Kufupisha kumswalia Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa Mfumo wowote Haijuzu
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amejibu kuhusu swali la hukmu ya kufupisha kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
“Kama ilivyoamrishwa kumswalia Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwenye Swalaah katika Tashahhud, na imeamrishwa katika kutoa khutbah na kuomba Du’aa na kuomba maghfirah, na baada ya Adhaan, na wakati wa kuingia na kutoka Msikitini, na wakati wa kumtaja katika hali nyinginezo, hivyo basi ni muhimu zaidi kufanya hivyo katika kumtaja jina lake katika kitabu, barua, makala n.k.
Kwa hiyo, imeamrishwa kuandika Swalaah na Salaam kwa ukamilifu ili kutimiza amri ya Allaah ('Azza wa Jalla) Aliyotuamrisha na ili msomaji apate kukumbuka kutaja kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anapoisoma. Hivyo tusiandike Swalaah na Salaam kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kifupi kama kuandika (S) au (S.A.W.) n.k. au mfumo wowote ambao watu wanatumia kwa sababu inakwenda kinyume na maamrisho ya Allaah na Kitabu Chake Anaposema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٥٦﴾
Enyi walioamini mswalieni na msalimieni kwa mamkizi ya amani na kwa tasliymaa. [Al-Ahzaab 33:56]
Juu ya hivyo, ni kwamba kusudio halitimii na ni kukosa fadhila zake (za kumswalia Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na huenda msomaji asitanabahi au asifahamu (hizo herufi) maana zake zilokusudiwa. Na juu ya hivyo pia kufupisha kwa herufi zimechukizwa na Ahlul-‘Ilm na wametahadharisha hivyo.”
[Majmuw’ Al-Fataawaa Wa Rasaail Al-Imaam Ibn Baaz (2/397 – 399)]
https://ift.tt/2uJHNNb i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni