Swali: Ni ipi hukumu ya kutangamana na mtu anayechezea dini shere?
Jibu: Anayeifanyia istihzai dini anaritadi kutoka nje katika Uislamu. Haijalishi kitu japokuwa atadai kuwa anafanya hivo kwa sababu ya mzaha tu. Haijuzu kufanya utani kwa mambo kama haya. Amesema (Ta´ala):
وَلَئِن سَأَلْتَهُمْ لَيَقُولُنَّ إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلْعَبُ ۚ قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ
“Ukiwauliza watasema: “Hakika tulikuwa tunaporoja na tunacheza.” Sema: “Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayah Zake na Mtume Wake?” Hivyo basi msitoe udhuru. Kwani mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.” (09:65.66)
Mwenye kufanya mzaha na dini hapana shaka kwamba ameritadi kutoka katika Uislamu. Hata kama atakuwa mwenye kufanya mzaha. Hapa sio sehemu ya kucheza shere.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2W2OnKN
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni