Swali: Mwanamke aliyekufa wakati wa damu ya uzazi anazikwa na nguo zake, anaoshwa na kuzikwa? Ni ipi kafara ya aliyemfanyia hivo mke wake?
Jibu: Mwanamke ambaye amekufa ndani ya nifasi yake ni kama wanawake wengine. Kwa maana kwamba ni wajibu kuoshwa na kuvikwa sanda ya kawaida kama wengine. Nguo zake zitabaki zikiwa ni mirathi kwa familia yake. Yule ambaye alimzika mke wake akiwa na nguo zake, tunataraji kwa Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala) atamsamehe juu ya kitendo chake hichi. Ilikuwa ni wajibu kwake kuuliza kabla ya kutenda.
Tunasikitika kuona watu wengi hii leo wanafanya mambo ya makosa pasi na kuwauliza wanachuoni isipokuwa baada ya kuyatenda. Baada ya kutokea kosa ndio wanakuja kuuliza. Kitendo hichi sio kizuri. Tunasema: mtu aulize kabla ya kutenda ili mtu asitumbukie katika jambo la kimakosa. Kuna faida gani mtu kishafanya kitendo cha kimakoa ndio anakuja kuuliza? Kitendo hichi kinaweza kuwa kinapelekea mambo mengi kwa njia asiyoihisi.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2TfnL7z
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni