Inajuzu kusimamisha Swalaah ya Ijumaa hata kama idadi imepunguka chini ya watu arubaini kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ
“Enyi walioamini! Inaponadiwa kwa ajili ya Swalaah siku ya Ijumaa, kimbilieni kumdhukuru Allaah.” [Al-Jumu’ah: 9]
[Rejea Kitab Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/215)]
Naam ama mtu anayepitwa na Rakaa katika Swalaah ya Ijumaa, na akaipata Rakaa nyingine, basi aiswali ile Rakaa (iliyompita) na hivyo atakuwa amepata Ijumaa kwa sababu limesihi kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hilo.
[Rejea Kitab Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/225)]
Imaam kuwasalimia Maamuma kabla ya Khutbah
Ni Sunnah kwa Khatwiyb (wa Ijumaa) kuwasalimia maamuma anapopanda minbari kabla ya kukaa kitako (kusubiri Adhana).
[Rejea Kitab Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/234)]
Kuongea katika Khutbah
Maongezi ya watu wakati Imaam anatoa khutbah siku ya Ijumaa ni haramu.
Kwahiyo maamuma wanatakiwa wawe watulivu na wasikivu katika Khutbah na wajiepushe sana na maongezi na shughuli zingine kama kuchezea simu nakadhalika.
[Rejea Kitab Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/240)]
Na pia haifai kusalimiana katika Khutbah wala kumtakia rahma mtu aliepiga chafywa kwasababu kauli iliyo sahihi ya ‘Ulamaa ni kwamba, haijuzu kumuombea rahmah anayepiga chafya wala kurudisha salaam wakati Imaam (Khatwiyb) anakhutubia.
[Rejea Kitab Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/242)]
Ama tukija katika swalah za Sunnah, Ukweli ni kwamba hakuna Sunnah za Rawaatib(kiwango) maalumu za qabliyyah (kabla ya Swalaah) katika Swalaah ya Ijumaa.
kwahiyo mtu atatakiwa kuswali swalah za Sunnah rakaa awezavyo mpaka Imaam aingie.
Lakini anaweza kuswali Sunnah atakazo kabla ya kuingia Imaam.
[Rejea Kitab Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/249)]
Na Allaah anajua zaidi
from fisabilillaah.com http://bit.ly/2Thn5yk
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni