Swali
Mwanamke huyu anasema kuwa mpaka sasa hajalipa deni lake la Ramadhaan kwa miaka mingi. Ni lipi linalomlazimu hivi sasa?
Jibu
Ni lazima kwake kulipa kile kilichompita. Akisema kuwa hajui ni idadi ngapi zilizompita, tunamwambia afanye lililo salama na akadirie halafu baada ya hapo alipe kile kilichompita.
Hana juu yake kulisha chakula au kutoa swadaqah kwa mujibu wa maoni yenye nguvu. Kinachomlazimu ni yeye kulipa zile siku ambazo zilizompita.
Rejea Kitab al-Liqaa' ash-Shahriy (25)
https://ift.tt/2uwGKzO i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni