Miongoni mwa mambo yanayoitia kasoro ´Aqiydah ni shirki ndogo. Nayo inakuwa kwa matamshi ya dhahiri. Kwa mfano kuapa kwa jina la asiyekuwa Allaah (´Azza wa Jall). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Atakayeapa kwa asiyekuwa Allaah amekufuru au amefanya shirki.”
“Msiape kwa baba zenu! Yule mwenye kutaka kuapa basi aape kwa jina la Allaah au anyamaze.”
Kuapa kwa asiyekuwa Allaah ni shirki. Lakini hata hivyo ni shirki ndogo isipokuwa tu ikiwa mtu huyo atakusudia kumuadhimisha yule anayemuapia kama anavyoadhimishwa Allaah (´Azza wa Jall) hapo itakuwa shirki kubwa. Hili hufanywa na watu wengi kuapa kwa asiyekuwa Allaah. Kwa mfano utawasikia wanasena ´naapa kwa Mtume` (wan-Nabiy), wanaapa kwa jina la Ka´bah na wanaapa kwa amana. Hii ni shirki. Inaweza kuwa shirki ndogo au kubwa itatokana na nia ya muapaji. Kuna watu wengi wasiojua uhakika wa Tawhiyd na wala hawasomi makatazo ya kuapa kwa ajili ya asiyekuwa Allaah.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2Sak0mB
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni