Swali: Siku ya ijumaa nilioga kwa ajili ya ijumaa na nikanuia kutawadha baada ya kumaliza kuoga. Lakini hata hivyo nikasahau kutawadha na nikaswali ijumaa. Ni kipi kinachonilazimu; nirudi kuswali tena au nifanye nini?
Jibu: Mosi: Ni lazima kwa mtu kujua kwamba josho la ijumaa ni wajibu. Yule ambaye hakuoga basi amemuasi Allaah na Mtume wake. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kuoga siku ya ijumaa ni wajibu juu ya kila mwenye kuota.”
Pili: Je, josho hili ni kwa ajili ya hadathi au ni pasi na hadathi? Sio kwa ajili ya hadathi. Ikiwa sio kwa ajili ya hadathi basi hadathi haikuondoka kwayo. Kwa sababu hadathi inaondoka pale ambapo kuoga kunakuwa kwa ajili ya hadathi. Ikiwa josho hili hadathi haikuodoka kwalo na mtu akaswali ijumaa pasi na wudhuu´, basi arudi kuiswali aina ya Dhuhr. Kwa sababu hakunuia hadathi. Lakini angelioga kwa ajili ya janaba na asitawadhe, basi swalah yake ni sahihi. Kwa sababu inafaa kwa mtu kuswali kwa josho la janaba hata kama hakutawadha. Lakini kwa sharti asukutue na apalizie. Kujengea juu ya haya tunamwambia ndugu muulizaji: lililo salama zaidi kwako ni kurudi kuiswali swalah ya ijumaa aina ya Dhuhr. Wewe – Allaah akitaka – umepata thawabu. Kwa sababu hukukusudia kuswali pasi na wudhuu´.
from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2YxFlH8
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni