Swali
Je, inajuzu kwa mwanamke kufanya kazi katika idara za serikali kwa hoja hana ambaye atampa matumizi?
Jibu
Katika hali kama hii, haijuzu. Kwa kuwa atachanganyika na mudiri, raisi na atachukua ujira kutoka kwake.
Hili halijuzu. Mwanamke anazingatiwa kuwa ni fitina.
Na Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema: “Mwanamke ni ´Awrah (uchi), Pindi anapotoka nje, matumaini ya Shaytwaan huongezeka.”
وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ
“Na mnapowauliza (wake zake) haja, waulizeni nyuma ya pazia.” (33:53)
Hata kama Aayah hii inawahusu wake za Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Hata hivyo, inawagusa wanawake wote, kama alivyosema Shaykh ash-Shinqiytwiy (Rahimahu Allaah). Mimi ninawanasihi kina dada, bali nasema kuwa haijuzu kufanya kazi katika idara kama hizi ambazo zina mchanganyiko na fitina. Hali kadhalika Hospitali za mchanganyiko, tunawanasihi kujiweka mbali na haya.
Na Allaah anajua zaidi
https://ift.tt/2FEnndw i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni