Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh
Swalaah ya Ijumaa ni Fardhw ‘Ayn (Fardhi kwa kila mtu mwanamme) wala haijuzu kuiacha kwa sababu ya kazi au masomo na sababu kama hizo.
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
“Na yeyote anayemcha Allaah; Atamjaalia njia ya kutoka (shidani).”
[Rejea Kitab Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/184)]
Ndugu zangu katika Imaani, Swalaah ya Ijumaa ni fardhi kwa kila mwanamme mwenye kukafilika katika ‘Ibaadah, mkazi, wala haikupasi kuikhalifu kwa sababu ya kazi hata kama mwajiri wako atakukataza.
[Rejea Kitab Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/185)]
Kwahiyo ndugu zangu katika Imaani ni wajibu kwa wanaume kuswali Ijumaa pamoja na ndugu zao Waislamu katika nyumba za Allaah (Misikitini). Ama wanawake wao hawana Ijumaa na ni wajibu kwao kuswali Adhuhuri.
[Rejea Kitab Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/196)]
Na Allaah anajua zaidi
from fisabilillaah.com http://bit.ly/2CDjMvY
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni