Translate

Alhamisi, 28 Machi 2019

Misingi ya Fiqh'i

▶MISINGI YA FIQHI◀

Assallaam Aleykum Warahmatullah Wabarakatuh Ndugu zangu katika Imaani.

🖌Naam ndugu zangu katika Imani,Baada ya kueleza katika Darsa iliyopita Maana ya FIQH ki Lugha na Maana ya Wanachuoni wa Fani hii vile vile kutaja MISINGI YA FIQ-HI,muda huu tunaendelea katika kueleza Maana ya Kila Msingi katika Misingi ya Elimu hii ya FIQH.

1⃣QUR-AN

➡Qur-an Tukufu ni kitabu kilichokusanya maneno matukufu ya Mwenyezi Mungu alichoshushiwa Mtume wa mwisho, Nabii Muhammad kupitia kwa Malaika Jibril ili kiwe ni sheria na muongozo kwa wanadamu wote.

2⃣HADITH(SUNNAH)

➡Hadith ni tafsiri sahihi na ufafanuzi kamili wa Qur-ani Tukufu uliotolewa na Bwana Mtume Muhammad (Swalla Allaahu Aleyhi wa Sallaam)kwa njia ya vitendo, maneno na "IQRAARI".

🖌"IQRAARI" ni kitendo cha Bwana Mtume kumuona mtu akitenda jambo fulani, kisha Mtume asitoe maelekezo yoyote ya kukemea au kukataza. Ukimya huu wa Mtume hutafsirika kuwa jambo lile linafaa kwani Mtume hawezi kulinyamazia jambo baya.

3⃣IJMAAI

➡Ijmaai maana yake ni kongamano na makubaliano ya wanazuoni wa kiislamu baada ya kuja Mtume juu ya jambo au suala ambalo halikuelezwa kwa uwazi ndani ya Qur-ani au hadithi

4⃣QIYAASI

➡Qiyaasi maana yake ni mizani ya kulipima jambo au suala ambalo halina ufafanuzi ndani ya Qur-ani au hadithi na jambo au suala lililotajwa ndani ya Qur-ani au Hadithi, kwa kulingana sababu.

🖌Kwa ufupi hizi ndizo maana nyepesi na za awali za misingi hii minne ambayo ndio chimbuko la elimu hii ya sheria ya Kiislamu, elimu ya FIQH.

🖌ANGALIZO

➡Misingi hii Minne Miwili ya Mwanzo Qur an na Sunna Wanawachuoni wote wamekubaliana katika Misingi hiyo.

➡Ama Namba 3 - 4 Wanawazuoni wametofautiana katika Misingi hii.

Na Allaah anajua zaidi



https://ift.tt/2Ozvz2K i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...