Translate

Alhamisi, 24 Januari 2019

Mwanachuoni wa ki-Ibaadhiy akimkufurisha ´Abdullaah bin Sallaam

Swuhayb  amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watapoingia watu wa Peponi Peponi basi Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) atasema: “Je, kuna kitu mnataka nikuzidishieni?” Watasema: “Je, hukuzifanya weupe nyuso zetu? Hukutuingiza Peponi na Ukatuokoa kutokamana na Moto? Kisha Atafunua pazia Yake. Hawajapatapo kupewa kitu kama kumtazama Mola wao (´Azza  wa Jall).”[1]

Hadiyth hii na mfano wake si hoja kabisa kutokana na sababu nyingi kukiwemo:

Sababu ya kwanza: Mapokezi yote haya cheni za wapokezi wake ni dhaifu. Ndugu ´Aliy al-Hijiriy amebainisha udhaifu wake katika uchunguzi ambao umepambanuka. Amekusanya mapokezi yote yanayotumiwa kama dalili na Ahl-ul-Hadiyth. Kadhalika Hasan as-Saqqaaf amebainisha udhaifu wake katika kitabu maalum ambapo amesema ndani yake:

“Ibn-ul-Qayyim amedai kuwa Hadiyth zinazozungumzia kuwa Allaah ataonekana [siku ya Qiyaamah] zimekuja kwa njia nyingi kabisa (Mutawaatir). Mambo sivyo kabisa. Bali ni Hadiyth zilizopokelewa kwa njia moja moja (Ahaad) na zilizotiwa kasoro. Sisi tunaona kuwa zimepokelewa na wana wa israaiyl haijalishi kitu hata kama zitakuwa katika vitabu “Swahiyh”. Zimechomekwa ndani ya Ummah huu na watu kama Ka´b al-Ahbaar, ´Abdullaah bin Sallaam na watu mfano wao.”[2]

[1] Muslim (449).

[2] Mas-alah Ru´yah, uk. 05



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2Tbz4xF
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...