Translate

Jumapili, 31 Machi 2019

Hukmu ya Siku ya Wajinga

HUKUMU YA SIKU YA WAJINGA (APRIL FOOL)

 


بسم الله الرحمن الرحيم


 

 

BismiLLaah walhamduliLLaah Rabbil 'Aalamiyn. Wasw-Swalaatu was-Salaamu ‘alaa Nabbiyihi Asw-Swaadiq Al-Amiynwa ‘alaa aalihi wa Swahaabatihi Al-Ghurr Al-Mayaamiyn, wa man Tabi'ahum bi Ihsaani ilaa Yawmid Diyn.

Amma ba’d:

 

 

ASILI YA APRIL FOOL

 

Asili ya April Fool haikujulikana kwa uhakika na kuna rai mbali mbali zinazohusiana nayo.

 

Wengine wamesema imeanza kutokana na sherehe za majira ya kuchipua (Spring) katika ikwinoksi (siku ya mlingano) tarehe 21 Machi.

 

Wengine wamesema kuwa huu ni uzushi uliochomoza France mwaka 1564 M, baada ya utangulizi wa kalenda mpya. Wakati mtu alipogoma kukubali kalenda mpya akaishia kuwa ni mwathirika wa baadhi ya watu ambao wamemsababisha aathirike kufedheheka na wakamfanyia istihzai na kumtania, akawa ni kichekesho kwa watu.

 

Wengine wanasema kuwa uzushi huu umeanza asili yake katika nyakati za kale na sherehe za mapagani zilikuwa na uhusiano na siku hasa mwanzo wa majira ya kuchipua. Kwa hiyo hii ni kasumba ya ibada za mapagani. Inasemekana kuwa nchi nyingine, kuwinda hakukufaulu siku za mwanzo za uwindaji.

 

 

Le poisson d'avril (Samaki wa Aprili)

 

Wazungu wameiita April Fool kwa jina la 'le poisson d'avril' (Samaki wa Aprili). Na sababu hii ni kutokana na jua linavyosogea kutoka nyumba ya zodiaki (nyota za unajimu) ya Pisces (Nyota ya samaki) ikielekea nyumba nyingine. Au kwa sababu ya neno la poisson ambalo maana yake ni samaki, hivyo ni ugeuzaji wa neno la 'passion' ambayo ina maana ya 'kuteseka'. Kwa hiyo ni alama ya kuteseka aliyovumulia Nabii 'Iysaa (Alayhis Salaam) kama walivyodai Wakristo. Na madai yao haya yalitokea wiki ya kwanza katika mwezi wa April.

 

Baadhi ya makafiri wameiita siku hii 'Siku nzima ya wajinga' kama inavyojulikana Kingereza. Hii ni kwa sababu uongo wanaousema ili wale wanaousikia waamini kwa hiyo wanakuwa ni waathirika wa wale wanaowafanyia dhihaka.

 

Utajo wa mwanzo kabisa kwa Lugha ya Kingereza ilikuwa ni katika gazeti la Dreck. Siku ya pili ya Aprili 1698 M, gazeti hili lilitaja kwamba idadi kadha ya watu walialikwa kuhudhuria uoshaji wa watu weusi katika mnara wa London asubuhi ya siku ya mwanzo ya Aprili.

 

Tukio maarufu kabisa lililotokea Ulaya tarehe 1 Aprili lilikuwa wakati gazeti la Kingereza 'Evening star' lilipotangaza mwezi wa Machi 1746 M kwamba siku ya pili tarehe 1 Aprili, kutakuwa na gwaride la punda mji wa Islington Uingereza. Watu wakakimbilia kuwatazama wanyama hao na kulikuwa na zahma kubwa. Wakaendelea kusubiri na walipochoka kusubiri, waliuliza kutaka kujua hili gwaride litakuweko baada ya muda gani. Hawakupata jibu, hivyo wakatambua kuwa wamekuja kufanya maonyesho yao wenyewe kama kwamba wao ndio mapunda.

 

Mmoja wao ameandika kuhusu asili ya uzushi huu kwa kusema: Wengi wetu tunasherehekea siku inayojulikana kuwa ni April Fool, au ikiwa itafasiriwa kihalisi 'Siku ya Ujanja'. Lakini je, tunajua siri chungu inayohusikana na siku hii?

 

Habari nyingine ambazo usahihi wake umetiliwa shaka na wanahistoria ni kuwa:

Waislamu walipotawala Hispania (Spain) takriban miaka elfu iliyopita, kulikuwa na nguvu kubwa ya utawala wa Kiislam ambayo haikuwezekana kuivunja. Wakristo wa Kimagharibi walitamani kuufuta Uislamu katika mgongo wa ardhi na walifaulu kwa kiwango fulani.

 

Walijaribu kuzuia Uislamu kusambaa Hispania na walitaka kuuzima na wautoweshe kabisa lakini hawakufaulu, ingawa walijaribu mara nyingi bila ya kufaulu.

 

Baada ya hapo, makafiri walituma majasusi Hispania kufanya utafiti ili kujua siri ya nguvu za Waislamu ambayo haikuwezekana kuishinda. Wakatambua kuwa kushikamana na Taqwa (Uchaji Allaah) ndio sababu.

 

Wakristo walipotambua siri ya nguvu za Waislamu, wakaanza kufikiria mikakati za kuvunja nguvu hiyo. Na kwa ajili hii wakaanza kupeleka ulevi na sigara bure huko Hispania.

 

Mbinu hizi kwa upande wa Magharibi zilifaulu kuleta taathira na imani za Waislamu zikaanza kulegea, hasa miongoni mwa vizazi vipya Hispania. Matokeo yake ni kwamba Wakristo Wakatholiki waliikandamiza Hispania nzima na wakauangamiza utawala wa Kiislamu katika ardhi hiyo, utawala ambao ulidumu zaidi ya miaka mia. Ngome ya mwisho ya Waislamu Grenada ilianguka tarehe 1 Aprili, hivyo wakaichukulia kuwa ni 'Siku ya Ujanja ya Aprili' au 'Siku ya Wajinga ya April'.  Ujanja kwa wale walioufanya, na Ujinga kwa wale waliofanyiwa na kutumbikia ndani yake.

 

Tokea mwaka huo hadi sasa, wanasherehekea siku hii na wanachukulia kuwa Waislamu ndio wajinga. Hawakuuhusisha ujinga huu na jeshi la Granada pekee kuwa ni wajinga, bali wamekusudia kuwa ni Umma wa Kiislamu mzima kuwa ni wajinga.

 

Hata hivyo, habari hizi tumezinukuu hapa kwa kuwa zimeenea sana miongoni wa Waislam, lakini kama tulivyotangulia kueleza, ni kuwa, uhakika na ukweli wake una mashaka kwa sababu kuna wanaosema kuwa wakati huo sigara na uvutaji tumbaku ulikuwa haujaanza hadi baada ya kushindwa Waislamu huko Hispania. 

 

Wahahistoria wanasema sababu za kushindwa Waislamu zilikuwa ni wenyewe kujiingiza zaidi kwenye mapenzi ya kidunia na starehe, pamoja na kuacha mafundisho sahihi ya Uislam na badala yake kuchanganya zaidi na falsafa ya Kigiriki na kutegemea zaidi fikra za kirumi katika kuendesha mambo yao badala ya mwongozo imara wa Kiislam. Kadhalika kuna Waislamu waliokuwa wakishirikiana na makafiri katika kupambana na makundi mengine ya Kiislam waliyokuwa hawaelewani nayo kama tunavyoona leo hii.

 

 

BAADHI YA UDANGANYIFU WANAODANGANYANA WATU KATIKA

SIKU HII YA APRIL FOOL

 

Wengine wanapewa habari ya mmoja wa kipenzi chake katika familia kama mtoto, mke au mume kwamba amefariki na kwa wengine taarifa hizo husababisha hata kifo chao kutokana na kutokustahamili kupata mshtuko huo. Wengine wanapewa habari ya kufukuzwa kazi, au kuwashtua kwa habari mbaya kama kuunguliwa moto nyumba yake, au familia yake kupata ajali, na husababisha aathirike mtu kwa mshtuko huo hadi apate maradhi ya moyo, au maradhi ya kupooza au hata kifo cha ghafla. 

 

Wengine wadanganywe kuwa wake zao wameonana na wanaume wengine, jambo ambalo husababisha mauaji au talaka ya wake. 

 

Kuna visa visivyokuwa na mwisho na matukio yanayotokea kutokana na uongo huu. Uongo ambao umeharamishwa katika Uislamu na ambao haukubaliwi katika tabia za kiungwana.

 

 

HUKUMU YA UONGO KATIKA UISLAMU

 

Uongo ni tabia ovu kabisa ambao dini zote na mfumo wa elimu za maadili zimeonya dhidi yake, na pia asili ya kimaumbile ya binaadamu (fitrah) inakubaliana kuwa ni uovu.

 

Ukweli ni moja wa nguzo ambayo maadili ya maisha ya kidunia yanategemea ili yahifadhike. Ni asasi ya tabia za kustahili kusifiwa, ni msingi wa Utume na matokeo ya Taqwa. Isingelikuwa ni ukweli, hukumu za shariy'ah za kufunuliwa kutoka mbinguni zingeliporomoka. Kuwa na tabia ya uongo ni ujamaa wa kupukusa tabia pekee ya ubinaadamu, kwani kuzungumza uongo ni uangamizaji wa hali ya kibinaadamu. 

 

Shariy'ah ya Kiislamu; Qur-aan na Sunnah inatuonya kusema uongo na kwa makubaliano ya wanachuoni kwamba ni haramu. Mtu muongo atachuma malipo mabaya duniani na Aakhirah.

 

Katika shariy'ah, kuongopa hakuruhusiwi ila katika hali fulani ambazo hazipotezi haki za mtu, au kumwaga damu au kufedhehesha, au kumvunjia mtu heshima yake. Bali katika mas-alah ya kuokoa maisha, kusuluhisha baina ya watu au kujenga mapenzi baina ya mume na mke umeruhusiwa uongo. Wala shariy'ah haikumruhusu mtu aseme uongo wa utani usio na maana kama huu wa April Fool.

 

 

MAKATAZO YA KUSEMA UONGO

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala) Anasema:

((إِنَّمَا يَفْتَرِي الْكَذِبَ الَّذِينَ لاَ يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِ اللّهِ وَأُوْلئِكَ هُمُ الْكَاذِبُونَ))

((Wanaozua uongo ni wale tu wasioziamini Ishara za Allaah. Na hao ndio waongo)) [An-Nahl: 105]

 

Ibn Kathiyr amesema kuhusu Aayah hiyo:

"Allaah Anatuambia kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) sio mzushi au muongo, kwa sababu ni watu waovu tu ambao hawaamini alama za Allaah, makafiri na wanafiki wanaojulikana baina ya watu kwa uongo wao, uongo kuhusu Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ni mkweli kabisa miongoni mwa watu, mchaji Allaah, mwenye elimu bora kabisa, mwenye matendo mema, tabia njema. Hakuna aliyekuwa na shaka naye hadi kwamba aliitwa 'Al-Amiyn' (Mkweli). Hivyo Hercules, mfalme wa Rome alipomuuliza Abu Sufyaan kuhusu tabia za Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), jambo moja alilouliza lilikuwa ni: "Je, mmepata kumtuhumu kwa uongo kabla ya kusema aliyoyasema?". Alijibu: "Hapana". Hercules akasema: "Ikiwa alijiepusha kusema uongo kwa watu basi hawezi kusema uongo kuhusu Allaah". [Tafsiyr Ibn Kathiyr, 2/588].

 

Imetoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Alama za munaafiq ni tatu; akizungumza husema uongo, akitoa ahadi huivunja, akiaminishwa kwa kitu hufanya khiyana" [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

UONGO ULIO MUOVU KABISA

 

1. Uongo Kuhusu Allaah Na Mtume Wake (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa aalihi Wa Sallam)

Huu ni uongo wa hatari kabisa na anayezua hivyo basi hupewa onyo kali. Baadhi wa Maulamaa wamesema kwamba anayezua uongo kama huu basi ashutumiwe kuwa kafiri.

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

((قُلْ إِنَّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللّهِ الْكَذِبَ لاَ يُفْلِحُونَ))

((Sema: Hao wanaomzulia uongo Allaah hawatofanikiwa)) [Yuunus: 69]

 

Imetoka kwa 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Msinizulie uongo. Yeyote atakayezua uongo kuhusu mimi basi ataingia motoni)) [Al-Bukhaariy]

 

Imetoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Yeyote atakayenizulia uongo basi ajitayarishie makazi yake motoni)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Ibnu Al-Qayyim amesema kuhusu maana ya Hadiyth hii kwamba:  "Yeyote atakayezua uongo kuhusu mimi basi ajitayarishie makazi yake motoni ambako ataishi milele, na sio kama kambi ambayo mtu huishi kwa muda kisha akahamia kwengine" [Twariyqul-Hijratayn ukurasa 169]

 

 

2. Uongo Katika Kununua Na Kuuza

Uongo mwengine ni wakati mtu anapofanya biashara na katika kununua huzua na kuuza pia hudanganya.

 

Imetoka kwa Abuu Dharr (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Watu watatu ambao Allaah Hatosema nao siku ya Qiyaamah na wala Hatowatazama wala kuwatukuza, na watapata adhabu iumizayo)) Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema mara tatu. Abu Dharr akasema: "Waangamizwe na wapotezwe, ni nani hao ewe Mjumbe wa Allaah?" Akasema: (([mwanaume] Mwenye kuachia nguo yake ivuke kiwiko cha mguu, mwenye kujisifu, na mwenye kufanya biashara yake kwa kuapa uongo)). [Muslim] 

 

Imesimuliwa na Hakiym bin Hizaam (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Watu wawili wanaohusika na makubaliano ya biashara wanayo khiyari (ya kuvunja makubaliano) hadi watakapofarikiana. Ikiwa waaminifu makubaliano yao yatabarikiwa na wakikhini kitu na kusema uongo, baraka itafutwa katika makubaliano yao)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Allaah Ameusia ukweli na uaminifu, na Ameharamisha uongo na khiana katika mambo yapasayo kujulikana na kufunuliwa kwa watu kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Watu wawili wanaohusika na makubaliano ya biashara wanayo khiari (ya kuvunja makubaliano) hadi watakapofarikiana. Ikiwa waaminifu makubaliano yao yatabarikiwa na wakikhini kitu na kusema uongo, baraka itafutwa katika makubaliano yao)) na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala) Anasema:

((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ كُونُواْ قَوَّامِينَ لِلّهِ شُهَدَاء بِالْقِسْطِ وَلاَ يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَى أَلاَّ تَعْدِلُواْ اعْدِلُواْ هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَى))  

((Enyi walioamini!  Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Allaah mkitoa ushahidi kwa uadilifu. Na wala chuki ya watu isikuchocheeni kutokufanya uadilifu. Fanyeni uadilifu; hivyo ni karibu zaidi na taqwa. Na mcheni Allaah; hakika Allaah ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika kwa yale myatendayo.)) [Al-Maaidah: 8] [Minhaajus-Sunnah 1/16]

 

 

3. Kuharamishwa Uongo Kuhusu Njozi Na Ndoto

Hii ni kuhusu baadhi ya watu wanaodai kuwa wameona ndoto kadhaa kisha asubuhi wanawasimulia watu mambo ambayo wala hawakuyaona.

 

Imetoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhuma) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Yeyote atakayesimulia ndoto ambayo hakuiona, ataamrishwa (Siku ya Qiyaamah) aunganishe pamoja chembe mbili za shayiri, lakini hatoweza. Yeyote atakayetega masikio (kwa umbea) kusikiliza mazungumzo ya watu ambao wasingelipenda (yeye asikilize), au ambao wanamuepuka atamiminiwa shaba ya moto iliyoyeyushwa katika masikio yake siku ya Qiyaamah. Na Yeyote atakayetengeneza (kuchora au kuchonga) picha ataadhibiwa na ataambiwa aitie uhai (roho) na wala hatoweza)) [Al-Bukhaariy] 

 

Katika kufafanua Hadiyth hiyo, Wanachuoni wanasema: "Kuunganisha shayiri mbili, lakini hatoweza kufanya hivyo" kwa sababu kuiunga moja kwa mwenziwe haiwezekani kikawaida. Ataadhibiwa mpaka aweze kuziunga, na wala hataweza kuziunga. Kama kwamba anasema, ameshurutishwa kufanya jambo asiloliweza na anaadhibiwa kwa hilo. Hii ni sitiari ya adhabu inayoendelea. Sababu ya kutajwa shayiri hasa, ni kwamba ndoto zina uhusiano na hisia (Kwa Kiarabu hisia ni shu'uur), maneno ya shayiri na shu'uur yanatokana na mzizi (asili ya neno) mmoja katika Kiarabu.

 

Adhabu ya aina hii ya uongo ni kali sana ingawa anapokuwa macho huenda akasababisha madhara zaidi, kwa sababu huenda yakahusiana na kutoa ushahidi na huenda yakampelekea kuuliwa au kupewa adhabu ya hadd. Hii ni kwa sababu kusema uongo kuhusu ndoto ni kumzulia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala) kwani ndoto ni sehemu ya Utume, hivyo zinatoka Kwake. Na kumzulia Muumba ni khatari zaidi kuliko kuwazulia viumbe.

 

 

4. Kuharamishwa Kusema Kila Anachokisikia Mtu

Imesimuliwa kwamba Hafsw bin 'Aaswim amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Inatosheleza kuwa ni uongo kwa mtu anayesema kila anachokisikia)) [Muslim]

 

"Kutokana na maana ya Hadiyth kuhusu maudhui hii, tunaona kwamba inakatazwa kutaja au kuhadithia kila jambo analolisikia mtu, kwa sababu kawaida mtu anasikia yote ya kweli na uongo. Kwa hiyo ikiwa atasema kila anachokisikia atakuwa anasema uongo kwa kusema jambo lisilotokea. Tumetaja juu rai za watu wakweli, kwamba uongo una maana kwamba kusema au kuelezea jambo katika hali dhidi ya lilivyotokea. Sio sharti juu yake ikiwa limefanyika makusudi lakini kufanyika kwake makusudi kunashurutisha kuwa ni dhambi. Na Allaah Anajua zaidi" [Sharh Muslim,1/75]

 

 

5. Uongo Wa Utani

Watu wengine wanadhania kwamba inaruhusiwa kusema uongo wakati wa utani. Na huu ndio udhuru wanaoutoa katika kuongopa siku ya terehe 1 Aprili au siku nyinginezo. Hayo ni makosa. Hakuna msingi wa jambo hili katika sharia safi. Kuongopa ni haraam ikiwa ni kwa kutania au kwa dhati. Kuongopa kwa kutania ni haramu sawa sawa na kuongopa kwa aina yoyote nyingine.

 

Imesimuliwa kwamba 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mimi hutania lakini sisemi ila ni ya kweli)) [At-Twabaraaniy katika 'Al-Mu'jam Al-Kabiyr 12/391 – Hadiyth hii imepewa daraja ya hasan na Al-Haythamiy katika Majma' Az-Zawaaid 8/89 na Shaykh Al-Albaaniy ameipa daraja ya sahihi katika Swahiyh Al-Jaami' 2394]]

 

Imesimuliwa kwamba amesema: "Walisema, ee Mjumbe wa Allaah, unafanya utani na sisi". Akasema: ((Lakini nnayoyasema ni ukweli tu)) [At-Tirmidhiy]

 

'Abdur-Rahmaan bin Abiy Laylaa amesema: "Maswahaba wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wametuambia kuwa walikuwa safarini pamoja na Mjumbe wa Allaah. Mtu mmoja miongoni mwao alilala na baadhi yao walikwenda kuchukua mishale yake. Alipoamka alishtuka (alipoona mishale yake haipo). Watu wakacheka. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Mnacheka nini?)) Wakasema: "Hakuna kitu isipokuwa tumechukua mishale yake na ameshtuka". Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Haimpasi Muislamu kumtisha Muislamu mwingine)) [Abuu Daawuwd, Ahmad na Shaykh Al-Albaaniy ameipa daraja ya Swahiyh katika Swahiyh Al-Jaami']

 

Imesimuliwa kutoka kwa 'Abdullaah bin As-Saa'ib bin Yaziyd kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake kwamba amemsikia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Haimpasi yeyote katika nyinyi kuchukua kitu cha ndugu yake, ikiwa ni kwa utani au kwa vyovyote. Yeyote aliyechukua kijiti cha ndugu yake basi akirudishe)) [Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Shaykh Al-Albaaniy ameipa daraja ya hasan katika Swahiyh Al-Jaami']

 

 

6.    Kuongopa Wakati Wa Kucheza Na Watoto

Lazima tutahadhari na kusema uongo tunapocheza na watoto kwa sababu itaandikwa katika kitabu cha hesabu. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameonya jambo hili.

 

Imesimuliwa kwamba 'Abdullaah bin 'Aamir (Radhwiya Allaahu 'anhu) alisema: "Siku moja mama yangu aliniita wakati alipokuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameketi nyumbani kwetu. Akasema: Njoo hapa nikupe (kitu). Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Je, unataka kumpa nini?)) Akasema: 'Nitampa tende'. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Kama usingelimpa basi ungelikuwa unasema uongo)).

 

Na imesimuliwa kwamba Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Yeyote atakayemuambia mtoto 'njoo hapa uchukue hii' kisha asimpe kitu basi itahesabiwa ni uongo)) [Abuu Daawuwd na Shaykh Al-Albaaniy ameipa daraja ya hasan katika Swahiyh Al-Jaami']

 

 

7.    Uongo Ili Kuchekesha Watu

Imesimuliwa kwamba Mu'aawiyah bin Hadah amesema: "Nimemsikia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Ole wake mtu anayezungumza kwa ajili ya kuwachekesha watu na akasema uongo, ole wake, ole wake)) [At-Trimidhiy akisema ni hadiyth hasan na Abuu Daawuwd]

 

 

ADHABU KWA AJILI YA KUSEMA UONGO

 

Mwenye kusema uongo amepewa onyo kali la adhabu ya hizaya duniani na adhabu kali Aakhirah nazo ni kama zifuatazo:

 

Unafiki Katika Moyo

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala) Anasema:

((فَأَعْقَبَهُمْ نِفَاقًا فِي قُلُوبِهِمْ إِلَى يَوْمِ يَلْقَوْنَهُ بِمَا أَخْلَفُواْ اللّهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُواْ يَكْذِبُونَ))

((Basi Akawalipa unafiki kuutia nyoyoni mwao mpaka Siku watapokutana Naye, kwa sababu ya kuwa walimkhalifu Allaah katika yale waliyomuahidi, na kwa sababu ya kusema kwao uongo))[At-Tawbah: 77]

 

'Abdullaah bin Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Unaweza kumjua mtu mnafiki kwa mambo matatu; anaposema anaongopa, anapotoa ahadi anaivunja, anapoaminiwa na amana hufanyakhiyana". Akasema: "Someni aya hizi:

وَمِنْهُم مَّنْ عَاهَدَ اللّهَ لَئِنْ آتَانَا مِن فَضْلِهِ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ الصَّالِحِينَ))

 ((فَلَمَّا آتَاهُم مِّن فَضْلِهِ بَخِلُواْ بِهِ وَتَوَلَّواْ وَّهُم مُّعْرِضُونَ))

((فَأَعْقَبَهُمْ نِفَاقًا فِي قُلُوبِهِمْ إِلَى يَوْمِ يَلْقَوْنَهُ بِمَا أَخْلَفُواْ اللّهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُواْ  يَكْذِبُونَ)) 

((Na miongoni mwao wapo waliomuahidi Allaah kwa kusema: Akitupa katika fadhila Yake hapana shaka tutatoa sadaka, na tutakuwa katika watendao mema)) 

((Alipowapa katika fadhila Yake wakaifanyia ubakhili na wakageuka, na huku wakipuuza))

((Basi Akawalipa unafiki kuutia nyoyoni mwao mpaka Siku watapokutana Naye, kwa sababu ya kuwa walimkhalifu Allaah katika yale waliyomuahidi, na kwa sababu ya kusema kwao uongo))[At-Tawbah: 75-77]

[Muswanaf Ibn Abiy Shaybah, 6/125] 

 

 

Uongo Humpeleka Mtu Motoni

Imesimuliwa kwamba 'Abdullaah bin Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ukweli ni utiifu, na utiifu huelekeza Peponi. Mtu ataendelea kusema ukweli hadi Ataandikiwa na Allaah kuwa ni mkweli. Uongo ni uovu, na uovu huelekeza motoni. Mtu ataendelea kusema uongo hadi Ataandikiwa kuwa ni muongo)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

As-Swan'aaniy amesema:

"Hadiyth hii inaonyesha kwamba yeyote anayeendelea kusema ukweli, itakuwa ni wasifu wake, na yeyote anayesema uongo makusudi na kuendelea, itakuwa ni wasifu wake. Hii ni sawa kama kitendo chochote kingine chema au kiovu. Mtu akiendelea nacho kinakuwa ndio sifa yake.

 

Vile vile Hadiyth hii inaonyesha jinsi gani ilivyo muhimu kusema ukweli hadi kwamba unampeleka mtu Peponi na imeonyesha vipi ubaya wa kusema uongo hadi unampeleka mtu motoni. Juu ya hivyo, bado kuna matokeo ya adhabu za duniya kwani anayesema ukweli atakuwa anakubaliwa usemi wake na watu na ushahidi wake utakubaliwa na jaji na atapendwa kwa yale anayoyasema. Ama mtu muongo ni dhidi ya hayo." [Subul-As-Salaam 2/687]

 

 

Ushahidi Wake Utakanushwa

Ibnul-Qayyim amesema kuhusu sababu ya ushahidi wa mtu muongo kukanushwa:

"Sababu ya nguvu kabisa kwa nini katika kutoa ushahidi, fatwa na ripoti zikanushwe ni kusema uongo, kwa sababu inafisidi asili ya ushahidi, fatwa au taarifa. Ni kama ushahidi wa kipofu kuona mwezi mpya, au ushahidi wa kiziwi kuhusu kusikia kuruhusiwa kuingia mtu mahali. Ulimi unaoongopa ni kama baadhi ya uelekevu ambao haufanyi kazi tena. Hakika ni mbaya zaidi kuliko hivyo, kwani kitendo kiovu kabisa mtu kumiliki ni ulimi muongo." [I’ilaam Al-Muwaqqi'iyn 1/95]

 

 

Nyuso Kuwa Nyeusi Duniani Na Aakhirah           

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala) Anasema:

((وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ تَرَى الَّذِينَ كَذَبُواْ عَلَى اللَّهِ وُجُوهُهُم مُّسْوَدَّةٌ أَلَيْسَ فِي جَهَنَّمَ مَثْوًى لِّلْمُتَكَبِّرِينَ))

((Na Siku ya Qiyaamah utawaona waliomsingizia uongo Allaah nyuso zao zimesawijika (zimekuwa nyeusi). Je! Si katika Jahannamu makaazi ya wanaotakabari?)) [Az-Zumar: 60]

 

Ibnul-Qayyim amesema: "Hivyo siku ya Qiyaamah Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aala) Atazifanya nyuso ziwe alama za waliosema uongo kuhusu Allaah na Mjumbe Wake. Kusema uongo kunaleta taathira kubwa ya kufanya nyuso ziwe nyeusi na kuzifunika na kitambaa cha hizaya na kila mtu mkweli ataziona nyuso hizo. Wasifu wa mtu muongo utatambulikana dhahiri kabisa usoni na kila mtu aliye na macho ataweza kumuona. Lakini Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala) Anambariki mtu mkweli kwa hadhi na heshima ili yeyote atakayemuona atamuheshimu na kumpenda. Na Atampa muongo fedheha na aibu ili yeyote atakayemuona atamchukia na kumdharau. Na Allaah Ni Mwenye Chanzo cha Nguvu" [I'laam Al-Muwaqi'iyn 1/95]

 

 

Mtu Muongo Atachanwa Mashavu Yake Kutoka Kisogoni

Imesimuliwa kwamba Samurah ibn Jundub (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema"Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwaambia mara kwa mara Maswahaba zake: ((Je, kuna yeyote miongoni mwenu aliyeona ndoto?)). Kisha yeyote aliyejaaliwa na Allaah ataelezea ndoto yake. Siku moja alituambia: (([Malaika] Wawili walinijia jana usiku na kuniamsha, kisha wakaniambia: 'Twende…' Tukatoka na kwenda hadi tukafika kwa mtu aliyelala chali na mwengine amesimama juu ya kichwa chake akiwa na ndoana ya chuma. (Akashtuka aliyoyaona na kusema) Na kitu gani cha kutazama! Alikuwa akitia ndoana katika upande mmoja mdomoni mwa mwenzake (aliyelala) akimchana kutoka upande mmoja wa uso hadi nyuma (ya shingo) na hivyo hivyo akiichana pua kutoka mbele hadi nyuma ya macho yake kisha akiendelea kufanya hivyo hivyo kama alivyofanya kwa upande mwingine. Hawahi kumaliza kumchana upande mmoja ila upande mwingine unarudishwa hali yake (ya mwanzo). Kisha hurudia kufanya hivyo hivyo upya tena. Nikasema kwa Maswahaba zangu (Malaika) wawili, 'Subhaanahu Allaah! Ni watu gani hawa wawili?' Wakaniambia: 'Endelea kwenda, endelea kwenda!' (kisha akasema akielezea vipi Malaika wawili wakielezea mambo aliyokuwa akiyaona): 'Ama yule mtu uliyemuona kuwa anachanwa mdomo, pua na macho yake, ni alama ya mtu anayetoka nyumbani kwake asubuhi na kusema uongo mwingi hadi unasambaa duniani kote')) [Al-Bukhaariy]        

 

 

KAULI ZA MASWAHABA KUHUSU UONGO

 

Abuu Bakr As-Swiddiyq (Radhwiya Allaahu 'anhu):   

"Tahadharini na uongo kwani hauna uhusiano na Iymaan".

 

'Umar Ibnul-Khattwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu):  

"Iymaan ya dhaati haiwezi kupatikana hadi mtu aache uongo wa utani"

 

'Abdullaah bin Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu):  

"Mtu atasema ukweli na kuendelea kufanya hivyo hadi hakutakuwa na nafasi ya uovu katika moyo wake japo kama ni wa kiasi cha sindano. Au mtu atasema uongo na kuendelea kufanya hivyo hadi hakutakuwa na nafasi ya ukweli katika moyo wake japo kama ni wa kiasi cha sindano".

 

Vile vile amesema:  "Haimpasi mtu kusema uongo ikiwa ni kwa kutania au kikweli". Kisha Ibn Mas'uud akasoma Ayah:

((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اتَّقُواْ اللّهَ وَكُونُواْ مَعَ الصَّادِقِينَ))

((Enyi mlioamini! Mcheni Allaah, na kuweni pamoja na wakweli)) [At-Tawbah: 119]

 

 Sa'ad bin Abi Waqqaasw (Radhwiya Allaahu 'anhu)    

"Muumini anaweza kuwa na sifa zote isipokuwa usaliti na uongo"

[Muswannaf Ibn Abi Shaybah, 5/235, 236] 

 

 

AINA YA UONGO UNAORUHUSIWA

 

Uongo unaruhusiwa katika hali tatu; kwenye vita, kusuluhisha baina ya watu wawili waliogombana, mume kumuongopea mkewe au kinyume chake kwa ajili ya mapenzi na maelewano.

 

Imesimuliwa kutoka kwa Ummu Kulthuwm bint 'Uqbah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba amemsikia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Sio muongo mwenye kupatanisha baina ya watu na akasimulia jambo zuri au akasema maneno mazuri)) [Al-Bukhaariy, Muslim]  

 

Imesimuliwa kwamba Asmaa bin Yaziyd amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hairuhusiwi kusema uongo isipokuwa katika hali tatu; mtu anapozungumza na mkewe katika njia ya kumfurahisha, kusema uongo katika vita, na uongo kwa ajili ya kusuluhisha baina ya watu)) [At-Tirmidhiy na Shaykh Al-Albaaniy ameipa daraja ya Swahiyh katika Swahiyh Al-Jaami']

 

 

KHITIMISHO

 

Baada ya kutambua chanzo cha siku hiyo ya April Fool, uongo na madhara yake, basi tujitahidi nafsi zetu kutosherehekea siku hiyo kabisa, ili tubakie katika tabia ya ukweli daima. Hata kama si muhimu kujua chanzo cha siku hii, bali lililo muhimu ni kujua hukumu ya kusema uongo na khofu ya adhabu zake kama tulivyopata mafundisho katika Aayah na Hadiyth zilizotangulia.

 

Hiyo ni shariy'ah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ambayo ina Hikma inayorekebisha nafsi za binaadamu kubakia katika hali ya fitrah (asili ya maumbile) ili abakie binaadamu daima ni mwenye kuishi salama na amani katika jamii, na vile vile ajiepushe na adhabu kali Alizoziandaa Mola Mtukufu kwa maovu kama hayo.

 

Mafundisho muhimu na yatakayoonekana mapya kwa wengi wetu tunayoyapata katika makala haya ni kujihadhari na matani yaliyojaa uongo; tukitazama matani mengi hadi yawe matani basi kutakuwepo na uongo ndani yake, na utani haufurahishi kwa wengi hadi uwe na udanganyifu na hila ndani yake, hivyo tujihadhari sana Waislam na uongo kwenye matani. Vilevile tujiepushe na tabia mbaya ambayo baadhi yetu wanaipenda, nayo ni kuleta matani watu wacheke, au kuwafurahisha watu kwa matani. Kuna watu kazi yao kukaa vijiweni na kumwaga matani hadi wakawa wanajulikana kwa sifa hiyo na wasipoonekana siku moja ni pengo kwenye kijiwe! Hadi inafika mtu jina lake kubadilishwa na kuitwa Fulani Matani! Na kuna wengine ambao tabia yao ni kupenda kuwa katika mwangaza daima (kuonekana) na kuwa na tabia ya kujipendekeza na haswa kwa watu wa jinsia tofauti ili akusanye sifa au kupendeka, mwisho akawa anajulikana kwa kufanya sifa hizo na vituko ambavyo vimejaa uongo, matusi, kuigiza wenzake, kebehi n.k.

 

Kadhaalika, tuifuate Hadiyth isemayo:((Mwenye kumuamini Allaah na siku ya mwisho, aseme khayr (maneno mazuri/ukweli) au anyamaze...)) [Hadiyth kutoka kwa Abu Hurayrah iliyosimuliwa na Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Aturuzuku ukweli daima na Ajaalie ndimi zetu ziseme yanayopasa tu kusema na Atujaalie miongoni mwa walioamini na wasemao kweli (Asw-Swiddiyqiyn). Aamiyn.

 



https://ift.tt/2FNNj7K i live islam

Dalili alizotumia al-Albaaniy kuonyesha kuwa inafaa kwa mwanamke kuyatembelea makaburi



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2V9eU8n
via IFTTT

Namna hii mnatakiwa kulingania katika Uislamu

Nimefikiwa na khabari kwamba baadhi yenu mmekemea Bid´ah zinazopatikana makaburi jambo ambalo limesababisha kutokea kwa matatizo. Mambo yakiwa ni hivo kweli basi natarajia kuwa mtalingania kwa Allaah kwa mujibu wa mfumo wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Kwa msemo mwingine muanze kulingania katika Tawhiyd na kumtakasia Allaah nia kwa aina zote za ´ibaadah, na khaswakhaswa du´aa. Kwa sababu watu wengi wamepondoka katika suala hili. Utawaona ni wenye kuwaomba mawalii, wakiwataka uokozi na msaada wakati wa shida na mfano wa hayo. Ilihali Allaah anasema:

وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّن يَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَن لَّا يَسْتَجِيبُ لَهُ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَهُمْ عَن دُعَائِهِمْ غَافِلُونَ وَإِذَا حُشِرَ النَّاسُ كَانُوا لَهُمْ أَعْدَاءً وَكَانُوا بِعِبَادَتِهِمْ كَافِرِينَ

“Ni nani aliyepotea zaidi kuliko yule anayemwomba badala ya Allaah, ambao hatowaitikia mpaka siku ya Qiyaamah nao hawatambui maombi yao. Na pale watakapokusanywa watu, [waungu wao wa batili] watakuwa ni maadui wao na watakuwa wenye kuzikanusha ‘ibaadah zao.” (al-Ahqaaf 46:05-06)

Allaah amesema kuwa wale wenye kumuomba mwingine asiyekuwa Yeye ni wapotevu na akabainisha kuwa wale wenye kuombwa watakuwa ni maadui wa wale waliokuwa wakiwaomba na kwamba watakuwa ni wenye kukanusha ´ibaadah zao siku ya Qiyaamah. Amesema (Ta´ala) hali ya kuwazungumzisha wale wenye kumuomba asiyekuwa Yeye:

وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا مَا اسْتَجَابُوا لَكُمْ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ ۚ وَلَا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ

“Na wale mnaowaomba badala Yake hawamiliki japo kijiwavu cha kokwa ya tende. Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu, na hata wakisikia, hawatakuitikieni na siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikina wenu – na wala hakuna atakayekujulisha vilivyo kama Mwenye khabari ya kila kitu].” (Faatwir 35:13-14)

Hapa Allaah amebainisha yafuatayo:

1- Wale wenye kuombwa badala ya Allaah ni mafukara, kwa njia ya kwamba hawamiliki hata kijiwavu cha kokwa ya tende.

2- Amebainisha kwamba hawasikii maombi ya wale wenye kuwaomba.

3- Kukikadiriwa kuwa wanawasikia basi hawawezi kuwaitikia wale wenye kuwaomba. Hayo ni kwa sababu si waweza na ni mafakiri ambao hawawezi kuwaitikia.

4- Siku ya Qiyaamah watakanusha shirki hii ya khatari. Allaah anasema:

فَادْعُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ

“Basi muombeni Allaah hali ya kuwa ni wenye kumtakasia dini japokuwa wanachukia makafiri.” (Ghaafir 40:14)

Haijuzu kuchinja kwa ajili ya mwingine asiyekuwa Allaah ambaye amesema:

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ

”Basi swali kwa ajili ya Mola wako na [pia ukichinja] na chinja [kwa ajili Yake]!” (at-Takaathuur 108:02)

Amebainisha kwamba swalah na kichinjwa hafanyiwi mwingine asiyekuwa Allaah na kwamba mwenye kuyafanya hayo akamfanyia mwingine asiyekuwa Allaah ni shirki kubwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah amemlaani mwenye kumchinjia asiyekuwa Allaah.”[1]

Nadhiri ni ´ibaadah ambayo hatakiwi kufanyiwa mwingine isipokuwa Allaah pekee:

يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا

“Wanatimiza nadhiri na wanaiogopa siku ambayo shari yake ni yenye kuenea.” (al-Insaan 76:07)

Hivo ndivo walivyolingania Mitume watukufu wote (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam).

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ

“Hatukutuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi; hivyo basi niabuduni.” (al-Anbiyaa´ 21:25)

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

”Hakika Tulituma katika kila ummah Mtume kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na Twaaghuut [waungu batili].” (Ibraahiym 16:36)

 Hivyo basi shikamaneni na mfumo wa Mitume na wabainishieni watu maana ya shahaadah, kwamba maana yake ni kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah. Ahl-ul-Bid´ah na wanafasalfa wameifasiri kimakosa na wanasema kwamba maana yake ni kuwa hakuna muumbaji wala mwenye kuruzuku isipokuwa Allaah pekee. Tafsiri hii ni ya kimakosa na imewatumbukiza watu wengi katika shirki.

Baada ya hapo linganieni katika Tawhiyd-ul-Asmaa´ was-Swifaat na Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah na chukueni msaada kutoka katika vitabu vya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na Ibn-ul-Qayyim. Kabla ya hapo mnatakiwa kuifahamu Qur-aan na Sunnah kisawasawa na chukueni msaada kutoka katika tafsiri za Salafiyyah ya Ibn Jariyr, Ibn Kathiyr, al-Baghawiy na ya as-Sa´diy. Kuweni wenye hekima mnapolingania kwa Allaah kama alivosema:

ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ

“Lingania katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri na jadiliana nao kwa ambayo ni mazuri zaidi.” (Ibraahiym 16:125)

Baada ya haya mnatakiwa kuwabainishia watu Bid´ah za kwenye makaburi na mengineyo ambayo yanapatikana kwa watu. Wale waliokinaika na mfumo wa Mitume mtawaona ni wenye kuitikia kwa urahisi.

[1] Muslim (1978).



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2I0AIzr
via IFTTT

Mtenda madhambi ataweza kujibu maswali ya Malaika wawili?

Swali: Je, mtenda madhambi na fasiki muislamu ataweza kujibu maswali ya Malaika wawili?

Jibu: Allaah ndiye anajua zaidi. Kafiri hatoweza kujibu. Mtenda madhambi yuko khatarini katika adhabu na hali mbalimbali [za kutisha].



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2HOyjIU
via IFTTT

Mnyama akiwa na pete ya Sulaymaan na fimbo ya Muusa

Swali: Je, ni sahihi wakati  mnyama atapotoka ardhini atakuwa na pete ya Sulaymaan na fimbo ya Muusa, kama jinsi hayo yalivyotajwa na Haafidhw Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah)?

Jibu: Yamepokelewa hayo katika Hadiyth dhaifu na hayakuthibiti.



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2FL7Byu
via IFTTT

“Allaah akuhifadhi kwa jaha ya Mtume”

Swali: Ni ipi hukumu ya kusema:

“Allaah akuhifadhi kwa jaha ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)”?

Jibu: Sema:

“Allaah akuhifadhi.”

Inatosha. Allaah hana haja ya jaha ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) anakuhifadhi pasi na jaha ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ni Bid´ah. Kwa sababu kuomba kwa jaha ni jambo halikuthibiti katika Qur-aan, Sunnah wala katika maneno ya Salaf. Ni njia miongoni mwa njia za shirki. Utaanza kuomba msaada kwa jaha kidogo kidogo mpaka umuombe msaada na kumuomba yeye. Hii ni njia miongoni mwa njia za shirki. Kitendo hichi ni Bid´ah na ni njia miongoni mwa njia za shirki. Kuomba kwa jaha, haki au kwa mtu mwenyewe. Yote haya hayajuzu.



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2I284ht
via IFTTT

“Chukia ukafiri na usimchukie kafiri”

Swali: Kuna mtu leo ameandika katika gazeti la ar-Riyaadh makala ambapo amekoso silebasi za masomo na kwamba zinasema kuwa ni lazima kumchukia kafiri. Yeye anachodai ni kwamba kilicho cha lazima ni kuchukia ukafiri na sio kuwachukia makafiri. Je, maneno yake ni sahih? Vipi mtu atamjibu?

Jibu: Sisi tunachukia ukafiri na yule mwenye kusifika na ukafiri. Tunachukia yote mawili. Kusema kwamba mtu achukie ukafiri na asimchukie mtu, ni utofautishaji batili.



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2uC7DCt
via IFTTT

Jumamosi, 30 Machi 2019

Kun Salafiyya ‘alaa al-Jaadah 09



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2TLVPb4
via IFTTT

Kun Salafiyya ‘alaa al-Jaadah 08



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2U84UQg
via IFTTT

Kun Salafiyya ‘alaa al-Jaadah 07



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2FDR2TT
via IFTTT

Sharh Swariyh-us-Sunnah 38



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2U7qDIj
via IFTTT

Nafasi ya Qur’an katika kuratibu mahusiano ya kiutu

Kufupisha kumswalia Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa Mfumo wowote Haijuzu

   Kufupisha kumswalia Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa Mfumo wowote Haijuzu


Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amejibu kuhusu swali la hukmu ya kufupisha kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):


“Kama ilivyoamrishwa kumswalia Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwenye Swalaah katika Tashahhud, na imeamrishwa katika kutoa khutbah na kuomba Du’aa na kuomba maghfirah, na baada ya Adhaan, na wakati wa kuingia na kutoka Msikitini, na wakati wa kumtaja katika hali nyinginezo, hivyo basi ni muhimu zaidi kufanya hivyo katika kumtaja jina lake katika kitabu, barua, makala n.k. 

Kwa hiyo, imeamrishwa kuandika Swalaah na Salaam kwa ukamilifu ili kutimiza amri ya Allaah ('Azza wa Jalla)  Aliyotuamrisha na ili msomaji apate kukumbuka kutaja kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  anapoisoma. Hivyo tusiandike Swalaah na Salaam kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kifupi kama kuandika (S) au (S.A.W.) n.k. au mfumo wowote ambao watu wanatumia kwa sababu inakwenda kinyume na maamrisho ya Allaah na Kitabu Chake Anaposema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٥٦﴾

Enyi walioamini mswalieni na msalimieni kwa mamkizi ya amani na kwa tasliymaa.  [Al-Ahzaab 33:56]

Juu ya hivyo, ni kwamba kusudio halitimii na ni kukosa fadhila zake (za kumswalia Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na huenda msomaji asitanabahi au asifahamu (hizo herufi) maana zake zilokusudiwa. Na juu ya hivyo pia kufupisha kwa herufi zimechukizwa na Ahlul-‘Ilm na wametahadharisha hivyo.”

[Majmuw’ Al-Fataawaa Wa Rasaail  Al-Imaam Ibn Baaz (2/397 – 399)]



https://ift.tt/2uJHNNb i live islam

Hukmu ya kuishi na Mke asiyeswali

SWALI

Ni ipi hukmu ya mke asiyeswali, kwa kutambua kuwa nimeshambainishia adhabu anayopata mwenye kuacha kuswali, kuna baadhi ya nyakati anaswali na wakati mwengine anaacha. Kwa mfano anaswali Adhuhuri na anaacha (Swalaah) zote za Faradhi zilizobaki?


JIBU

Hukmu yake ni Kafiri.

Na haijuzu kuendelea kubaki naye katika hifadhi yako. Inapasa kuwa naye mbali, isipokuwa kama atatubu tawbah ya kweli, la sivyo, ni waajib kuwa naye mbali (kuachana naye).

Kwa sababu kuacha Swalaah ni ukafiri mkubwa.

Anasema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Baina ya mtu na baina ya ushirikina na ukafiri ni kuacha Swalaah.” [Muslim]

Na anasema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Agano (Kinachotutofautisha) baina yetu (Waumini) na baina yao (Washirikina, Makafiri na Wanafiki) ni Swalaah, anayeiacha (Swalaah) amekufuru.” [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah na An-Nasaaiy]

Hii ndio kauli sahihi katika kauli za Wanachuoni; kwamba kuiacha (Swalaah) ni ukafiri mkubwa.

Na  Allaah  anajua  zaidi


https://ift.tt/2I12ThB i live islam

Maana ya Duaa ya ufunguzi wa Swalaah

                          Maana ya Duaa Ya ufunguzi wa Swalaah  "Wa Ta’ala Jadduka"



SWALI

Nini maana ya kauli yetu katika du’aa ya ufunguzi wa Swalaah:


  وَتَعـالى جَـدُّكَ  
Wwa Ta’ala Jadduka  
Na Umetukuka Ujalali Wako


JIBU
  
Maana yake ni:  Ukubwa, Uadhama, Ujalali kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) katika Suwratul Jinn kuhusu majini:
وَأَنَّهُ تَعَالَىٰ جَدُّ رَبِّنَا مَا اتَّخَذَ صَاحِبَةً وَلَا وَلَدًا﴿٣﴾
 “Na kwamba hakika umetukuka kabisa Ujalali wa Rabb wetu, Hakujifanyia mke wala mwana.” [Al-Jinn: 3]
  
[Majmuw’ Al-Fataawaa 11/74]


Du’aa hiyo ya ufunguzi wa Swalaah kikamilifu ni:

سُبْـحانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمْـدِكَ وَتَبارَكَ اسْمُـكَ وَتَعـالى جَـدُّكَ وَلا إِلهَ غَيْرُك
Subhaanaka-LLaahumma wabihamdika watabaarakas-Smuka wa Ta’aalaaa Jadduka walaa ilaaha Ghayruka
Utakasifu ni Wako Ee Allaah, na Himdi ni Zako, na Limebarikika Jina Lako, na Umetukuka Ujalali Wako, na hapana muabudiwa wa haki, ghairi Yako


Na  Allaah  anajua  zaidi


https://ift.tt/2OAQEti i live islam

Kuzishikilia Sunnah kwa Magego

                                             Kuzishikilia Sunnah kwa Magego 




عن أبي نَجِيح الْعِرْبَاضُ  بن سارية (رضي الله عنه) قال: وَعَظَنَا رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه و آله وسلم) مَوْعِظَةً بَلِيغَةً وَجِلَتْ مِنْهَا الْقُلُوبُ  وَذَرَفَتْ مِنْهَا الْعُيُونُ. فَقُلْنَا:  يَا رَسُولَ اللَّهِ كَأَنَّها مَوْعِظَةُ مُوَدِّعٍ فأوْصِنا. فَقَالَ: ((أُوصِيكُمْ بِتَقْوَى اللَّهِ وَالسَّمْعِ وَالطَّاعَةِ وَإِنْ تأَمَّرَ عَلَيْكُم عَبْدٌ حَبَشِيّ ، وَأَنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيَرَى اخْتِلاَفًا كَثِيرًا ، فَعَلَيْكُمْ بِسُنَّتِي وَسُنَّةِ الْخُلَفَاءِ الرَّاشِدِينَ الْمَهْدِيِّينَ ، عَضُّوا عَلَيْهَا بِالنَّوَاجِذِ وَإِيَّاكُمْ وَمُحْدَثَاتِ الأُمُورِ فَإِنَّ كُلَّ بِدْعَةٌ ضَلاَلَةٌ)) رواه أبو داوود والترمذي وقال حديث حسن صحيح

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Najiyh Al-‘Irbaadhw bin Saariyah (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitupa mawaidha mazito (yenye maana kubwa), nyoyo zikaogopa na macho yakabubujikwa machozi. Tukasema: Ee Rasuli wa Allaah! Yanaonekana kama kwamba mawaidha ya kutuaga, basi tuusie.  Akasema: ((Nakuusieni kuwa na taqwa ya Allaah na kusikiliza na kutii japokuwa mtaongozwa na mtumwa Mhabashi. Hakika atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu ataona ikhtilaaf nyingi. Kwa hiyo, shikamaneni na Sunnah zangu na mwenendo wa Makhalifa waongofu, yashikilieni kwa magego [mambo yao]. Na tahadharini na mambo yenye kuzushwa, kwani kila uzushi ni upotovu)) [Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth Hasan Swahiyh].


                                                       Mafunzo ya  Hadiythi


1.Wajibu wa kumcha Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kufuata maamrisho na makatazo Yake kama Anavyosema:

قُلْ أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْهِ مَا حُمِّلَ وَعَلَيْكُم مَّا حُمِّلْتُمْ ۖ وَإِن تُطِيعُوهُ تَهْتَدُوا ۚ وَمَا عَلَى الرَّسُولِ إِلَّا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ ﴿٥٤﴾
Sema: “Mtiini Allaah na mtiini Rasuli.” Mkigeukilia mbali, basi hakika jukumu lake ni lile alobebeshwa tu nanyi ni juu yenu yale mliyobebeshwa. Na mkimtii mtaongoka; na hapana juu ya Rasuli isipokuwa ubalighisho bayana.


وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا ۚ وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿٥٥﴾
Allaah Amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema kwamba bila shaka Atawafanya makhalifa katika ardhi kama Alivyowafanya makhalifa wale waliokuwa kabla yao, na bila shaka Atawamakinishia Dini yao Aliyowaridhia, na bila shaka Atawabadilishia amani badala ya khofu yao; wawe wananiabudu Mimi wasinishirikishe na chochote; na yeyote yule atakayekufuru baada ya hapo, basi hao ndio mafasiki.

وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٥٦﴾
Na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah, na mtiini Rasuli ili mpate kurehemewa. [An-Nuwr 24: 54-56)]


Rejea pia:  Al-Anfaal (8: 46), Al-Ahzaab (33: 70), At-Tawbah (9: 119), Muhammad (47: 33).

Na jambo hilo limepatiwa kipaumbele kwa kutajwa mwanzo kwa kuwa umuhimu wake ni mkubwa sana.


2. Wajibu wa kumtii kiongozi anayeongoza kwa kufuata Shariy’ah japokuwa ni mtu anayeonekana kuwa duni, na inapotokea ikhtilaaf, arudie mtu katika Qur-aan na Sunnah.


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا ﴿٥٩﴾
Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri zaidi. [An-Nisaa (4: 59)]


3. Hadiyth hii ni miongoni mwa miujiza ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kubashiria yatakayotokea, kwani zimeshadhihirika ikhtilaaf nyingi baina ya Waislamu.


4. Kufuata amri za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni dalili ya mapenzi ya Allaah (سبحانه وتعالى) na tahadharisho la kumkhalifu. Rejea: Aal-‘Imraan (3: 31), An-Nuwr (24: 63).


5. Umuhimu wa kufuata Sunnah za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kuzishikilia bila ya kutoka nje ya mipaka na njia iliyonyooka ikapeleka kufarikiana Waislamu na kujitokeza makundi makundi. Rejea: Al-An’aam (6: 153).

Na kila kundi hufurahia watu wake wakijiona kuwa wako katika haki. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
مِنَ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا ۖ كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ ﴿٣٢﴾
 (Wala msiwe) Miongoni mwa wale walioitenganisha dini yaowakawa makundi makundi. Kila kundi wananafurahia waliyonayo.  [Ar-Ruwm (30: 32)]



6. Kufuata Sunnah za Makhalifa Waongofu na kuamini kauli ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Sunnah zao khaswa pale inapokuwa ni jambo walilolitenda wao bila ya kutendwa na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).


7.  Kujiepusha kabisa na bid’ah (Uzushi), kwani hatari yake ni upotofu na motoni. [Hadiyth((Na kila upotofu unapeleka motoni))[Muslim]


8. Vitendo vya bid’ah havina thamani wala havitapokelewa.

Rejea Hadiyth namba (15).


8. Kuonyesha usawa ulioletwa na Uislamu baina ya waja bila kujali tofauti ya ukoo, kabila, utaifa na mwengineo. Ndio tukaamrishwa kumfuata kiongozi mchaji Allaah hata kama ni mtumwa.

Rejea: Al-Hujuraat (49: 13)


9. Utiifu kwa Amiri ni wajibu, maadamu hajakuamrisha jambo la kumuasi Allaah (سبحانه وتعالى) na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم).


10. Fadhila za Maswahaba wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) waliopata hadhi ya kuwa Makhalifa baada ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).


https://ift.tt/2FKLkkD i live islam

Iga dini yako kwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum)



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2HOFfpg
via IFTTT

Mwezi mtukufu wa Rajab na yaliyozuliwa ndani yake



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2JUycgK
via IFTTT

Mafunzo katika tukio la New Zealand



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2uD1AOe
via IFTTT

Ni nani anayestahiki kuwa imamu katika hali hii?

Swali: Mtu akiingia baada ya kuwa ameshapitwa na swalah ya Maghrib ambapo akasimama mtu na kutaka kumpa swadaqah. Ni yupi ana haki zaidi ya kuswali na mwingine? Je, kuna ubaya wa kuirudi swalah ya Maghrib ambayo ni Witr ya mchana?

Jibu: Akiingia mtu msikitini na akataka mtu mwingine kumtolea swadaqah, yule mwenye kuonelea kuwa ambaye anaswali swalah ya Sunnah hasihi kuwa imamu wa anayeswali swalah ya faradhi basi itatakikana kwa yule aliyeingia ndiye awe imamu. Kwa sababu mtu huyu anaswali faradhi na huyu wa pili anaswali Sunnah. Upande mwingine yule mwenye kuonelea kuwa inafaa kwa ambaye anaswali swalah ya Sunnah kuwa imamu wa anayeswali swalah ya faradhi – na haya ndio maoni sahihi – wamesema kuwa ataongoza swalah yule ambaye ni msomi zaidi wa Qur-aan. Ni mamoja yule aliyeingia au yule ambaye tayari yuko msikitini.

Kuhusu swali lake juu ya swalah ya Maghrib kwamba irudiwe au isirudiwe, tunaona kuwa irudiwe. Itakuwa Witr kabisa kama swalah ya imamu. Haipingani ile swalah ya kwanza aliyoswali na imamu wa kwanza ndio ikawa Witr ya mchana na hii ya pili ikawa ni marudilio. Hakuna ubaya wake akairudi mara tatu kwa sababu ameirudi akimfuata imamu wake.



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2ODHCfq
via IFTTT

Mwanamke kuvaa suruwali ni kujifananisha na wanaume

Swali: Ni ipi hukumu kwa mwanamke kuvaa suruwali?

Jibu: Haitakikani kwa mwanamke kuvaa suruwali. Huku ni kujifananisha na wanaume.



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2FL0GW1
via IFTTT

ar-Raajihiy kuhusu pete ya uchumba au ya ndoa

Swali: Ni ipi hukumu mwanaume kumvisha mchumba wake pete ya ndoa au ad-Dublah? Nimesikia kwamba jambo hilo ni kujifananisa na manaswara[1].

Jibu: Ikiwa ni kujifananisha basi ni haramu na wala haifai. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kujifananisha watu basi yeye ni katika wao.”

Kadhalika ikiwa ni katikati ya wanawake basi kitendo hichi ni uchache wa haya kwa kule kukaa kwake mbele ya wanawake. Ama akiionyesha mbele ya wanaume ndio kitendo hichi ndio khatari zaidi. Haifai ikiwa ni kujifananisha. Pia ni haramu kutokana na ule uchache wa haya ulio ndani yake.

[1] Tazama http://firqatunnajia.com/46-maovu-ya-sita-pete-ya-uchumba/



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2UnFrSg
via IFTTT

Sote ni wenye mapungufu

Swali: Ni miongoni mwa wale watu ambao wanawaficha watu ukhalifu wao na wala simfichi Allaah, wale wanaowaamrisha watu mema ilihali wao wenyewe hawayafanyi, wanakataza maovu ilihali wao wenyewe wanayafanya, sisimami usiku kuswali na wala sisomi Qur-aan. Nina miaka ishirini na sita. Sijawahi kukhitimisha Qur-aan isipokuwa takriban mara tano tu. Nataraji kutoka kwa Allaah kisha kwako uniawaidhi na unipe nasaha. Huenda Allaah akaninufaisha mimi na wale waliohudhuria kwazo.

Jibu: Hapana shaka kwamba sote ni wenye mapungufu. Lakini mambo haya ni baina yako wewe na Allaah. Tubu kwa Allaah baina yako wewe na Allaah. Usiwatajie mambo haya watu. Mambo haya ni baina yako wewe na Allaah. Tubu kwa Allaah, pupia kumtii Allaah na Allaah atakusaidia.



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2HKYDDC
via IFTTT

Kuwasaidia makafiri kumg´oa mtawala wa Kiislamu aliyekufuru

Makafiri watamg´oa na wamweke badala yake mwenzao. Mkiwasaidia watamg´oa kweli na wamweke mwezao. Faida iko wapi? Zingatieni! Waislamu wakiwa na nguvu na kumg´oa kiongozi kafiri, watamg´oa. Ama wakiwa hawana nguvu basi wanatakiwa kufanya subira na wasiziweke nafsi zao katika maangamivu na khatari. Ama kusema wawasaidie makafiri kumg´oa hapana. Makafiri wanafurahishwa na hili na wanamweka badala yake mwenzao. Katika hali hiyo sisi tutakuwa tumemwondosha kafiri na tumemlata kafiri mwingine.



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2WxRWrR
via IFTTT

Ijumaa, 29 Machi 2019

Sharh Swariyh-us-Sunnah 37



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2U97jKD
via IFTTT

Sharh Swariyh-us-Sunnah 36



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2CIIavK
via IFTTT

Sharh Swariyh-us-Sunnah 35



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2HPC6pb
via IFTTT

Sharh Swariyh-us-Sunnah 34



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2WAvmip
via IFTTT

Sharh Swariyh-us-Sunnah 33



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2HKZ8Oh
via IFTTT

Usidharau katika wema jambo lolote hata bashasha kwa ndugu yako

Siku moja Hudhaifa (Allah amridhie) alimsikia Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) akisema: “Hakika mtu mmoja miongoni mwa wale waliokuwapo kabla yenu (katika umati zilizopita) alijiwa na Malaika kwa ajili ya kuchukua roho yake, akasema, ‘Je, kuna kheri yoyote umeifanya?’ Akasema, ‘Sijui.’ Malaika akamuambia, ‘Tazama,’ akasema, ‘Sijui kitu chochote (nilichokifanya) isipokuwa duniani nilikuwa nikiwauzia watu vitu, nikimpa tajiri muda wa ziada kulipa deni na ninamsamehe maskini. Allah akamuingiza peponi,” [Bukhari].

Mafunzo ya tukio hili

Watu wataingia peponi kwa fadhila za Allah
Muislamu hatakiwi kudanganyika na wingi wa matendo anayoyafanya kwa kuona kuwa amali anazozifanya zinatosha kumuingiza peponi. Watu wataingia peponi kwa fadhila za Allah Mtukufu kupitia njia zake, yaani sababu zinazopelekea kupata fadhila za Allah. Yapo mambo lukuki ambayo Mwenyezi Mungu ametuamuru kuyafanya ili tuvune thawabu nyingi na hatimaye atuingize peponi kwa huruma yake na fadhila zake.

Kukithirisha matendo mema
Tukio hili linatupa hamasa ya kukithirisha kufanya mambo mema hasa ikizingatiwa kuwa Muislamu hajui ni aina gani ya ibada ambayo akiifanya itapelekea kupata fadhila za Allah na hatimaye kuingia peponi.

Katika tukio hili, tumeshuhudia mmoja wa waja wa Allah akiwapa watu muda wa kutosha wa kulipa madeni na kuwasamehe watu masikini na wale walioshindwa kuyalipa. Jambo hili lilimpendeza mno Allah hadi akamuingiza mja wake huyo peponi.

Na hayo ndiyo makusudio na shabaha ya Sharia ya Kiislamu, ambayo licha ya kuwahimiza watu kusaidiana pia inazingatia hali na mazingira yao na si kung’ang’ania makubaliano pekee. Mwenyezi Mungu anasema “Na akiwa [mdaiwa] ana shida, basi [mdai] angoje mpaka atakapojiweza. Na mkilifanya deni kuwa ni sadaka, basi ni bora kwenu, ikiwa mnajua.” [Qur’an, 2:280].

Kuwa na nyoyo za huruma
Duniani kuna watu wapole wenye imani, na ambao Allah amewapa ukarimu wa kuwasaidia wanyonge, maskini na wenye uhitaji. Kupitia kwao watu wengi wanajikwamua na hali ngumu ya maisha. Allah Mtukufu anawapenda watu wa aina hii kutokana na kujitolea kwao katika kuwanufaisha waja wake.

Katika kulibainisha hilo, Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) amesema: “Mtu anayependwa zaidi kwa Allah Mtukufu ni yule mwenye kuwanufaisha watu, na matendo yanayopendeza sana kwa Allah ni furaha unayoiingiza kwa Muislamu au kumuondoshea tatizo, au kumlipia deni,” [Twabraniy].

Kuwa mwema au muovu
Katika maisha yake hapa ulimwenguni, mwanadamu hufanya mambo mema yatakayobaki katika kumbukumbu nzuri hata baada ya kufa. Kwa upande mwingine, mwanadamu hufanya mambo maovu ambayo baada ya kufa yataacha kumbukumbu mbaya kwa walimwengu.

Katika tukio hili tunaona namna mja huyu wa Allah alivyofanya matendo mema yenye kuwanufaisha watu hadi Allah akamfanya kielelezo cha watu wema na matendo yake kubaki katika kumbukumbu nzuri hata baada ya kufa kwake. Kadri mali yake ilipoongezeka ndivyo alivyomshukuru Mola wake kwa kauli na matendo.

Kutokana na wingi wa mali yake watu walikuwa wakimuendea na kumueleza shida zao, akawa anawakopesha na ulipofika muda wa kulipa madeni alikuwa akitazama hali ya wale anaowadai, akiwapa watu muda wa ziada kulipa madeni yao na kuwasamehe wanyonge, maskini na walioshindwa kulipa.

Huruma ya Allah
Tukio hili pia linatupa mwangaza juu ya huruma ya Allah juu ya waja wake. Pamoja na mja wake huyu kufanya amali njema chache, Allah alimruzuku pepo kutokana na tabia yake ya kuwahurumia watu.

Ni jambo jema mtu kufanya kheri kwa ajili ya manufaa binafsi na ya jamii nzima. Mfano wa kheri hizo ni kama vile kutoa sadaka, kuwalingania watu, kulea yatima, kusaidia maskini na mafukara na kutoa ufadhili wa masomo.

Fadhila za kusaidia watu
Zimethibiti fadhila nyingi ndani ya Qur’an Tukufu na Sunna (Hadithi) za Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) kwa mtu mwenye kuwasaidia watu pindi wanapokabiliwa na shida na matatizo mbalimbali. Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) amesema: “Yeyote atakayemfanyia wepesi mtu aliyepatwa na uzito (shida) Allah atamfanyia wepesi duniani na Akhera.” [Muslim].

Na katika riwaya ya Imam Ahmad, Mtume amesema: “Atakayemuondoshea yule anayemdai, au kumuondoshea kabisa deni lake, basi Siku ya Kiyama atakuwa chini ya kivuli cha arshi.” Hizi ni fadhila kubwa ambazo aghalabu watu wengi huzikosa kutokana na nyoyo zao kuegemea zaidi matamanio ya kidunia na kusahau njia za kheri zenye kujenga upendo katika maisha ya kijamii.



from TIF https://ift.tt/2FM0E0m
via IFTTT

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...