Swali
Kuna mwanamke aliacha kufunga Ramadhaan kwa muda wa miaka kumi kwa sababu ya mimba na kunyonyesha kwa sababu ya kuchelea afya na mtoto wake. Baada ya hapo akatubia. Je, tawbah inatosha au kuna kitu kingine kinachomlazimu?
Jibu
Ndio. Tawbah inatosha kwa sharti alipe yale masiku anayodaiwa. Akilipa masiku anayodaiwa itatosha.
Halazimiki kulisha kwa mujibu wa maoni yaliyo na nguvu miongoni mwa maoni mbalimbali ya wanachuoni. Wako wanachuoni wanaosema mtu akila na akachelewesha kulipa mpaka akaingiliwa na Ramadhaan ya pili bila udhuru wowote basi ni wajibu kwake kulipa na kulisha.
Lakini maoni sahihi ni kwamba halazimiki kulisha na kwamba kufunga kunamtosha.
Rejea Kitab Al-Liqaa' ash-Shahriy (44)
https://ift.tt/2utUWd3 i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni