Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
05-Akiwapendelea Waumini Yaliyo Mepesi Katika ‘Amali Zao Na Katika Da’wah
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwapendelea Maswahaba kutenda yaliyo mepesi na hakuwatakia wataabike katika ‘amali zao wala katika kutaamuli na watu katika Da’wah. Hadiyth ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amesema:
كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا أَمَرَهُمْ أَمَرَهُمْ مِنَ الأَعْمَالِ بِمَا يُطِيقُونَ قَالُوا: ((إِنَّا لَسْنَا كَهَيْئَتِكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ اللَّهَ قَدْ غَفَرَ لَكَ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ. فَيَغْضَبُ حَتَّى يُعْرَفَ الْغَضَبُ فِي وَجْهِهِ ثُمَّ يَقُولُ: ((إِنَّ أَتْقَاكُمْ وَأَعْلَمَكُمْ بِاللَّهِ أَنَا))
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapowaamrisha (Waumini) jambo katika 'amali aliwaamrisha (mepesi) ambayo walikuwa na uwezo nao wakawa wanasema: “Sisi si kama wewe, Allaah Amekughufuria madhambi yako yaliyotangulia na ya baadae.” Akaghadhibika mpaka ghadhabu ikadhihirika usoni mwake kisha akasema: ((Mimi ni mwenye taqwa zaidi yenu, na namjua zaidi Allaah kulikoni nyinyi)) [Al-Bukhaariy]
Na katika Da’wah (ulinganiaji):
عَنْ أَنَسِ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَسِّرُوا وَلاَ تُعَسِّرُوا وَبَشِّرُوا ولاَ تُنَفِّرُوا)) متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Sahilisheni wala msifanye uzito, wapendekezeni watu khayr na muwabashirie wala msiwakimbize)). [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na katika ‘Ibaadah: Hadiyth ya ‘Abdullaah Ibn ‘Amru Ibn Al-‘Aasw:
كُنْتُ أَصُومُ الدَّهْرَ وَأَقْرَأُ الْقُرْآنَ كُلَّ لَيْلَةٍ - قَالَ - فَإِمَّا ذُكِرْتُ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم وَإِمَّا أَرْسَلَ إِلَىَّ فَأَتَيْتُهُ فَقَالَ لِي"أَلَمْ أُخْبَرْ أَنَّكَ تَصُومُ الدَّهْرَ وَتَقْرَأُ الْقُرْآنَ كُلَّ لَيْلَةٍ". قُلْتُ بَلَى يَا نَبِيَّ اللَّهِ وَلَمْ أُرِدْ بِذَلِكَ إِلاَّ الْخَيْرَ. قَالَ "فَإِنَّ بِحَسْبِكَ أَنْ تَصُومَ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ ثَلاَثَةَ أَيَّامٍ ". قُلْتُ يَا نَبِيَّ اللَّهِ إِنِّي أُطِيقُ أَفْضَلَ مِنْ ذَلِكَ . قَالَ " فَإِنَّ لِزَوْجِكَ عَلَيْكَ حَقًّا وَلِزَوْرِكَ عَلَيْكَ حَقًّا وَلِجَسَدِكَ عَلَيْكَ حَقًّا - قَالَ - فَصُمْ صَوْمَ دَاوُدَ نَبِيِّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَإِنَّهُ كَانَ أَعْبَدَ النَّاسِ". قَالَ قُلْتُ يَا نَبِيَّ اللَّهِ وَمَا صَوْمُ دَاوُدَ قَالَ "كَانَ يَصُومُ يَوْمًا وَيُفْطِرُ يَوْمًا". قَالَ "وَاقْرَإِ الْقُرْآنَ فِي كُلِّ شَهْرٍ" . قَالَ قُلْتُ يَا نَبِيَّ اللَّهِ إِنِّي أُطِيقُ أَفْضَلَ مِنْ ذَلِكَ قَالَ " فَاقْرَأْهُ فِي كُلِّ عِشْرِينَ ". قَالَ قُلْتُ يَا نَبِيَّ اللَّهِ إِنِّي أُطِيقُ أَفْضَلَ مِنْ ذَلِكَ قَالَ "فَاقْرَأْهُ فِي كُلِّ عَشْرٍ" . قَالَ قُلْتُ يَا نَبِيَّ اللَّهِ إِنِّي أُطِيقُ أَفْضَلَ مِنْ ذَلِكَ . قَالَ " فَاقْرَأْهُ فِي كُلِّ سَبْعٍ وَلاَ تَزِدْ عَلَى ذَلِكَ . فَإِنَّ لِزَوْجِكَ عَلَيْكَ حَقًّا وَلِزَوْرِكَ عَلَيْكَ حَقًّا وَلِجَسَدِكَ عَلَيْكَ حَقًّا". قَالَ فَشَدَّدْتُ فَشُدِّدَ عَلَىَّ. قَالَ وَقَالَ لِيَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم "إِنَّكَ لاَ تَدْرِي لَعَلَّكَ يَطُولُ بِكَ عُمْرٌ". قَالَ فَصِرْتُ إِلَى الَّذِي قَالَ لِيَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَلَمَّا كَبِرْتُ وَدِدْتُ أَنِّي كُنْتُ قَبِلْتُ رُخْصَةَ نَبِيِّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم.
“Nilikuwa nikifunga mwaka mzima, na nikisoma Qur-aan kila usiku. Alipojulishwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaniita kwake nikaenda. Akasema: ((Nimesikia kwamba unafunga (Swawm) mwaka mzima na unasoma (unakhitimisha) Qur-aan kila usiku?)) Nikasema: Ndio ee Rasuli wa Allaah. Wala sitaki lolote ila khayr tu. Akasema: ((Inakutosheleza ukifunga katika kila mwezi siku tatu…)) Kisha akasema: ((Na usome Qur-aan (ukhitimishe) kila mwezi)). Akasema: Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah, mimi hakika naweza kufanya vizuri zaidi ya hivyo. Akasema: ((Basi soma katika siku saba na usizidishe juu ya hivyo, kwani mke wako ana haki na wewe, na wageni wako wana haki kwako, na mwili wako una haki kwako)). Akasema: Kila nikimkazania (nizidishe ‘ibaadah) alikuwa akinikazania (nipunguze). Akasema: Akaniambia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Huenda umri ukawa mrefu kwako)) Nikaendeleza (‘ibaadah) kama alivyoniambia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Nilipokuwa mkubwa kiumri nilipendelea kufuata rukhsa aliyonipa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]
from Alhidaaya.com http://bit.ly/2FZU5IF
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni