Translate

Ijumaa, 28 Desemba 2018

Mafunzo ya Swalah- Kuanza Kuswali

                                            Kwanza Kabisa Mswaliji anatakiwa Kuelekea Qiblah 


Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh

Naam,kuanzia sasa tutaanza kujifunza namna ya kuswali hatua kwa hatua


Mswalaji atanatakiwa kuelekea Qiblah ambapo ni Ka´bah popote alipo.

Anatakiwa kuuelekeza Qiblah mwili wake wote na huku anuie kwa moyo wake kutekeleza swalah ile anayotaka kuswali - ni mamoja iwe ya faradhi au ya Sunnah - na asitamke nia kwa ulimi wake (Niyah ni Moyoni).

Kwa sababu kutamka nia kwa ulimi wake haikuwekwa katika Shari´ah.

Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakupatapo kutamka nia wala Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum).

Imesuniwa kuweka Sutrah ambapo ataswali kwa kuielekea. Hili linamuhusu imamu au anayeswali peke yake.

Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kufanya hivo. Takbiyrat-ul-Ihraam, kunyanyua mikono wakati wa Takbiyrah na kufunga mikono

Mswaliji alete Takbiyrat-ul-Ihraam kwa kusema "Allaahu Akbar" na huku ni mwenye kutazama pahali pa kusujudia.

Pale anaposema "Allaahu Akbar" anatakiwa ainyanyue mikono yake sawa na mabega yake au na masikio yake.

Kisha Mswaliji anatakiwa aiweke mikono yake juu ya kifua chake, yaani  kitanga cha kulia akiweke juu ya kitanga cha kushoto.

Hilo ni jambo limethibiti kutoka kwa Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

                                                 
                                                           Du´aa ya kufungulia swalah 

Imesuniwa kusoma du´aa ya kufungulia swalah.

Nayo ni kusema

ال ابعد بيين ب خطا ي ك ا ابعدت ب املش ق املغ ب، ال نقين من خطا ي ك ا ينقى الث ب األبيض من الدنس، ال اا ين من خطا ي ابملا الث ج الربد

"Allaahumma baa´id bainiy wa baina khatwaayaayaa kamaa ba´atta bainal-Mashriq wal-Maghrib. Allaahumma naqqiniy min khatwaayaayaa kamaa yunaqqaa thawb al-Abyadhw minad-Danas. Allaahumma ighsilniy min khatwaayaayaa bil-Maa´ wath-Thalj wal-Barad... " 


"Ee Allaah! Niweke mbali na madhambi yangu kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi. Ee Allaah! Nitakase kutokamana na madhambi yangu kama vile inavyotakaswa nguo nyeupe na uchafu. Ee Allaah! Nisafishe kutokamana na madhambi yangu kwa theluji na kwa maji na kwa barafu... "


 Vilevile akipenda badala ya du´aa hiyo anaweza kusoma ifuatayo:

وب انك ال حب دك تبا ك امسك تعا دك ال لو اريك

 "Subhaanak Allaahumma wa bihamdik, wa tabaaraka-ismuk, wa ta´aalaa jadduk, wa laa ilaaha ghayruk."


"Utakasifu na himdi zote ni Zako, limetukuka jina Lako, utukufu ni Wako na hapana mungu wa haki asiyekuwa Wewe."

Akisoma du´aa zingine za kufungulia swalah mbali na hizo mbili ni sawa. Lililo bora zaidi ni wakati fulani asome hii na wakati mwingine asome nyingine. Huku ni kufuata kikamilifu zaidi. Baada ya hapo aseme:

"A´udhu billaahi min ash-Shaytwaan ar-Rajiym. Bismillaahi ar-Rahmaan ar-Rahiym." 

"Ninajilinga kwa Allaah kutokana na shaytwaan aliyetiwa mbali na Rahmah zaa Allaah, kwa jina la Allaah Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu." Kisha asome Suurah "al-Faatihah".

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Hana swalah yule ambaye hakusoma mama wa Kitabu."al-Bukhaariy (714), Muslim (595), at-Tirmidhiy (230) na an-Nasaa´iy (901).

Atapomaliza kuisoma aseme:

"Aamiyn".

Aseme hivyo kwa sauti ya juu ikiwa ni katika swalah za kusoma kwa sauti.


Baada ya hapo Mswaliji Aakimaliza kusoma "al-Faatihah" asome kile kitachomkuwa chepesi katika Quraan (yaani asome Surah yoyote anayoitaka)



Na  Allaah  anajua  zaidi

from fisabilillaah.com http://bit.ly/2ETkLu3
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...