Swali: Mtu ambaye anakuja kuswali msikitini akiwa na nguo za kulalia (pyamas) anatakiwa kukemewa na khaswakhaswa ikiwa ni msikiti Mtakatifu? Watu wengi wanafanya hivo.
Jibu: Swalah ni sahihi. Lakini bora ni yeye kuja na nguo nzuri. Kunaweza kusemwa kwamba ni kwenda kinyume na muruwa ikiwa kitendo hicho kinaenda kinyume na desturi za watu. Haitakiwi kwa mtu kuja na nguo zinazokwenda kinyume na desturi za watu. Kwa sababu ni kwenda kinyume na muruwa. Ama kuhusu swalah yenyewe ni sahihi endapo nguo hiyo itakuwa ni safi na ni yenye kusitiri vile viungo visivyotakiwa kuonekana.
from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2T94cBR
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni