Translate

Alhamisi, 24 Januari 2019

093-Asbaabun-Nuzuwl: Adhw-Dhwuhaa:

 

 

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

093-Adhw-Dhwuhaa:

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

وَالضُّحَىٰ ﴿١﴾

1. Naapa kwa dhuha.

 

وَاللَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ ﴿٢﴾

2. Na Naapa kwa usiku unapotanda kiza na kutulia.

 

مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ ﴿٣﴾

3. Rabb wako Hakukutelekeza na wala Hakukuchukia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).

 

 

حَدَّثَنَا إِسْحَاقُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، أَخْبَرَنَا سُفْيَانُ، عَنِ الأَسْوَدِ بْنِ قَيْسٍ، أَنَّهُ سَمِعَ جُنْدُبًا، يَقُولُ أَبْطَأَ جِبْرِيلُ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ الْمُشْرِكُونَ: قَدْ وُدِّعَ مُحَمَّدٌ فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: ((وَالضُّحَى * وَاللَّيْلِ إِذَا سَجَى * مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَى‏))‏

 

Ametuhadithia Is-haaq bin Ibraahiym, ametujulisha Sufyaan kutoka kwa Al-Aswad bin Qays kuwa amemsikia Jundub akisema: Jibriyl alichelewa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), washirikina wakasema kuwa Jibriyl amemtelekeza Muhammad hivyo Allaah Akateremsha:

 

وَالضُّحَىٰ ﴿١﴾

1. Naapa kwa dhuha.

 

وَاللَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ ﴿٢﴾

2. Na Naapa kwa usiku unapotanda kiza na kutulia.

 

مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ ﴿٣﴾

3. Rabb wako Hakukutelekeza na wala Hakukuchukia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).

 

[Muslim: Kitaab Al-Jihaad Was-Siyar - Mlango wa maudhi aliyoyapata Nabiy kutoka kwa Washirikina na wanafiki]‏‏.

 

Pia,

 

حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ يُونُسَ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، حَدَّثَنَا الأَسْوَدُ بْنُ قَيْسٍ، قَالَ سَمِعْتُ جُنْدُبَ بْنَ سُفْيَانَ رضى الله عنه قَالَ: اشْتَكَى رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَلَمْ يَقُمْ لَيْلَتَيْنِ أَوْ ثَلاَثًا، فَجَاءَتِ امْرَأَةٌ فَقَالَتْ:  يَا مُحَمَّدُ! إِنِّي لأَرْجُو أَنْ يَكُونَ شَيْطَانُكَ قَدْ تَرَكَكَ، لَمْ أَرَهُ قَرِبَكَ مُنْذُ لَيْلَتَيْنِ أَوْ ثَلاَثًا‏.‏ فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: ((وَالضُّحَى * وَاللَّيْلِ إِذَا سَجَى * مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَى‏))

Ahmad bin Yuwnus ametuhadithia na Zuhayr pamoja na Al-Aswad ametuhadithia kuwa, Nimemsikia Jundub bin Sufyaan (رضي الله عنه) kwamba:  Wakati fulani Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alionesha masikitiko yake (ya kutoteremka kwake Jibriyl) au kuumwa na hakusimama kwa muda wa siku mbili au tatu, akatokea mwanamke akasema: Yaa Muhammad! Mimi nadhani shaytwaan wako amekuacha, sijamuona akikukurubia kwa muda wa siku mbili au tatu. Allaah (عزّ وجلّ) Akateremsha:

 

وَالضُّحَىٰ ﴿١﴾

1. Naapa kwa dhuha.

 

وَاللَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ ﴿٢﴾

2. Na Naapa kwa usiku unapotanda kiza na kutulia.

 

مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ ﴿٣﴾

3. Rabb wako Hakukutelekeza na wala Hakukuchukia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).

 

[Al-Bukhaariy: Kitaab At-Tafsiyr]

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

وَلَسَوْفَ يُعْطِيكَ رَبُّكَ فَتَرْضَىٰ ﴿٥﴾

5. Na bila shaka Rabb wako Atakupa na utaridhika.

 

 

Ibn Kathiyr katika Tafsiyr  yake (4/522) amesema:

 

Abuu ‘Umar Al-Awzaa’iyy kutoka kwa Ismaa’iyl bin ‘Ubaydillaah bin Abiy Al-Muhaajir Al-Makhzuwmiyy kutoka kwa ‘Aliy bin ‘Abbaas kutoka kwa baba yake amesema kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimdhihirishia kilichofunguliwa katika Ummah wake hazina baada ya hazina, akafurahishwa kwa hilo na Allaah Akateremsha:

 

5. Na bila shaka Rabb wako Atakupa na utaridhika.

Allaah Akampa Jannah kuna kasri elfu na elfu na katika kila kasri kuna unachotaka katika wake na wahudumu. [Imepokewa na Ibn Jurayj na Ibn Abiy Haatim kutoka katika njia yake na hii ni Isnaad Swahiyh hadi kwa Ibn ‘Abbaas].

 

Hadiyth imepokelewa na Ibn Jurayj kama alivyosema Al-Haafidhw Ibn Kathiyr (30/232) kutoka katika njia mbili kutoka kwa Al-Awzaa’iy katika mojawapo njia hizo yupo ‘Amru bin Hishaam Al-Bayruwniy mpokezi kutoka kwa Al-Awza’iy nayo ni dhaifu.

 

Na imepokewa na Al-Haakim na kusema kuwa ni Swahiyh (2/526)  imefuatiwa na maneno ya Adh-Dhahabiy: amepwekeka nayo ‘Iswaam bin Rawaad kutoka kwa baba yake na imepokewa na kudhoofishwa na Atw-Twabaraaniy katika kitabu chake Al-Kabiyr na Al-Awsatw. Al-Haythamiy amesema: na riwaayah kwenye Al-AwsatwRasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nilionyeshwa yale ambayo Ummah wangu utafunguliwa baada ya kuondoka kwangu nikafurahishwa Allaah Akateremsha:
 

وَلَلْآخِرَةُ خَيْرٌ لَّكَ مِنَ الْأُولَىٰ ﴿٤﴾

4. Na bila shaka Aakhirah ni khayr kwako kuliko ya awali (dunia).

 

Akataja mfano wake na ndani yake Muaawiyah bin Abiy Al-‘Abbaas na sikumjua, na baki ya watu wake ni waaminifu, na Isnaad kwenye Al-Kabiyr ni Hassan, na imepokewa na Abuu Nu’aym katika Al-Hilyah (3/212) kutoka kwa Atw-Tabaraaniy na ndani yake yupo ‘Amru bin Hishaam Al-Bayruwniy kasha akasema kuwa Hadiyth ni Ghbariy (ngeni) miongoni mwa Hadiyth za ‘Aliy bin ‘Abdillaah bin ‘Abbaas na haikupokewa kutoka kwake isipokuwa Ismaa’iyl na Sufyaan Ath-Thawriy kutoka kwa Al-Awzaa’iy kutoka kwa Ismaa’iyl mfano wake.

 

Amepokea Imaam Ahmad kutoka kwa Jundub amesema, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliumwa wakati fulani na hakupata kusimama ila baada ya siku moja au mbili hivi akaja mwanamke mmoja akasema, ‘Ee Muhammad simuoni shaytwaan wako isipokuwa amekuacha, Allaah Akateremsha:

 

وَالضُّحَىٰ ﴿١﴾

1. Naapa kwa dhuha.

 

وَاللَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ ﴿٢﴾

2. Na Naapa kwa usiku unapotanda kiza na kutulia.

 

 

مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ ﴿٣﴾

3. Rabb wako Hakukutelekeza na wala Hakukuchukia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).

 

[Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy, an-Nasaaiy, Ibn Abiy Haatim, Ibn Jariyr (Fat-h Al-Baariy (7:23) kutoka kwa Jundub huyo ni Ibn 'Abdillaah Al-Bajaliyy kisha Al-‘Alaqiyy.

 

Anasema Al-‘Awfiyy kutoka kwa Ibn ‘Abbaas, kuwa kuna wakati Qur-aan ilichelewa kumteremkia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa masiku kadhaa. Mushrikina wakasema: Bwana wake Amemuacha na Amemchukia.  Allaah Akateremsha:  

 

وَالضُّحَىٰ ﴿١﴾

1. Naapa kwa dhuha.

 

وَاللَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ ﴿٢﴾

2. Na Naapa kwa usiku unapotanda kiza na kutulia.

 

 

مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ ﴿٣﴾

3. Rabb wako Hakukutelekeza na wala Hakukuchukia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم

 

وَالضُّحَىٰ ﴿١﴾

1. Naapa kwa dhuha.

 

وَاللَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ ﴿٢﴾

2. Na Naapa kwa usiku unapotanda kiza na kutulia.

 

مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ ﴿٣﴾

3. Rabb wako Hakukutelekeza na wala Hakukuchukia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).

 

وَلَلْآخِرَةُ خَيْرٌ لَّكَ مِنَ الْأُولَىٰ ﴿٤﴾

4. Na bila shaka Aakhirah ni kheri kwako kuliko ya awali (dunia).

 

وَلَسَوْفَ يُعْطِيكَ رَبُّكَ فَتَرْضَىٰ ﴿٥﴾

5. Na bila shaka Rabb wako Atakupa na utaridhika.

 

أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًا فَآوَىٰ ﴿٦﴾

6. Je, kwani Hakukukuta yatima, Akakupa makazi?

 

وَوَجَدَكَ ضَالًّا فَهَدَىٰ ﴿٧﴾

7. Na Akakukuta mpotevu Akakuongoza?

 

وَوَجَدَكَ عَائِلًا فَأَغْنَىٰ ﴿٨﴾

8. Na Akakukuta mhitaji, Akakutosheleza?

 

فَأَمَّا الْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ ﴿٩﴾

9. Kwa hivyo basi yatima usimuonee.

 

وَأَمَّا السَّائِلَ فَلَا تَنْهَرْ ﴿١٠﴾

10. Na muulizaji usimkaripie.

وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ ﴿١١﴾

11. Na neema ya Rabb wako ihadithie.

 



from Alhidaaya.com http://bit.ly/2UfYWbQ
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...