MAANA YA MASIKU MEUPE
Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh
Yameitwa ‘Biydhw’ (meupe) sababu usiku wa siku hizo hung'aa kutokana na mwanga wa mwezi. Ayyaam Al-Biydhw (Masiku Meupe) tarehe zake ni 13, 14 na 15 katika kila mwezi wa kalenda ya Kiislamu.
عَنْ جريرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَن النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيهِ وَسَلَّمَ قَالَ : ((صِيَامُ ثَلاثَةِ أَيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ صِيَامُ الدَّهْرِ ، أَيَّامُ الْبِيضِ صَبِيحَةَ ثَلاثَ عَشَرَةَ وَأَرْبَعَ عَشَرَةَ وَخَمْسَ عشَرَةَ))
Imepokelewa kutoka kwa Jariyr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabii (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Swiyaam (kufunga) siku tatu kila mwezi ni sawa na swiyaam ya dahari (milele!) Na masiku meupe ni tarehe kumi na tatu, kumi na nne na kumi na tano [13, 14, 15]))
[An-Nasaaiy (2420) na ameisahihisha Al-Abaaniy katika Swahiyh At-Targhiyb (1040) ]
عن أبي ذر رضي الله عنه: قال لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((يَا أَبَا ذَرٍّ ، إِذَا صُمْتَ مِنَ الشَّهْرِ ثَلاثَةَ أَيَّامٍ فَصُمْ ثَلاثَةَ عَشَرَ وَأَرْبَعَةَ عَشَرَ وَخَمْسَةَ))
Imepokelewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia:
((Ee Abu Dharr! Endapo utafunga (swiyaam) siku tatu za kila mwezi, basi funga siku ya 13, ya 14, na ya 15))
[Imepokewa na At-Tirmidhiy na kasema Shaykh Al-Albaaniy kuwa ni Swahiyh ]
قال صلى الله عليه وسلم: ((أَلا أُخْبِرُكُمْ بِمَا يُذْهِبُ وَحَرَ الصَّدْرِ صَوْمُ ثَلاثَةِ أَيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْر))
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Je, nikujulisheni jambo litakaloondosha uovu wa moyo? Ni swiyaam (kufunga) siku tatu kila mwezi))
[An-Nasaaiy 2/2386 na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh An-Nasaaiy (2249)]
Asw-Swuyuutwiy (Rahimahu Allaah) amesema katika An-Nihaayah: "Uovu wa moyo ni; udanganyifu, wasiwasi, na imesemwa pia ni uhasidi, chuki, na imesemwa pia uadui na imesemwa ghadhabu".
Na Allaah anajua zaidi
https://ift.tt/2uhSFRY i live islam
Inshallah mung akubarik akh
JibuFutaUbora wa kufunga siku hizo ni upi?
JibuFuta