Translate

Jumatatu, 28 Januari 2019

He, Uislamu umegawanyika makundi?

*Swali*

Jee
Uislam umegawanyikaaa?
Una makundii?

*Majibu*

✅Naam ni kweli kwamba Uislamu umegawanyika katika Makundi tofauti tofauti.

➡Kwa kifupi tu kwa kukupa mwangaza kidogo, utayajua yale makundi yaliyo potofu kwa kuona na kujua itikadi zao.

➡Mfano mzuri leo utaona wanaodai kuna mtume baada ya Mtume wa haki na wa mwisho Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), utawaona pia wale wanaowakufurisha Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) na kuwatukana wake za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), pia utawaona wengine wanaokufurisha Waislam na kuwatoa katika Dini kwa sababu wanaamini kuonekana Allaah Qiyaamah, na wanakufurisha Waislamu kwa sababu ya kufanya baadhi ya maasi, na pia utawaona wengine wanakataa Hadiyth za Mtume na kudai kuwa wao wanafuata Qur-aan pekee, na pia utawakuta wengine wanakwenda kuwaomba watu waliokufa makaburini ili wawasaidie haja zao, na wengi wengine wasio na idadi.

➡Tutalijua kundi lililookoka na ambalo halipo katika hayo makundi 72, kwa kuitazama ile Hadiyth ya bwana Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo⤵

((Wamegawanyika Mayahudi katika mapote 71, wakagawanyika Wakristo katika mapote 72 na Ummah wangu utagawanyika mapote 73. Yote hayo yataingia motoni ila moja tu)) Maswahaba waliuliza: Ni lipi hilo, ewe Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wa Allaah! Akasema: ((Ni lile nililokuwemo mimi na Swahaba zangu))
↪Imepokelewa na Imaam Ahmad, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ad-Daarimiy.

✅Kundi hilo litakuwa ni lenye kufuata maagizo ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Makhalifa waongofu (Radhiya Allaahu ‘anhum) na Maswahaba wengine (Radhiya Allaahu ‘anhum) na wema wote waliotangulia (Salafus-Swaalih). Muislam atakayejikita na kuwa imara katika hayo basi atakuwa katika njia nyoofu. Dalili ni nyingi katika Qur-aan na Sunnah.

➡Miongoni mwayo ni kauli ya Allaah (Subhaana wa Taala)⤵

((Na anayemtii Allaah na Mtume Wake, bila ya shaka amefanikiwa mafanikio makubwa))
↪Rejea Qur'an 33: 71. 

➡Pia Amesema Allaah (Subhaana wa Taala)⤵

((Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Allaah basi nifuateni mimi, Allaah Atakupendeni na Atakufutieni madhambi yenu. Na Allaah ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu))
↪Rejea Qur'an 3: 31.

➡Mtume Muhammad(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) naye anatueleza yafutayo katika khutbah yake ya Hijjatul Wadaa: ((Hakika nimewaachia kitu ambacho hamtapotea baada yangu lau mtashikana nacho, Kitabu cha Allaah))
↪Imepokelewa na Imaam Muslim

Sehemu nyengine kasema: ((Kitabu cha Allaah na Sunnah zangu))
↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy na Muslim.

➡Na katika masimulizi ya Abu Najiih al- 'Irbaadh bin Saariyah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba⤵

"Alituwaidhia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yaliyozifanya nyoyo kuingia hofu na macho yakatokwa na machozi. Tukamwambia: "Ewe Mtume wa Allaah! Yaonyesha kama haya ni mawaidha ya kuaga, basi tuusie". Akasema: ((Nawausia kumcha Allaah, Kwani hakika atakayeishi katika nyinyi ataona khitilafu nyingi, basi jilazimisheni kufuata Sunnah zangu na Sunnah za Makhalifa walioongoka, yashikeni kwa magego mambo yao))
↪Imepokelewa na Imaam Abu Daawuwd, Ahmad, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah na Ad-Daarimiy

✅Mambo muhimu ambayo tunayapata katika dondoo za hapo juu ni kuwa, kuwepo kwetu katika kundi litakaloongoka ni kufuata mwendo aliokuwa nao Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Makhalifa wake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na kushikamana nao kivitendo barabara.

Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Atufanye ni wenye kuyashikilia hayo vilivyo ili tuwe ni wenye kuingia katika Rehma Yake na kuwa ni kundi lililosalimika na moto, kundi lililonusurika na ni kundi liliokoka. Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Atusahilishie hatua zetu katika kuelekea katika mwendo wa sawa na wa haki.

Na Allaah Anajua zaidi 

Imeandaliwa na *Imaam Masjid Tawbah*



from fisabilillaah.com http://bit.ly/2RlWwqj
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...