Translate

Jumatatu, 28 Januari 2019

Hukmu ya mke kutoroka kwa Mumewe sababu ya mume kuongeza mke wa pili

Naam

➡Hakika ni kuwa ni vigumu kutoa hukumu ya moja kwa moja kwani tumesikia kesi au kujitetea kwa upande mmoja. Hatujasikia yaliyomfanya mke atoroke. Hata hivyo, katika hali yoyote ile mke kisheria hafai kutoka kwa mumewe kwa sababu yoyote ila iwe kwa ajili ya kisheria ambayo amemnasihi mumewe mpaka akachoka.

➡Suala la mke kutoka mara moja ni ikiwa mume ameritadi kutoka katika Uislamu au maasiya makubwa dhahiri shahiri.

➡Mara nyingi wake kwa wivu ulio nje ya sheria hupandwa na hasira wakafanya mambo kama hayo kisha wakajuta baadaye. Wakati huo huenda majuto kama hayo yakawa hayana faida yoyote ile.

➡Kwa kuwa suala hilo lishatendeka wewe usiwe na hasira bali fuata njia za kisheria kumpata na kumrudisha mkeo. Njia ya rahisi ni kwako kwenda kwa wazazi wake na kutoa taarifa hiyo.

➡Mbali na kuwa wazazi wake huenda wakawa pamoja na binti yao. Hiyo ni kwa kuwa mke wa mtu akaja kwa wazazi na wazazi nao wakamuacha bila kumshurutisha kurudi.

➡Hata hivyo, tukichukulia dhana nzuri ni kuwa huenda wazazi walimwambia arudi kwako naye akatoka lakini asifike kwako. Kwa hiyo, nenda kwa wazazi wake na uzungumze nao kwa upole, ulaini na kwa heshima kuhusu hilo.

➡Kwa mke kumtoroka mumewe kwa sababu yoyote ile au bila ya sababu ni makosa ambayo mwanamke wa Kiislamu hafai kufanya kabisa. Ikiwa mume amemkosea mke zipo njia ambazo zinaweza kufuatwa ili kutatua tatizo ambalo limetokea. Inatakiwa tuelewe kuwa kosa halitatuliwa na kosa.

➡Uislamu umeweka nidhamu ya kila jambo na kutoa suluhisho kwa matatizo yetu yote hata katika mas-ala ya ndoa, talaka na mengineyo. Kutoroka kutoka nyumba ya mume huwa bado hujatatua tatizo ambalo lipo. Ikiwa mume amemkosea mke inatakiwa mke amueke chini na kumueleza anavyofikiri kwa lile jambo.

➡Ikiwa hakuweza kutatua, anaweza kuwatumia wazazi wake na wale wa mumewe au masheikh wazoefu katika mas-ala ya suluhu za kindoa. Mke kafanya vizuri kujirudi kwa makosa yakutoroka kwani makosa hayasamehewi na Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) mpaka mtu aombe msamaha kwa aliyemkosea akiwa ni mwanadamu mbali na kujuta, kuwa na azma ya kutorudia kosa na pia kutolifanya kosa hilo. Sasa mke hajaomba msamaha kwani huu unakuwa ni kama mfano wa gazeti la Denmark, Jyllands-Posten, pale meneja aliposema tunaomba msamaha kuwaudhi Waislamu lakini sio kuchapisha vikaragosi vya Mtume Muhammad(Swalla Allahu  'alayhi wa aalihi wa sallam). Na hapa tunaona hivyo hivyo kuwa mke amejirudi kwa kumuomba mumewe msamaha lakini hataki kubaki naye na mas-ala makubwa ya mtu anapofanya kosa na kusamehewa ni ajiondoe katika lile kosa na kurudi kama awali.

➡Ili kosa hilo kuondoka ni mke arudi baada ya kusamehewa katika nyumba yake ili waweze kuishi pamoja na mumewe na wawalee watoto wao ikiwa wanao. Na lau amekimbia kwa sababu ya tatizo baina yake na mumewe wanaweza kukaa chini na wakaangalia ni njia gani wanaweza kutumia ili kusuluhisha tatizo hilo.

➡Allaah (Subhaana wa Taala) Anasema kwamba⤵

“Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Allaah Atawawezesha. Hakika Allaah ni Mjuzi Mwenye khabari”
↪Rejea Qur'an 4: 35.

✅Mwanamke kama huyu hatima yake ni mbaya hapa ulimwenguni na Kesho Akhera, kwani Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Ikiwa mwanamke yeyote atamuomba mumewe talaka bila ya kuwa na sababu nzito (yenye nguvu), harufu ya Pepo itakuwa ni haramu kwake”
↪Imepokelewa na Imaam Abu Dawuud kutoka kwa Thawbaan [Radhiya Allahu 'anhu] )

✅Hii itakuwa ni hasara ambayo mke atapata Kesho Akhera.

✅Tufahamu kuwa hapa duniani pia atapigwa muhuri wa unafiki. Mtume (Swalla Allahu  'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Wanawake ambao watajiachisha kutoka kwa waume zao na wanawake wenye kuwashawishi waume zao wawapatie talaka kwa malipo ni wanafiki”
↪Imepokelewa na Imaam At-Tirmidhiy na an-Nasa’iy kutoka kwa Abu Hurayrah [Radhiya Allahu 'Anhu] 

➡Na hakika ni kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amewazungumzia wanawake ambao wana sifa ya kubaki na waume zao hata kama waume wanataka kuwaacha kwa kuwa na maagano na ahadi kati yao.

➡Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema kwamba⤵

“Na mwanamke akichelea kutupwa au kutojaliwa na mumewe, basi si vibaya kwao wakisikizana kwa suluhu. Na suluhu ni bora. Na nafsi zimewekewa machoni mwake tamaa na choyo. Na mkifanya wema na mkamchamngu basi hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayoyatenda”
↪Rejea Qur'an 4: 128.

➡Aishah (Radhiya Allahu 'anha) amesema yafuatayo kuhusu aya hii kuwa⤵

“Ikiwa mwanamke akichelea kutupwa au kutojaliwa na mumewe” (yaani mume ameona kitu asichopenda kwa mkewe, kama uzee au mfano wake, na akataka kumpatia talaka, lakini mke akamtaka mume akae na ampatie anachopenda mwenyewe. Ndio Allah Akasema: ‘basi si vibaya kwao wakisikizana kwa suluhu’”
↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy. 

➡Ikiwa hakutakuwa na natija yoyote na mke akakataa kukaa kwako kwa ajili ya kuoa mke wa pili basi ni afadhali umuache na ubakie na huyo wa pili kwani ukitofanya hivyo utasumbuka pasi na kuwa na haja hiyo.

Na Allaah Anajua zaidi

Imeandaliwa na *Imaam Masjid Tawbah*



from fisabilillaah.com http://bit.ly/2Wrs1mo
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...