Translate

Jumatatu, 28 Januari 2019

Mume afanye nini ikiwa mkewe hataki kuswali?

*Swali*

Mume achukue hatua gani ikiwa mke hataki kuswali?

*Jibu*

✅Mara nyingi kama vile wanawake wanashindwa kufuata maagizo ya kuchagua mume wa sawa Kidini ndivyo wanaume wanavyofanya makosa hayo hayo.

➡Mume wa Kiislamu anatakiwa amchague mke mwenye Dini na Imani, maadili na tabia nzuri.

✅Kukosa kufuata maagizo hayo ya Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ndio kunatokea matatizo kama hayo.

➡Hata hivyo, kosa lishatokea na inabidi tupate suluhisho kwa suala hilo nyeti.

➡Kulingana na maelezo yako ni kuwa mkeo inaonyesha bado ana Uislamu na Imani, hivyo anataka msukumo wa kuweza kutekeleza wajibu huo bila ya tatizo.

➡Jambo ambalo unatakiwa mwanzo kabisa kufanya ni kumnasihi mkeo kwa njia nzuri, kwani Allaah (Subhaana wa Taala) Anatuambia⤵

“Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora”
↪Rejea Qur'an 16: 125.

➡Inatakiwa utumie mbinu tofauti za kuweza kumvutia katika kuswali bila ya yeye kuwa na kinyongo juu ya suala hilo.

➡Mpatie vipeperushi kuhusu umuhimu wa Swalah na madhara ya kuacha, vitabu, kanda, kaseti na njia nyingine.

✅Ikiwa imeshindikana hilo, itabidi sasa uingize mkono wa wazazi wenu kama inavyotaka sheria.

➡Allaah (Subhaana wa Taala) Anasema kwamba⤵

“Na ambao mnachelea kutoka katika utiifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikutiini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Allaah ndiye Aliye juu na Mkuu. Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Allaah Atawawezesha. Hakika Allaah ni Mjuzi Mwenye khabari”
↪Rejea Qur'an 34 – 35.

➡Hivyo Mume inatakiwa ufuate mfumo ufuatao⤵

1⃣Kuwanasihi katika ya haki na ukweli.

2⃣Mhame(Jitenge naye katika Kitanda) katika malazi.

3⃣Mpige mkeo kipigo ambacho hakitamuumiza bali cha kumtisha wala usimpige uso.

4⃣Kuwe na suluhisho kwa kutumia waamuzi kutoka upande wa mke na mume ili waamue hilo.

✅Ikiwa hakukupatikana suluhisho lolote na wala mkeo hakubadilika basi itabidi umuache.

➡Na ikiwa itatokea hilo itabidi usirudie kosa tena unapotaka kuoa mwingine. Hata hivyo, tunaamini kuwa haitofikia hapo, In Shaa Allaah

Na Allaah Anajua zaidi

Imeandaliwa na *Imaam Masjid Tawbah*



from fisabilillaah.com http://bit.ly/2CL0y68
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...