Vivyo hivyo mtu kutaka kusikika. Ni kama kujionyesha. Kutaka kusikika ni kule mtu kupenda asikike na watu. Kwa mfano wasikie du´aa zake, kauli zake ambazo uinje wake ni nzuri na anaonekana anamdhukuru Allaah ilihali anachokusudia watu wamsifu na watu waseme kwa kweli fulani anamdhukuru Allaah sana, fulani anatafuta elimu, anafundisha elimu, fulani anafanya hivi na vile. Anaboresha sauti yake katika kisomo cha Qur-aan kwa ajili ya kutaka kusifiwa na watu. Yote haya ni katika aina za mtu kutaka kusikika. Mwenye kutaka kuonekana, basi Allaah atamfanya kweli aonekane. Kwa sababu malipo yanategemea na vile mtu alivyotenda. Mwenye kutaka kusikika, basi Allaah atamfanya kweli asikike.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2CMSvG8
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni