Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
096-Suwrah Al-‘Alaq Aayah 6-19
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ ﴿٦﴾
Laa hasha! Hakika mwana Aadam bila shaka amepindukia mipaka kuasi.
أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ ﴿٧﴾
Kwa kuwa amejiona amejitosheleza.
إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الرُّجْعَىٰ ﴿٨﴾
Hakika kwa Rabb wako ni marejeo.
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَىٰ ﴿٩﴾
Je, umemuona yule anayekataza?
عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰ ﴿١٠﴾
Mja pale anaposwali?
Sababun-Nuzuwl:
Imaam Ibn Kathiyr amesema kuhusu kauli hizo za Allaah (سبحانه وتعالى) kwamba hizo kakusudiwa Ubay wa Abuu Jahal na makamio kwa kumpatiliza.
Aayah hizi zilimshukia Abuu Jahal (Allaah Amlaani) ambaye alimkamia na kumtisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa akiswali mbele ya Al-Ka’bah. Allaah (سبحانه وتعالى) Akamuonya Abu Jahl kwa maneno ambayo yalikuwa ni mazuri kwa kusema:
أَرَأَيْتَ إِن كَانَ عَلَى الْهُدَىٰ ﴿١١﴾
Je, umeona kama alikuwa katika Uongofu?
Maana: Ni nini dhana yako juu ya mtu huyu ambaye unamkataza asifanye jambo la kheri kwa kufuata njia iliyonyooka katika matendo yake na (au akiamrisha kumcha Allaah) kwa maneno yake. Na wewe unamkamia kwa hilo alifanyalo. Kauli yake Allaah (سبحانه وتعالى) baada ya hayo ni:
أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَىٰ ﴿١٢﴾
Au ameamrisha kuhusu taqwa?
Maana: Hali ya kuwa unaendelea kumghasi na kumuonya katika Swalaah yake. Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ اللَّـهَ يَرَىٰ ﴿١٤﴾
Je, hajui kwamba hakika Allaah Anaona?
Maana: Je, Hivi huyu mtu mkatazaji wa Wahyi wa mtu anayefuata mwongozo (naye ni Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم je, (Abuu Jahl) hajui kwamba Allaah Anamuona na Anasikia maneno yake na atamtia hesabuni kumlipa juu ya matendo yake malipo yaliyokamilika? Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Amesema kwa hali ya kumkamia na kumtisha:
كَلَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ ﴿١٥﴾
Laa hasha! Asipoacha, bila shaka Tutamburuta kwa nywele za paji la uso.
Maana: Tutaupakaza utosi wake rangi nyeusi Siku ya Qiyaamah, kisha Akasema:
نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ ﴿١٦﴾
Paji la usio linalokadhibisha lenye hatia.
Anaukusudia utosi wa Abuu Jahal ni muongo maneno yake yana makosa katika matendo yake,
فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ ﴿١٧﴾
Basi na aite timu yake.
Maana: Watu wake na jamaa zake na awaite atake kwao nusura.
سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ ﴿١٨﴾
Nasi Tutawaita Az-Zabaaniyah (Malaika wa adhabu).
Maana: Na Sisi tutawaita Mazaabaniyah na hao ni Malaika wa adhabu ili ajue ni nani atakayeshinda ni kundi lake au kundi letu?
كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَاسْجُدْ وَاقْتَرِب ۩﴿١٩﴾
Laa hasha! Usimtii; na sujudu na kurubia (kwa Allaah).
[Tafsiyr Ibn Kathiyr]
from Alhidaaya.com http://bit.ly/2DPA3yj
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni