Swali: Tofauti iliopo juu ya kumpa udhuru mjinga ni miongoni mwa mambo ambayo wanachuoni wametofautiana?
Jibu: Ni masuala makubwa. Msingi ni kwamba hapewi udhuru yule ambaye anaishi kati ya waislamu. Yule aliyefikiwa na Qur-aan na Sunnah hapewi udhuru. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
هَـٰذَا بَلَاغٌ لِّلنَّاسِ
“Hii ni ufikishwaji wa ujumbe kwa watu.” (14:52)
وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ
“Nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayomfikia.” (06:19)
Ambaye kafikiwa na Qur-aan na Sunnah si mwenye kupewa udhuru. Yaliyomfikia ni kutokana na kufanya kwake mchezo na kutokujali.
Swali: Lakini mtu anaweza kusema kwamba ni miongoni mwa mambo ambayo wanachuoni wametofautiana?
Jibu: Hapana, hakuna tofauti. Isipokuwa katika mambo nyeti ambayo kweli yanaweza kujificha. Kama mfano wa kisa cha yule aliyewaambia watu wake: “Nichomeni moto.”
from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2YwN0VY
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni