Translate

Alhamisi, 28 Machi 2019

066-Asbaabun-Nuzuwl: At-Tahriym: Aayah 1-5

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

066-At-Tahriym Aayah 1-5

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكَ ۖ تَبْتَغِي مَرْضَاتَ أَزْوَاجِكَ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١﴾

1. Ee Nabiy! Kwanini unaharamisha kile Alichokuhalalishia Allaah? Unataka kuwaridhisha wake zako; na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

قَدْ فَرَضَ اللَّـهُ لَكُمْ تَحِلَّةَ أَيْمَانِكُمْ ۚ وَاللَّـهُ مَوْلَاكُمْ ۖ وَهُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ﴿٢﴾

2. Allaah Amekwishakufaridhishieni ukomboaji kwa viapo vyenu, na Allaah ni Mola wenu Naye Ndiye Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.

 

وَإِذْ أَسَرَّ النَّبِيُّ إِلَىٰ بَعْضِ أَزْوَاجِهِ حَدِيثًا فَلَمَّا نَبَّأَتْ بِهِ وَأَظْهَرَهُ اللَّـهُ عَلَيْهِ عَرَّفَ بَعْضَهُ وَأَعْرَضَ عَن بَعْضٍ ۖ فَلَمَّا نَبَّأَهَا بِهِ قَالَتْ مَنْ أَنبَأَكَ هَـٰذَا ۖ قَالَ نَبَّأَنِيَ الْعَلِيمُ الْخَبِيرُ﴿٣﴾

 

3. Na pale Nabiy alipompa mmoja wa wake zake jambo la siri, na huyo mke alipoipasha habari na Allaah Akamdhihirishia (Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم), akataarifu baadhi yake na akaacha nyingine. Basi alipomjulisha hayo, akasema: “Nani aliyekujulisha haya?” Akasema: “Amenijulisha Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.”

 

 

إِن تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا ۖ وَإِن تَظَاهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ مَوْلَاهُ وَجِبْرِيلُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ بَعْدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ﴿٤﴾

4. Ikiwa nyinyi wawili mtatubia kwa Allaah (ni kheri kwenu) kwani kwa hakika nyoyo zenu zimeelemea (yanayomchukiza Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم). Na mkisaidiana dhidi yake, basi hakika Allaah Ndiye Mlinzi Msaidizi wake na Jibriyl na Waumini wema, na zaidi ya hayo, Malaika pia watasaidia.

 

عَسَىٰ رَبُّهُ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبْدِلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِّنكُنَّ مُسْلِمَاتٍ مُّؤْمِنَاتٍ قَانِتَاتٍ تَائِبَاتٍ عَابِدَاتٍ سَائِحَاتٍ ثَيِّبَاتٍ وَأَبْكَارًا﴿٥﴾

 

5. Akikutalikini, asaa Rabb Wake Akambadilishia wake bora kuliko nyinyi; Waislamu, Waumini, watiifu na wanyenyekevu, wanaotubia, wenye kufanya ‘ibaadah, wanaofunga Swiyaam au wanaohajiri kwa ajili ya Allaah, wajane, na walio bikra.

 

 

Sababun-Nuzuwl (1):

 

حَدَّثَنِي الْحَسَنُ بْنُ مُحَمَّدِ بْنِ صَبَّاحٍ، حَدَّثَنَا حَجَّاجٌ، عَنِ ابْنِ جُرَيْجٍ، قَالَ زَعَمَ عَطَاءٌ أَنَّهُ سَمِعَ عُبَيْدَ بْنَ عُمَيْرٍ، يَقُولُ سَمِعْتُ عَائِشَةَ  رضى الله عنها   أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَمْكُثُ عِنْدَ زَيْنَبَ ابْنَةِ جَحْشٍ، وَيَشْرَبُ عِنْدَهَا عَسَلاً، فَتَوَاصَيْتُ أَنَا وَحَفْصَةُ أَنَّ أَيَّتَنَا دَخَلَ عَلَيْهَا النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَلْتَقُلْ إِنِّي أَجِدُ مِنْكَ رِيحَ مَغَافِيرَ، أَكَلْتَ مَغَافِيرَ فَدَخَلَ عَلَى إِحْدَاهُمَا فَقَالَتْ لَهُ ذَلِكَ، فَقَالَ ‏"‏ لاَ بَلْ شَرِبْتُ عَسَلاً عِنْدَ زَيْنَبَ ابْنَةِ جَحْشٍ وَلَنْ أَعُودَ لَهُ ‏"‏‏.‏ فَنَزَلَتْ:‏ ((‏يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّهُ لَكَ‏)) إِلَى: ((إِنْ تَتُوبَا إِلَى اللَّهِ‏))‏ لِعَائِشَةَ وَحَفْصَةَ ‏  ((وَإِذْ أَسَرَّ النَّبِيُّ إِلَى بَعْضِ أَزْوَاجِهِ‏))‏ لِقَوْلِهِ ‏"‏ بَلْ شَرِبْتُ عَسَلاً ‏"‏‏.‏

 

Amenihadithia Al-Hassan bin Muhammad bin As-Swabbaah amenihadithia Hajaaj kutoka kwa Ibn Jurayj amesema: ‘Atwaa alisema kuwa alimsikia ‘Ubayd bin ‘Umayr akisema nimemsikia ‘Aaishah (Radhwiya Allahu ‘anhaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikaa na kushinda kwa Zaynab bint Jahsh na huwa akinywa kwake asali. Mimi (‘Aaishah) nikakubaliana na Hafswah kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) atakapoingia kwa mmoja wetu basi   aseme: “Mimi nasikia kwako harufu ya Maghaafiyr (gundi la kwenye mti), je umekula Maghaafiyir?” Akafika kwa mmoja wao na akamwambia yeye hivyo. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  akasema: ((Hamna neno nilikunywa asali kwa Zaynab bint Jahsh na sitorudui kufanya hivyo tena)). Baada ya hapo ikateremka:

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكَ ۖ

 

1. Ee Nabiy! Kwanini unaharamisha kile Alichokuhalalishia Allaah?

 

Hadi

إِن تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ

4. Ikiwa nyinyi wawili mtatubia kwa Allaah…  

 

(imekusudiwa ‘Aaishah na Hafswah)

 

Na ikateremka tena:

وَإِذْ أَسَرَّ النَّبِيُّ إِلَىٰ بَعْضِ أَزْوَاجِهِ حَدِيثًا  

3. Na pale Nabiy alipompa mmoja wa wake zake jambo la siri,  

 

Kuhusu kauli yake: ((Bali nilikunywa asali))

 

[Al-Bukhariy Kitaab Atw-Twalaaq]

 

 

Sababun-Nuzuwl (2):

 

 عَنْ أَنَسٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَتْ لَهُ أَمَةٌ يَطَؤُهَا فَلَمْ تَزَلْ بِهِ عَائِشَةُ وَحَفْصَةُ حَتَّى حَرَّمَهَا عَلَى نَفْسِهِ فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ ‏: ‏ يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّهُ لَكَ   ‏ إِلَى آخِرِ الآيَةِ ‏.‏

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na kijakazi ambaye alikuwa akimwingilia, lakini ‘Aaishah na Hafswah hawakumuacha mpaka  akafanya kuwa ni haraam kwa nafsi yake, Allaah Akateremsha:

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكَ ۖ تَبْتَغِي مَرْضَاتَ أَزْوَاجِكَ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١﴾

1. Ee Nabiy! Kwanini unaharamisha kile Alichokuhalalishia Allaah? Unataka kuwaridhisha wake zako; na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.

 

[An-Nasaaiy, Tafsiyr Ibn Kathiyr (Juz 4 uk 386), Al-Hakam (Juz 2 uk 493) na akasema ipo katika shuruti za Muslim na ikathibitishwa na Adh-Dhahabiy]

 

 

Pia:

 

Kutoka kwa Ibn ‘Abbas (Radhwiya Allaahu ‘ahumaa) amesema: "Aayah

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكَ ۖ تَبْتَغِي مَرْضَاتَ أَزْوَاجِكَ  

1. Ee Nabiy! Kwanini unaharamisha kile Alichokuhalalishia Allaah? Unataka kuwaridhisha wake zako;  

 

imeteremka hii kuhusu kijakazi wake."

 

[Majma’ Az-Zawaaid (Juz 7 uk 126) Imepokewa na Al-Bazzar kwa Isnaad mbili na At-Twabaraaniy na wapokezi wa Al-Bazzar ni wapokezi sahihi isipokuwa mmoja ambaye ni Bishri bin Adam nae ni Thiqqha (mwaminifu)].

 

 

Pia:

 

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  kumwambia Hafswa, “Usimwambie mtu kwa hakika Ummu Ibraahiym ni haraam kwangu.” Hafswah akasema: Unakiharamisha Alichokuhalalishia Allaah kwako. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  akasema, “Wallahi sitomkaribia.” Akasema: Hivyo hakumkurubia hadi alipomwambia ‘Aaishah akasema baada ya hapo Allaah Akateremsha:

 

قَدْ فَرَضَ اللَّـهُ لَكُمْ تَحِلَّةَ أَيْمَانِكُمْ ۚ وَاللَّـهُ مَوْلَاكُمْ ۖ وَهُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ﴿٢﴾

2. Allaah Amekwishakufaridhishieni ukomboaji kwa viapo vyenu. 

 

[Imepokewa na Al-Haytham bin Kuleyb katika musnad yake kama ilivyo katika tafsiri ya Ibn Kathiyr (Juz 4 uk 386)]

 

Al-Haafidhw amesema katika Al-Fat-h (Juz 10 Uk 283) inawezekana ikawa Aayah hiyo imeteremka kwa ajili ya sababu mbili kwa wakati mmoja. Sababu zenyewe ni kuharamisha asali na sababu ya pili ni kujiharamishia kijakazi wake (Maariyah Al-Qubtwiyyah).

 

Ash-Shawkaaniy amesema katika tafsiri yake (Juz 5 Uk 252) na hizi ni sababu mbili za kushuka kwa Aayah, na kukusanya kunawezekana kwa kutokea kwa visa viwili kisa cha asali na kisa cha Maariyah Al-Qubtwiyyah na ya kuwa Qur-aan imeteremka kwa ajili ya visa vyote viwili na kwa kila kimoja ni kule alipo mwambia mmoja wa wake zake jambo la siri.
 

 



from Alhidaaya.com https://ift.tt/2TM8ta8
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...