FADHILA ZA DUA
Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh
Fadhila za du’aa ni nyingi mno, zifuatazo ni baadhi ya fadhila zake:
1- Du’aa ni ‘Ibaadah
Juu ya kuwa ‘ibaadah zetu hazimfai wala kumnufaisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) chochote, lakini Yeye (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anatuhimiza tumkabili kumuomba:
عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فِي قَوْلِهِ ((وَقَالَ رَبُّكُمْ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ)) قَالَ: ((الدُّعَاءُ هُوَ الْعِبَادَةُ)) وَقَرَأَ ((وَقَالَ رَبُّكُمْ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ)) إِلَى قَوْلِهِ: ((دَاخِرِينَ))
Amesimulia Nu’maan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika kauli yake [Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa]((Na Rabb (Mola) wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni))Amesema: ((Du’aa ni ‘ibaadah)) kisha akasoma: ((Na Rabb (Mola) wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni)) mpaka kauli Yake: ((daakhiriyn)) [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad – Hadiyth Hasan Swahiyh]
2- Du’aa ni ‘Amali Tukufu Kabisa
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) عَنْ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((لَيْسَ شَيْءٌ أَكْرَمَ عَلَى اللَّهِ تَعَالَى مِنْ الدُّعَاءِ))
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna kitu kitukufu mbele ya Allaah kama du’aa)) [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad, na amesema At-Tirmidhiy: Hasan Ghariyb na ameisahihisha Ibn Hibbaan, Al-Haakim na ameipa muwafaka Adh-Dhahaabiy na ameipa daraja ya Hasan Al-Albaaniy katika Swahiyh Adaab Al-Mufrad]
3- Du’aa Inadhihirisha Tawhiyd ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa)
Mja anapomkabili Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa kumuomba du’aa, huwa anamkabili kwa aina zote za Tawhiyd; kwani huwa ameamini kwamba ni Rabb, Mola Muumba, (Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah) na kwamba Yeye Pekee Ndiye Anayestahiki kuabudiwa na kuombwa (Tawhiyd Al-Uluwhiyyah), na kwamba Yeye Ndiye Mwenye Majina Mazuri kabisa na Sifa Zake (Tawhiyd Al-Asmaa wasw-Swifaat).
4- Kuomba Du’aa Ni Kujikurubisha Na Allaah(Subhaanahu wa Ta’aalaa) kama Anavyosema:
وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ
Na watakapokuuliza waja Wangu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Mimi, basi Mimi ni Qariyb (Aliye karibu kwa ujuzi Wake); [Al-Baqarah 2: 186]
5- Kuomba Du’aa ni Sifa mojawapo ya ‘Ibaadur-Rahmaan’ (Waja wa Mwingi wa Rahmah)
Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Ametaja baadhi ya sifa ambazo Amezihusisha na waja Wake aliowaita ‘Ibaadur-Rahmaan katika Suwratul-Furqaan. Miongoni mwa sifa hizo ni kuomba du’aa mbili zifuatazo:
وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ ۖ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا ﴿٦٥﴾
Na wale wanaosema: “Rabb (Mola) wetu! Tuepushe adhabu ya (Moto wa) Jahannam. Hakika adhabu yake daima ni yenye kugandamana (isiyomwacha mtu).” [Al-Furqaan 25: 65]
وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا ﴿٧٤﴾
Na wale wanaosema: “Rabb (Mola) wetu! Tutunukie katika wake zetu na dhuria wetu viburudisho vya macho yetu, na Tujaalie kuwa waongozi kwa wenye taqwa. [Al-Furqaan 25: 74]
6- Kuomba Du’aa ni Miongoni Mwa Sifa za Watu wa Jannah:
Waumini watakapokuwa Jannah hawatakuwa na la kuwashughulisha kama wanavyoshughulika duniani, bali ni starehe tupu na maombi yao na kauli zao zitakuwa ni kumtakasa, kumtukuza na kumhimidi Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kama Anavyosema:
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ يَهْدِيهِمْ رَبُّهُم بِإِيمَانِهِمْ ۖتَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ﴿٩﴾ دَعْوَاهُمْ فِيهَا سُبْحَانَكَ اللَّـهُمَّ وَتَحِيَّتُهُمْ فِيهَا سَلَامٌ ۚوَآخِرُ دَعْوَاهُمْ أَنِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿١٠﴾
Hakika wale walioamini na wakatenda mema, Rabb (Mola) wao Atawaongoza kwa iymaan zao. Zitapita chini yao mito katika Jannaat za neema (za kila aina).
Wito wao humo (utakuwa) ni: “Subhaanaka-Allaahumma” (Utakasifu ni Wako ee Allaah). Na maamkizi yao humo ni “Salaam” (amani). Na wito wao wa mwisho ni ‘AlhamduliLLaahi (Himidi zote Anastahiki Allaah) Rabb (Mola) wa walimwengu. [Yuwnus 10: 9 -10]
7- Du’aa ni Sababu ya Kufunguliwa Milango ya Rahmah na sababu ya Kuondolewa na Balaa Kabla ya Kuteremka:
عَنْ ابْنِ عُمَرَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((مَنْ فُتِحَ لَهُ مِنْكُمْ بَابُ الدُّعَاءِ فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ الرَّحْمَةِ وَمَا سُئِلَ اللَّهُ شَيْئًا يَعْنِي أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ أَنْ يُسْأَلَ الْعَافِيَةَ)) وَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((إِنَّ الدُّعَاءَ يَنْفَعُ مِمَّا نَزَلَ وَمِمَّا لَمْ يَنْزِلْ فَعَلَيْكُمْ عِبَادَ اللَّهِ بِالدُّعَاءِ))
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayefunguliwa mmoja wenu mlango wa du’aa, amefunguliwa mlango wa Rahmah, na Akipendacho Allaah Zaidi kuombwa ni al-‘aafiyah (afya, siha, amani, hifadhi n.k)) Na akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Hakika du’aa inanufaisha (misiba) inayoteremka na isiyoteremka, hivyo basi juu yenu waja wa Allaah kwa kuomba du’aa)) [At-Tirmidhiy na ameipa daraja ya Hasan Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’]
8- Du’aa inaweza kubadilisha Qadar (Majaaliwa):
Majaaliwa yaliyokwishaandikwa katika Lawhum-Mahfuwdhw (Ubao Uliohifadhiwa) mbingu ya saba, haibadilishwi na chochote ila tu kwa du’aa. Mfano ni du’aa ya Qunuwt Al-Witr tunaomba humo Atukikinge na shari Alizozikidhia:
اللّهُـمَّ اهْـدِنـي فـيمَنْ هَـدَيْـت، وَعـافِنـي فـيمَنْ عافَـيْت، وَتَوَلَّـني فـيمَنْ تَوَلَّـيْت، وَبارِكْ لـي فـيما أَعْطَـيْت، وَقِـني شَرَّ ما قَضَـيْت، فَإِنَّـكَ تَقْـضي وَلا يُقْـضى عَلَـيْك، إِنَّـهُ لا يَـذِلُّ مَنْ والَـيْت، (وَلا يَعِـزُّ مَن عـادَيْت) تَبـارَكْـتَ رَبَّـنا وَتَعـالَـيْت.
Ee Allaah! Niongoze pamoja na Uliowaongoza, na Unipe afya njema pamoja na Uliowapa afya njema, na Nifanye kuwa ni mpenzi Wako pamoja na Uliowafanya wapenzi na Nibariki katika Ulichonipa na Nikinge na shari ya Ulilolihukumu kwani Wewe Unahukumu wala Huhukumiwi. Hakika hadhaliliki Uliyemfanya mpenzi (wala hatukuki Uliyemfanya adui) Umebarikika Ee Mola wetu na Umetukuka [Hadiyth ya Al-Hasan bin ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) - Aswhaabus-Sunan wane; Abu Daawuwd [1425], At-Tirmdhiy [464], An-Nasaaiy (1/252), Ibn Maajah [1178], Ahmad (1/200) – na wengineo]
Dalili katika Sunnah:
عَنْ سَلْمَانَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((لاَ يَرُدُّ الْقَضَاءَ إِلاَّ الدُّعَاءُ ولاَ يَزِيدُ فِي الْعُمْرِ إِلاَّ الْبِرُّ))
Kutoka kwa Salmaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hairudishi Qadhwaa ila du’aa na haizidishi umri ila wema)) [At-Tirmidhiy]
9- Kuomba Du’aa Ni Kuepushwa Na Moto
Waumini wenye taqwa watakapoepushwa na Moto huko Aakhirah, watakabiliana na wenzao na kuulizana sababu za kuingizwa kwao Jannah, na kuomba du’aa ni mojawapo wa sababu hizo; Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٢٥﴾ قَالُوا إِنَّا كُنَّا قَبْلُ فِي أَهْلِنَا مُشْفِقِينَ ﴿٢٦﴾ فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْنَا وَوَقَانَا عَذَابَ السَّمُومِ ﴿٢٧﴾ إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلُ نَدْعُوهُ ۖ إِنَّهُ هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ ﴿٢٨﴾
Na watakabiliana baadhi yao kwa wengineo wakiulizana.
Watasema: “Hakika sisi tulikuwa kabla kwenye ahli zetu wenye kuogopa (kumuasi Allaah).
Basi Allaah Akatufanyia fadhila na Akatuokoa na adhabu ya Moto unaobabua.
Hakika sisi tulikuwa kabla Tunamuomba (Yeye Pekee), hakika yeye Ndiye Al-Barrur-Rahiym (Mwingi huruma na fadhila - Mwenye kurehemu).” [Atw-Twuwr 52: 25- 28]
Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) alipokuwa akisoma Aayah hizi, akiomba du’aa:
"اللَّهُمَّ مُنَّ عَلَيْنَا وَقِنَا عَذَاب السَّمُوم إِنَّك أَنْتَ الْبَرّ الرَّحِيم"
‘Ee Allaah, Tufanyie fadhila, na Tuepushe na adhabu Moto unaobabua, hakika Wewe ni Al-Barrur-Rahiym (Mwingi huruma na fadhila - Mwenye kurehemu).”[Tafsiyr Ibn Kathiyr]
10- Kuomba Du’aa Ni Kufuata Sunnah Za Manabiy, Na Nyendo Za Salaf.
Kuhusu Manabiy, Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwamba kuomba du’aa ilikuwa ni shani yao. Manabiy walipokosea walirudi kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kuomba maghfirah na msamaha.
Iliwasibu Manabiy balaa, maudhi, madhara na shari za kila aina kutoka kaumu zao baada ya kuwalingania Ujumbe wa Allaah. Walipotaka nusura, walitumia du’aa kuwa ni ufumbuzi, utatuzi wa mashakili yao wapate faraja. Mfano kuhusu Nuhw (‘Alayhis-salaam) aliposhindwa kabisa baada na kaumu yake:
كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ فَكَذَّبُوا عَبْدَنَا وَقَالُوا مَجْنُونٌ وَازْدُجِرَ ﴿٩﴾ فَدَعَا رَبَّهُ أَنِّي مَغْلُوبٌ فَانتَصِرْ ﴿١٠﴾
Walikadhibisha kabla yao watu wa Nuwh, wakamkadhibisha mja Wetu, wakasema: “Majnuni.” Na akakaripiwa (kuwekewa vitisho).
Basi akamwita Rabb (Mola) wake kwamba: “Hakika mimi nimeshindwa nguvu basi Nusuru.” [Al-Qamar 54: 9-10]
Mfano wa Nabiy Zakariyyah alipotamani mwana ili amrithi katika Unabiy:
وَزَكَرِيَّا إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ رَبِّ لَا تَذَرْنِي فَرْدًا وَأَنتَ خَيْرُ الْوَارِثِينَ ﴿٨٩﴾ فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَوَهَبْنَا لَهُ يَحْيَىٰ وَأَصْلَحْنَا لَهُ زَوْجَهُ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ ﴿٩٠﴾
Na Zakariyyaa alipomwita Rabb (Mola) wake (kuomba): “Rabb wangu! Usiniache pekee; Nawe Ndiye Mbora wa wenye kurithi.”
Basi Tukamuitikia (du’aa yake), na Tukamtunukia Yahyaa, na Tukamtengenezea mke wake. Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri, na (walikuwa) wakituomba kwa matumaini na khofu, na walikuwa Kwetu wenye kunyenyekea. [Al-Anbiyaa 21: 89-90]
Na mifano mingineyo mbali mbali ya du’aa za Manabiy katika katika Qur-aan. [Rejea mlango wa Du’aa katika Qur-aan]
Ilikuwa pia ni nyendo za Salafus-Swaalih ambao wakimuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa unyenyekevu nyakati za usiku:
إِنَّمَا يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا الَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا بِهَا خَرُّوا سُجَّدًا وَسَبَّحُوا بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ ۩﴿١٥﴾ تَتَجَافَىٰ جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿١٦﴾
Hakika wanaamini Aayaat Zetu wale wanapokumbushwa nazo huporomoka kusujudu, na wakasabbih kwa Himidi za Rabb (Mola) wao, nao hawatakabari.
Mbavu zao zinatengana na vitanda, wanamuomba Rabb (Mola) wao kwa khofu na matumaini, na katika yale Tuliyowaruzuku wanatoa. [As-Sajdah [32: 15-16]
11- Kuomba Du’aa Ni Amali Mojawapo Itendwayo Na Malaika Kuwaombea Waumin:
الَّذِينَ يَحْمِلُونَ الْعَرْشَ وَمَنْ حَوْلَهُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيُؤْمِنُونَ بِهِ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَيْءٍ رَّحْمَةً وَعِلْمًا فَاغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا وَاتَّبَعُوا سَبِيلَكَ وَقِهِمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ﴿٧﴾ رَبَّنَا وَأَدْخِلْهُمْ جَنَّاتِ عَدْنٍ الَّتِي وَعَدتَّهُمْ وَمَن صَلَحَ مِنْ آبَائِهِمْ وَأَزْوَاجِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٨﴾ وَقِهِمُ السَّيِّئَاتِ ۚ وَمَن تَقِ السَّيِّئَاتِ يَوْمَئِذٍ فَقَدْ رَحِمْتَهُ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٩﴾
Wale (Malaika) wanaobeba ‘Arsh na walio pembezoni mwake, wanasabbih kwa Himidi za Rabb (Mola) wao, na wanamwamini; na wanawaombea maghfirah wale walioamini: “Rabb wetu! Umekienea kila kitu kwa Rahmah na elimu. Basi waghufurie wale waliotubu, na wakafuata njia Yako, na wakinge na adhabu ya (Moto wa) Al-Jahiym.”
“Rabb (Mola) wetu! Waingize Jannaat ya ‘Adn ambayo Umewaahidi, pamoja na waliotengenea miongoni mwa baba zao, na wake zao, na dhuria wao. Hakika Wewe Ndiye Al-’Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika - Mwenye hikmah wa yote).
“Na wakinge maovu, kwani Unayemkinga na maovu Siku hiyo, basi kwa yakini Umemrehemu. Na huko ndiko kufuzu adhimu. [Ghaafir 40: 7-9)]
12- Kuomba Du’aa Ni Dalili Ya Wenye Akili Wanaothibitisha Tawhiyd
Wenye akili hutafakari uumbaji wa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake. Hutafakari pia jinsi Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anavyoendesha mambo yote ya ulimwengu kwa ajili ya walimwengu.
Hapo hutambua utukufu na uwezo wa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa), kisha huomba du’aa. Basi hao Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amewasifu kuwa ni dalili ya ‘wenye akili’:
إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ﴿١٩٠﴾ الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَـٰذَا بَاطِلًا سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ﴿١٩١﴾ رَبَّنَا إِنَّكَ مَن تُدْخِلِ النَّارَ فَقَدْ أَخْزَيْتَهُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ ﴿١٩٢﴾ رَّبَّنَا إِنَّنَا سَمِعْنَا مُنَادِيًا يُنَادِي لِلْإِيمَانِ أَنْ آمِنُوا بِرَبِّكُمْ فَآمَنَّا ۚ رَبَّنَا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَكَفِّرْ عَنَّا سَيِّئَاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ الْأَبْرَارِ ﴿١٩٣﴾ رَبَّنَا وَآتِنَا مَا وَعَدتَّنَا عَلَىٰ رُسُلِكَ وَلَا تُخْزِنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ إِنَّكَ لَا تُخْلِفُ الْمِيعَادَ ﴿١٩٤﴾
Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko (ya mfuatano) ya usiku na mchana; bila shaka ni Aayaat (ishara, dalili, zingatioa n.k) kwa wenye akili.
Ambao wanamdhukuru Allaah (kwa) kusimama, na (kwa) kukaa na (kwa) kulala ubavuni mwao na wanatafakari katika kuumbwa mbingu na ardhi (wakisema): “Rabb (Mola) wetu, Hukuumba haya bure. Subhaanak! (Utakasifu ni Wako!) Tukinge na adhabu ya Moto.
Rabb (Mola) wetu, hakika Umuingizaye Motoni, kwa yakini Umemhizi. Na madhalimu hawana yeyote mwenye kuwanusuru.
Rabb (Mola) wetu, hakika sisi tumemsikia mwitaji anaita kwenye iymaan kwamba ‘mwaminini Rabb wenu’ basi tukaamini. Rabb (Mola) wetu, Tughufurie madhambi yetu na Tufutie makosa yetu na Tufishe pamoja na Al-Abraar (Waumini wema).
Rabb (Mola) wetu na Tupe Uliyotuahidi kupitia Rasuli Wako, wala Usituhizi Siku ya Qiyaamah; hakika Wewe Huendi kinyume na miadi”. [Aal-‘Imraan 3: 190-194]
Fadhila zao Waumini hao wenye kuomba du’aa hizo, ni kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amewatakabalia du’aa zao, na Amewaghufuria maovu yao, na Amewaahidi mengi mazuri pamoja na kuwaingiza katika Jannah Yake yenye neema [Aal-‘Imraan 3: 195-199]
Tutaendelea In Shaa Allaah......
Na Allaah anajua zaidi
from fisabilillaah.com https://ift.tt/2R38XLA
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni