anapoitamka, humvutia mtu atanabahi, na hakika kupiga makofi ni kwa ajili ya wanawake)).” Al-Bukhaariy (684), Muslim (421)
Imeulizwa kuhusu tafsiyr ya:
وَمَا كَانَ صَلَاتُهُمْ عِندَ الْبَيْتِ إِلَّا مُكَاءً وَتَصْدِيَةً
((Na haikuwa Swalaah [‘ibaadah] zao [makafiri] kwenye Nyumba [Tukufu yaani Ka’bah] isipokuwa ni miruzi [mbinja] na kupiga makofi)). [Al-Anfaal: 8: 35
Imaam ‘Abdul-’Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
Hiyo ni Swalaah ya watu wa jaahiliyyah yaani makafiri wa ki-Quraysh na waliyokuwa wakifanya ya miruzi na kupiga makofi. Ikawa ada yao kupiga makofi kwa mikono na kupigia miruzi wakaharamishwa Waislamu vitendo kama vyao. Kwa hiyo haimpasi Muislamu apige miruzi au makofi katika ‘ibaadah zao wala katika Masjidul-Haraam wala katika vitendo vyake vinginevyo, bali kupiga makofi ni kwa ajili ya wanawake. Ama mwanamme aseme anapotanabahisha jambo; alete tasbiyh katika Swalaah: Subhaana-Allaah! Subhaana-Allaah! Wala asitumie miruzi, bali atamke maneno yanaohitajika bila ya miruzi.
Swali
Nini hukmu ya watu kupiga makofi katika sherehe, matukio na mihadharah na makongamano?
Kupiga makofi ni katika vitendo vya ujaahiliyyah na hukmu ya chini kabisa ni jambo ka kuchukiza na lililo dhahiri kabisa katika dalili ni kuharamishwa kwake kwa sababu Waislamu wamekatazwa kuigiza makafiri, Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) katika kuwaelezea makafiri wa Makkah:
وَمَا كَانَ صَلَاتُهُمْ عِندَ الْبَيْتِ إِلَّا مُكَاءً وَتَصْدِيَةً
((Na haikuwa Swalaah [‘ibaadah] zao [makafiri] kwenye Nyumba [Tukufu yaani Ka’bah] isipokuwa ni miruzi [mbinja] na kupiga makofi)). [Al-Anfaal: 8: 35].
Wanavyuoni wamesema: ‘Al-Mukaa’ ni Miruzi na ‘At-Taswdiyah’ ni kupiga makofi. Na Sunnah kwa Muumini ni kwamba anapoona au kusikia jambo linalompendeza au linalomchukiza aseme: “Subhaana-Allaah” au aseme: “Allaahu Akbar” kama ilivyothibiti kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth nyingi. Na imeruhusiwa wanawake kupiga makofi hasa wanapotanabahisa kitu katika Swalaah au wanapokuwa na wanaume pale Imaam anaposahau kitu katika Swalaah basi inaruhusiwa atanabahishe kwa kupiga kofi. Ama wanaume anapokosea Imaam, wao wanatakiwa walete tasbiyh kama ilivyotibiti katika Sunnah kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na kwa hayo, inatambulikana kwamba wanaume kupiga makofi ni katika kuigiza makafiri na kuwaiga wanawake; na yote hayo yamekatazwa.
Na Allaah Ndiye Mwenye kuleta Tawfiyq.
Kwa faida, Ash-Shawakaan amesema katika ‘Niyl Al-Awtwaar’: (kuhusu kauli ya Mtume Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Hakika kupiga makofi ni kwa ajili ya wanawake))
inamaanisha kwamba imekatazwa kwa wanaume kabisa kwani Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayejishabihisha na watu basi yeye ni miongoni mwao)).
Na Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema katika: ‘Al-Iqtidhwaa’ (1/83):
“Hadiyth hii, inaonyesha na kuthibitisha kuwa, hali ya chini kabisa ni kuharamishwa kushabihiana nao japokuwa dhahiri yake ni hukmu kuwa ni kufru kushabihiana nao kama katika kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ
((Na yeyote atakayewafanya marafiki; basi hakika yeye ni miongoni mwao)) [Al-Maaidah: 51].
Na akasema pia kuhusu Hadiyth hii katika ‘Al-Iqtidhwaa’ (1/81):
“Sababu ya kuharamishwa huku ni kushabihiana (kujifananisha) nao.”
Na Fatwa ya ‘Allaamah Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) chini, inatilia nguvu yaliyotanguliwa kuelezwa:
Swali:
“Fadhwilat Shaykh, Allaah Akuhifadhini: Nafanya kazi ya udaktari na nnapohudhuria vikao au makongamano ya udaktari, wanaume husimama kumpigia makofi mtoa mada. Ninapowaambia kwamba hakika kupiga makofi haifai kwenu bali ni kwa wanawake tu, husema: Hukmu hiyo imekusudiwa katika Swalaah pekee. Je, maneno haya ni sahihi?
Akajibu ‘Allaamah Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah):
Hapana! Si sahihi. Wanaume hawatakiwi kupiga makofi katika Swalaah wala kwengineko. Kupiga makofi ni kwa ajili ya wanawake na si kwa wanaume katika Swalaah au kwengineko. Hivyo ni kwa upande mmoja. Ama kwa upande mwengine, ni kwamba kuna kujifananisha na makafiri. Hiyo ni ada ya makafiri hatukuwa tukiijua wala Waislamu hawakuwa wakiijua (wakifanya) au hapakuwepo wanaume kupiga makofi isipokuwa ilipotujia mila na desturi za kikafiri katika sherehe zao na katika mikusanyiko yao. Na kupiga makofi pia ni katika mambo ya kijaahiliyyah:
وَمَا كَانَ صَلَاتُهُمْ عِندَ الْبَيْتِ إِلَّا مُكَاءً وَتَصْدِيَةً
((Na haikuwa Swalaah [‘ibaadah] zao [makafiri] kwenye Nyumba [Tukufu yaani Ka’bah] isipokuwa ni miruzi [mbinja] na kupiga makofi)). [Al-Anfaal: 8: 35
Wanavyuoni wamesema: ‘Al-Mukaa’ ni Miruzi na ‘At-Taswdiyah’ ni kupiga makofi. Kwa hiyo kupiga makofi ni katika kitendo cha kafiri. Na sasa (siku hizi) Subhaana-Allaah Wanapiga makofi na kupiga miruzi katika sherehe kama kitendo cha jaahiliyyah.”
Na Allaah Anajua zaidi
http://bit.ly/2PCgT3i i live islam
Anaishi na Mwanaume Mkristo Je akifunga Ramadhaan Swawm itaswihi?
Swali
Swali langu ndugu zangu katka iman ..inakuaje binti waislam anaishina mkristu na amezaa nae watt zaidi ya mmoja alafu anajiweka katk kuufunga mwezi waradhani nabado anaendelea kuishi nae na anahudumiwa kama mke
Je hukumu yake nini au je inaswihi au laa
Jibu
Naam Swawm yake inaswihi
Naam kwanza kabisa ni WAJIBU kwa Muislam kufunga Mwezi wa Ramadhaan.
Maulamaa wamekubaliana kufunga ni wajibu kwa Muislam mwenye akili timamu, Baleghe, mwenye afya na mkazi wa mji. Tukiongezea wanawake waliotwaharika na hedhi na nifasi.
Kwahiyo ikiwa wewe Mwanamke ni Muislam basi ni Lazima Ufunge Mwezi wa Ramadhaan na haijalishi unaishi na kafiri.
Jambo lingine ni kwamba ni HARAMU kwa Mwanamke wa Kiislamu kuishi na Mwanaume Mkristo kama Mumewe.
Hapo Mwanamke unakuwa unafanya Zinaa na Allaah amekataza Zinaa na ni Uchafu.
Allaah(Subhaana wa Taala) Ametoa ruhusa kwa mwanamume wa Kiislamu tu kumuoa mwanamke wa Kitabu (Mkristo au Myahudi).
Hata hivyo Allaah (Subhaana wa Taala) hakuliacha jambo hilo bila kuliekea masharti.
Ikiwa masharti hayo yaliyowekwa yatakuwa ni yenye kutimizwa basi kutakuwa hakuna tatizo. Aayah inayohusiana na hilo ni ile ya Suratul Maa’idah Aya ya 5
*“Leo mmehalalishiwa vyote vizuri, na pia chakula cha waliopewa Kitabu ni halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao. Na wanawake Waumini Muhswanaat na wale Muhswanaat waliopewa Kitabu kabla yenu ikiwa mtawapatia ujira (mahari) wao kuwataka kwa ndoa wala sio kuweka wazi zinaa wala kuwachukua kama vimada kwa siri”.*
Ama hili neno *Muhswanaat* lina maana ya *wanawake wema watwaharifu waliojiweka mbali na uzinzi(Uzinifu).*
Na ibara za mbele zinamaanisha kuwa wanawake hawa wasiwe ni wale wenye kufanya zinaa kwa siri au dhahiri.
Basi ikiwa Mkristo ana sifa hizo basi unaweza kumuoa baada ya kutimiza na hayo masharti mengine ya ndoa.
Hukumu ya zinaa ikiwa ni kwa siri au ni dhahiri adhabu yake ni mijeledi 100 ikiwa mwanamke au mwanamume hajaolewa na ikiwa ameoa au ameolewa basi adhabu yake ni kupigwa mawe mpaka kufa.
Kwahiyo Kinachotakiwa Hapo Mwanamke wa Kiislamu ni kuachana kabisa na huyo Mwanaume Mkristo na Kisha Kufanya Tawbah ya Kweli.
Ama pia huyo mwanaume anaweza kubadili Dini na kusilimu kuwa Muislam na Kisha kufunga Ndoa ya Kisheria.
Hukmu ya Watoto watakuwa ni wa mama kwasababu watoto wamepatikana kwa njia ya Zinaa.
Ama Kuhusu Swawm ikiwa Mwanamke atafunga basi Swawm yake Itaswihi.
Naam mara nyingi sisi kama wanadamu na hasa kama waislamu tunakosa hisia kwa kuona kuwa tukifanya dhambi kwa siri basi huwa hakuna dhambi wala adhabu.
Allaah (Subhaana wa Taala) Anasema:
((كَذَلِكَ الْعَذَابُ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ))
((Namna hivi inakuwa adhabu (Ya Mola duniani) Na adhabu Akhera ni kubwa zaidi, laiti wangalijua!))
[Surat Al-Qalam Aya ya 33]
Nasaha zangu nasaha tunawausia ndugu na dada zetu sote kwa pamoja tumche Allaah kwani mafanikio yetu hapa duniani na kesho Akhera ni kuwa katika msimamo huo.
Ikiwa tumefanya jambo baya, la makosa hiyo ni katika udhaifu wetu, binadamu. Hivyo, tuombe toba na tufanye mambo mema. Na tunamuomba Allaah Atuepushe kufanya madhambi kwa siri au dhahiri.
Na Allaah Anajua zaidi.
http://bit.ly/2ISsURM i live islam
Watoto wa makafiri wataingia Peponi
1818- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Nilimuomba Mola wangu wachanga ambapo akawanipa.” Nikamuuliza ni nini wachanga? Akasema: “Watoto wa watu.”
Ameipokea al-Mukhallas (09/23-24) kupitia Ahmad bin Yuusuf at-Taghlabiy ambaye amesema: Swafwaan bin Swaalih ametuhadithia: al-Waliyd ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Hassaan al-Kitaaniy ametuhadithia: Muhammad bin al-Munkadir ametuhadithia, kutoka kwa Anas, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Tukikusanya njia zake zote naona kuwa Hadiyth ni nzuri na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
Hadiyth hii ni dalili inayoonyesha kwamba watoto wa makafiri wataingia Peponi. Haya ndio maoni yenye nguvu, kama nilivyobainisha “Dhwilaal-ul-Jannah” (01/95).
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2J6qK06
via IFTTT
18. Ni ipi hukumu ya mwenye kufunga ilihali ni mwenye kuacha swalah?
Swali 18: Ni ipi hukumu ya mwenye kufunga ilihali ni mwenye kuacha swalah? Je, funga yake ni sahihi?
Jibu: Maoni yenye nguvu ni kwamba kuacha swalah kwa makusudi mtu anafuru ukafiri mkubwa kwa kitendo hicho. Hivyo swawm yake wala ´ibaadah zake zengine hazisihi mpala pale atapotubia kwa Allaah (Subhaanah). Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ
“Lau wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda.”[1]
Kuna Aayah na Hadiyth nyingi zilizo na maana yake.
Wapo wanachuoni wengine wenye kuona kwamba mtu hakufuru kwa kitendo hicho na wala swawm na ´ibaadah zake zengine haziharibiki midhali ni mwenye kukubali uwajibu wake lakini hata hivyo ameacha swalah kwa sababu ya kuzembea na uvivu. Lakini maoni yenye nguvu ni yale ya kwanza yanayosema kwamba anakufuru kwa kuiacha kwake kwa makusudi japokuwa atakiri uwajibu wake. Zipo dalili nyingi ikiwa ni pamoja na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Baina ya mtu na ukafiri na shirki ni kuacha swalah.”
Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa).
Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yule mwenye kuiacha amekufuru.”
Ameipokea Imaam Ahmad na waandishi wane wa “as-Sunan” kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kupitia kwa Buraydah bin al-Huswayb al-Aslamiy (Radhiya Allaahu ´anh). ´Allaamah Ibn-ul-Qayyim (Radhiya Allaahu ´anh) amelizugumza hilo vya kutosha katika kijitabu chake cha kipekee katika “Ahkaam-us-Swalaah wa Tarkiyhaa”. Ni kijitabu chenye faida na kizuri ambacho ni vizuri kukirejelea na kufaidika nacho.
[1] 06:88
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2IS4J5C
via IFTTT
39. Hukumu ya uasi dhidi ya mtawala wa Kiislamu
Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
“Yule anayefanya uasi dhidi ya kiongozi wa waislamu ambaye watu wamekusanyika juu yake na wakakubali ukhaliyfah wake kwa njia yoyote ile, kwa kuridhia au kwa nguvu, amewatawanyisha waislamu na ameenda kinyume na mapokezi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mfanya uasi huyu akifa katika hali hii, basi amekufa kifo cha kipindi cha kikafiri.”
MAELEZO
Haijuzu kumfanyia uasi kiongozi wa waislamu ijapokuwa atakuwa ni mtenda maasi na madhambi. Kuna sampuli mbili za uasi:
1- Uasi wa kimatendo na mapambano.
2- Uasi wa kimaneno, uchokozi na uchochezi. ´Ubaadah bin as-Swaamitw (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alituita kuja kula kiapo ambapo tukampa kiapo cha kusikiliza na kutii kwa kupenda kwetu na kutokupenda kwetu, katika kipindi chepesi na kigumu, pindi mtu anapopendelewa juu yetu na kwamba tusivutane na watawala mpaka pale mtakapoona ukafiri wa wazi ambao tuna dalili kwao kutoka kwa Allaah.”[1]
Kuna Hadiyth nyingi na zenye kutambulika katika maudhui haya. Miongoni mwazo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Atakayefanya uasi dhidi ya mtawala akafa, basi amekufa kifo cha kipindi cha kikafiri.”[2]
Kama tulivosema kuna Hadiyth nyingi na zenye kutambulika katika maudhui haya.
Ni uasi pia kule kutaja mabaya ya kiongozi, kuwatukana, kuwakemea mbele ya umati wa watu na kuwatweza. Mambo kama haya yanapelekea katika khatari kubwa na madhara makubwa ikiwa ni pamoja vilevile na watawala kuasiwa na yanapelekea katika uasi wa kimatendo. Uasi wa kimatendo unapelekea kumwagika kwa damu, heshima kuvunjwa, njia kufungwa na kutandaa kwa khofu.
Enyi wanafunzi! Mcheni Allaah juu ya Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)! Msihadaike na watu wenye mirengo ya kisiasa. Nchi yetu[3] ni ya Kiislamu. Inatilia umuhimu suala la Tawhiyd, inahukumu kwa Shari´ah ya Allaah na inaeneza uadilifu. Tunamuomba Allaah aiongoze mahakama yake katika kila kheri. Hatusemi kwamba haina makosa. Hapana shaka kwamba makosa yapo, lakini makosa haya yanatakiwa kurekebishwa kwa njia yenye manufaa na si yenye madhara, kama mfano wa nasaha za siri na mfano wa hayo.
Sipendi kuingia ndani zaidi katika mlango huu. Ni ishara tu tunazoashiria na kulenga juu ya makosa ya watu wa Bid´ah. Huenda Allaah akamwongoza kwazo na akatulinda na shari za Bid´ah na watu wa Bid´ah – kwani hakika Yeye ni Mwingi wa kutoa na mkarimu.
[1] al-Bukhaariy (7056) na Muslim (1709).
[2] al-Bukhaariy (7053) na Muslim (1849).
[3] Saudi Arabia – Allaah aikinge na kila ovu.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2LeH7Kv
via IFTTT
38. Swalah ya ijumaa nyuma ya watawala
Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
“Swalah ya ijumaa nyuma yao na nyuma ya magavana wao inafaa na ni timilifu na ni Rak´ah mbili. Yule mwenye kuirudi ni mtu wa Bid´ah mwenye kuyaacha mapokezi na anaenda kinyume na Sunnah. Hapati chochote katika fadhila za ijumaa midhali haonelei kuwa ni sahihi kuswali swalah ya ijumaa nyuma ya viongozi sawa wawe wema au waovu. Sunnah ni kuswali Rak´ah mbili pamoja nao na kuonelea kuwa ni timilifu. Usiwe na shaka kwenye kifua chako juu ya hilo.”
MAELEZO
Swalah ya ijumaa, swalah za mkusanyiko na swalah za ´iyd mbili ni lazima kuziswali nyuma ya watawala. Yule mwenye kuonelea kwamba kuswali swalah ya ijumaa nyuma ya kiongozi aliyepo si sahihi na kwamba inasihi tu kuswali nyuma ya ambaye amekingwa na makosa kutoka katika familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama ilivyo kwa Shiy´ah na wale wafuasi wao, ni mpotevu. Haifai kuiga fikira hii. Haifai kutilia shaka kwamba swalah ya ijumaa nyuma ya mtawala Rak´ah mbili ni sahihi, ni mamoja mtawala huyo ni mwema au mwovu. Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2GOisXV
via IFTTT
37. Zakaah wanapaswa kupewa watawala
Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
“Inafaa na ni sahihi kuwapa zakaah sawa wakiwa wema au waovu.”
MAELEZO
Miongoni mwa haki za watawala ni kuwapa zakaah. Zakaah wanatakiwa kupewa wao au manaibu wao na si wengineo. Yule mwenye kutoa zakaah kumpa mwengine asiyekuwa wao basi ni lazima kwake kuilipa tena.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2V4Kh8p
via IFTTT
Jumatatu, 29 Aprili 2019
08. Inafaa kwa mwanamke mjamzito na mwenye kunyonyesha kuacha kufunga
Swali 08: Inafaa kwa mwanamke mjamzito na mwenye kunyonyesha kuacha kufunga? Je, ni lazima kwao kulipa au kuna kafara juu ya kuacha kwao kufunga?
Jibu: Mwanamke mjamzito na mwenye kunyonyesha swawm ikiwa ngumu kwao basi ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa wao kula. Hata hivyo ni lazima kulipa pindi watapoweza kufanya hivo kama mfano wa mgonjwa. Wapo wanachuoni wenye kuonelea kwamba inatosha kwao kulisha masikini kwa kila siku moja walioacha kufunga. Lakini hata ni maoni dhaifu yaliyoshindwa nguvu. Maoni ya sawa ni kwamba ni lazima kwao kulipa kama anavofanya msafiri na mgonjwa. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ
“Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu au yuko safarini, hivyo basi akamilishe idadi katika siku nyinginezo.” (02:184)
Kumefahamisha juu ya hayo Hadiyth ya Anas bin Maalik al-Ka´biy aliyesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah amemwondoshea msafiri funga na nusu ya swalah na mjamzito na mnyonyeshaji swawm.”
Wameipokea wale watano.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2ZIjBZB
via IFTTT
17. Ni ipi hukumu ya aliyechelewesha kulipa mpaka akaingiliwa na Ramadhaan nyingine?
Swali 17: Ni ipi hukumu ya ambaye aliacha kulipa swawm ya Ramadhaan mpaka akaingiliwa na Ramadhaan ilio baada yake ilihali hakuwa na udhuru? Je, inatosha kwake kutubia pamoja na kulipa au ni lazima vilevile kutoa kafara?
Jibu: Ni lazima kwake kutubia kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na kulisha masikini kwa kila siku moja aliyoacha pamoja na kulipa funga. Kafara ni nusu ya pishi kwa kipimo cha ile pishi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kile chakula kilichozoeleka kuliwa katika nchi kama mfano wa tende, ngano, mchele au vyenginevyo. Kiwango chake ni 1,5 kg kwa njia ya kukadiria. Hana kafara nyingine zaidi ya hiyo. Hivo ndivo walivyofutu baadhi ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) akiwemo Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa).
Lakini kama alikuwa na udhuru kwa mfano mgonjwa au msafiri au mwanamke alikuwa na udhuru kama mfano wa ujauzito au kunyonyesha ambapo angelifunga basi angelihisi uzito, hakuna kinachomlazimu zaidi ya kulipa.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2ZJgrEP
via IFTTT
Kuna wakati wa kupokelewa du´aa baada ya swalah za faradhi?
Swali: Ibn-ul-Qayyim ametaja katika “ad-Daa´ wa ad-Dawaa´” kwamba baada ya swalah za faradhi kuna wakati ambapo du´aa inakuwa ni yenye kupokelewa. Hayo yanakuwa vipi? Je, inakuwa baada ya nyuradi za Kishari´ah, baada ya Raatibah zake au lini?
Jibu: Mimi sijui haya katika Sunnah kwamba kuna du´aa baada ya swalah isipokuwa zile zilizofungamana na swalah kama kufanya Istighfaar mara tatu baada ya kutoa salamu. Kwa sababu zinafungamana na swalah. Kuhusu du´aa inakuwa kabla ya salamu. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipotaja Tashahhud akasema:
“Kisha achague katika du´aa anayotaka.”
Du´aa ilioko kati ya adhaana na Iqaamah ni jambo lisilokuwa na shaka kwamba ni yenye uwezekano mkubwa wa kuitikiwa. Ni mamoja mtu anaiomba katika swalah ya Sunnah au baada ya swalah.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2GFUM81
via IFTTT
36. Haki za watawala
Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
Kiongozi kugawa fai na kusimamisha adhabu ni mambo yenye kuendelea. Hakuna yeyote aliye na haki ya kuwaponda wala kupambana nao.”
MAELEZO
Hapa Imaam Ahmad kabainisha haki za watawala na kwamba wao ndio wenye aki ya kugawa fai na kusimamisha adhabu. Haifai kwa yeyote kujifanyia chochote kwa mikono yake katika mambo haya. Ni katika haki zao. Kadhalika inahusiana na kumsaidia yule mwenye kukandamizwa, kutatua magomvi na mfano wa hayo.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2GF5KdN
via IFTTT
35. Jihaad ni yenye kuendelea mpaka siku ya Qiyaamah
Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
“Vita ni vyenye kuendelea pamoja na viongozi wema na waovu mpaka siku ya Qiyaamah na haitakiwi kuachwa.”
MAELEZO
Vita ni vyenye kuendelea pamoja na viongozi, bi maana watawala, na swalah ya ijumaa na swalah za ´iyd mbili ni wajibu kwa kila yule ambaye yuko chini yake. Ni lazima kwao kupigana bega kwa bega pamoja naye dhidi ya makafiri na waasi. Hayo yameamrishwa na Allaah (´Azza wa Jall) pale aliposema:
وَإِن طَائِفَتَانِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ اقْتَتَلُوا فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا ۖ فَإِن بَغَتْ إِحْدَاهُمَا عَلَى الْأُخْرَىٰ فَقَاتِلُوا الَّتِي تَبْغِي حَتَّىٰ تَفِيءَ إِلَىٰ أَمْرِ اللَّـهِ
“Ikiwa makundi mawili ya waumini yatapigana, basi suluhisheni kati yao. Endapo mojawapo likikandamiza jengine, basi piganeni na ambalo linakandamiza mpaka lielemee katika amri ya Allaah.”[1]
Kiongozi ambaye uongozi wake umekubaliwa na waislamu – ni mamoja ameupata kwa mashauriano au kimabavu – ni lazima atiiwe. Ni lazima vilevile kupambana chini ya uongozi wake. Yule mwenye kufanya upungufu katika hayo basi ataulizwa mbele ya Allaah, kwa sababu ameacha jambo la wajibu.
[1] 49:09
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2LazEfK
via IFTTT
34. Kuwatii watawala
Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
“Viongozi na kiongozi wa waumini wanatakiwa kusikilizwa na kutiiwa sawa wawe wema au waovu. Yule mwenye kuchukua ukhaliyfah, watu wakakusanyika juu yake na wakaridhika nao na yule mwenye kuchukua uongozi kwa mabavu mpaka akawa khaliyfah anaitwa kiongozi wa waumini.”
MAELEZO
Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amebainisha kwamba ni lazima kwa kila muislamu kumtii mtawala, ni mamoja mtawala huyo ni mwema au mwovu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Sikiliza na tii japokuwa utatawaliwa na mja wa kihabeshi aliyeadhibiwa.”[1]
Katika upokezi mwingine imekuja:
“…kana kwamba kichwa chake ni kama zabibu.”[2]
Kuna Hadiyth nyingi kuhusiana na hilo ambazo mtu anatakiwa kuzirjelea.
[1] Muslim (648).
[2] al-Bukhaariy (693).
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2IT8h83
via IFTTT
Jumapili, 28 Aprili 2019
Mambo yanayofaa Kufanywa na Mwenye Kufunga
http://bit.ly/2J1tNqa i live islam
Mambo Sita Yanayobatilisha Swawm
http://bit.ly/2IO3Afo i live islam
Mambo yenye Umuhimu kwa Ujumla wa Kutekeleza ´Ibaadah ya Swawm (Kufunga)
http://bit.ly/2J1tI5Q i live islam
Mwanamke Mja Mzito (Mwenye Mimba) au Mwenye Kunyonyesha
http://bit.ly/2IMDtFN i live islam
Yanayomlazimu Mtu Mzima na Mwenye Ugonjwa wa kuendelea
http://bit.ly/2J1xJao i live islam
Nani Anawajibika Kufunga?
http://bit.ly/2IMYiB6 i live islam
20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh YAFUATAYO NI MAJINA YA MASWAHABA WANAWAKE (RADHI ZA ALLAAH...
-
Dalili 18 zinazoashiria una ujauzito wa mtoto wa kiume Awali ya yote nitoe pongezi kwa mama K na Baba K wote popote walipo kwa kazi nzuri ...
-
Assallaaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Naam, Ndugu zangu katika Imaani, Siku chache zimebaki kwa ajili ya Vijana wetu wanaosoma Elim...