Je,inafaa kusheherekea Death Anniversary..? na ipi Hukmu ya Kusheherekea kumbukumbu ya Kifo (Anniversary)
Jibu
Kwanza ni dhambi katika Uislamu kuweka kumbukumbu ya kifo inayojulikana kama ni ‘death anniversary’. Hili ni jambo la kuiga makafiri ambalo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekemea. Kwa hiyo kulitenda ni miongoni mwa madhambi makubwa unapaswa ujiepushe nalo kabisa.
Uislamu ni Dini yenye kutuongoza katika mfumo mzima wa maisha hapa duniani. Kwa ajili hiyo, lolote tufanyalo ni lazima liambatane na Shariy’ah ya Uislamu.
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwakuta watu wa Madiynah wakisherehekea siku kuu zao. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaambia kuwa wao wamebadilishiwa hizo sikukuu zao kwa siku mbili kuu zilizo bora kabisa, nazo ‘Iyd al-Fitwr na Al-Adhw-haa.
Ama sherehe ya anniversary hata ya Nabiy mwenyewe (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) haipo katika siku za sherehe.
Ama hizi anniversaries ambazo tunasherehekea ni katika ada na desturi za makafiri na mushrikina. Na kwa hilo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza katika Hadiyth:
عن إبن عمر ((من تشبه بقوم فهو منهم)) ابن حبان - صحيح
Kutoka kwa Ibn 'Umar ((Mwenye kujifananisha na watu naye ni kama wao)) [Ibn Hibbaan ikiwa swahiyh]
Na zimezuka anniversaries nyenginezo mbali na ya ndoa ambayo ndio iliyoanzishwa mwanzo na makafiri. Kumezuka mpaka anniversary za kifo.
Shariy’ah ya Kiislamu kuhusu mtu anapoweka nadhiri kwa ajili ya jambo lisilofaa basi anatakiwa asitekeleze hiyo nadhiri bali ajiepushe na hilo jambo. Dalili ni Hadiyth ifuatayo ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
عَنْ أبي طريفٍ عَدِيَّ بْنَ حَاتِمٍ الطَّائي (رضي الله عنه) قال: سَمِعْتُ رسول اللَّهِ (صلى الله عليه و آله وسلم) يَقُولُ: ((مَنْ حَلَفَ عَلَى يَمِينٍ ثُمَّ رَأَى أَتْقَى لِلَّهِ مِنْهَا فَلْيَأْتِ التَّقْوَى)) رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abu Twariyf ‘Adiyy bin Haatim (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nimesikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
((Atakayeapa yamini [kufanya jambo] kisha akaona linalomridhisha zaidi Allaah kuliko aliloliapia, basi amche Allaah kwa kufanya linalomridhisha Allaah)) [Muslim]
Na Allaah anajua zaidi
from fisabilillaah.com http://bit.ly/2FOdzju
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni