Translate

Jumatatu, 31 Desemba 2018

Neno kutoka kwa Mwenyekiti


Mtume Muhammad (ص) amesema: “wepesisheni kwa watu (kuhusu mambo ya Dini) na wala msiwafanyie uzito na wala msiwakimbize’’


(Bukhari na Muslim)

Sisi kuwekeza katika jamii yetu kwa ajili ya mwangaza wa baadaye kama Waislamu, tunahisi ni wajibu wetu kuleta mabadiliko kwa njia ambazo zimewekwa na za kumridhisha Allah (S.W) ili kuwasaidia wengine katika nyakati tofauti. Roho hii ya wasiwasi juu ya ustawi wa waislamu na watanzania kwa ujumla katika jamii inayotuzunguka ndio imesababisha sisi kuanzisha The Islamic Foundation hapa nchini Tanzania.

“TUMEAHIDI, TUMETIMIZA NA ALLAH NI SHAHIDI”







from TIF http://bit.ly/2QeXhAI
via IFTTT

Kuzidisha kheri

Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh


Baada ya Allaah Kufaradhisha kufunga Ramadhaan, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawashaji´isha kuifuatisha Ramadhaan kwa kufunga siku zile za Shawwaal.

Amefanya hivi ili ujira wao uweze kuwa mkubwa na ili waweze kulipwa kama aliyefunga mwaka mzima. Abu Ayyuub al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anhu) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anayefunga Ramadhaan na akaifuatisha kwa kufunga siku sita za Shawwaal, ni kama amefunga mwaka mzima.” Haafidhw al-Mundhiriy amesema: “Ameipokea Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa´iy, Ibn Maajah na at-Twabaraaniy amezidisha na kusema:

“Nilisema: “Kila siku hulipwa kwa kumi.” Akasema: “Ndio.” Wamepokezi wake ni wapokezi sahihi.


Mwaka hauwezi kuzidi siku 360. Siku sita za Shawwaal zikiwekwa katika Ramadhaan nzima na kila siku moja inalipwa kwa thawabu kumi (kwa kuwa tendo moja zuri linalipwa mara kumi) Waislamu wanazingatiwa kuwa wamefunga mwaka mzima. Kwa ajili hiyo amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Ni kama amefunga mwaka mzima.” Hiyo ni fadhila kutoka kwa Allaah. Himdi na shukurani zote ni za Allaah zisizohesabika.


Kutoka kheri kwenda nyingine 


Katika fadhila za Allaah kwa waja Wake ni kwamba Amewasahilishia njia ambazo zinawanyanyua katika daraja.

Vile vile Amewajaalia daima mafungamano yenye nguvu na ´ibaadah za Allaah. Baada ya masiku na usiku za Ramadhaan (ambapo ndani yake Allaah Anayasamehe madhambi, Anazinyanyua daraja na kuyafuta makosa) kuisha, viumbe wanakuwa wamemkurubia Mola Wao.

Baada ya hapo kidogo huanza miezi ya Hajj, ambapo ndani yake inaendewa Nyumba Tukufu ya Allaah. Siku ya ´Iyd-ulFitwr, ambayo ni ile siku ya kwanza ya Shawwaal, ndio siku ya kwanza ya miezi ya Hajj.

Allaah (Ta´ala) Amesema juu yake:

 ٌت ا َ لُوم ْ َّمع ٌ ر ُ ْشه ج أَ ُّ َ ۚ ا ْْل ج ِّ َ اَل ِِف ا ْْل َ د ََّل جِ َ وَق و ُ ُس ََّل ف َ َ َث و ف َ ََل ر ج ف َّ َ ن ا ْْل َّ ِه ي ِ َ َض ف َر ن ف َ َم ۚ لُوا ف َ ْع َف ا ت َ م َ و ُ ه َّ الل ُ ه ْ لَم ْ ع َ ي ٍ ْ َْي ْ خ ن ۚ ى ِ م َ ْو َّ ق الت ِ زاد الَّ َ ر ْ ي َ ن خ َّ ِ إ َ وا ف ُ ود َّ َ َز ت َ ۚ و َ ا أُوِِل اْْلَلْب َ ي ُونِ َّ ق ات َ ِب و ا

“Hajj ni miezi maalumu. Na atakayekusudia kuhiji, basi asifanye tendo la ndoa wala ufasiki wala mabishano katika Hajj. Na lolote mlifanyalo katika ya kheri Allaah Analijua. Na jitengenezeeni akiba. Na hakika bora ya akiba ni taqwa. Na nicheni Mimi enyi wenye akili!” 02:197


Katika Ramadhaan ndio kumeteremshwa Qur-aan iliyobarikiwa. Katika Ramadhaan milango ya Pepo inafunguliwa na milango ya Moto inafungwa.


Katika siku za Swawm Mashaytwaan wanafungwa. Allaah (Ta´ala) Amesema kuhusu siku hizi katika Hadiyth al-Qudsiy: “Kila ´amali ya mwanaadamu inalipwa mara kumi. Isipokuwa Swawm tu. Ni Yangu na Mimi ndio nitailipa.” Wakati masiku haya hayanaisha, kunakuja masiku ya Hajj. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu masiku haya:

“Atakayefanya Hajj, kisha asiseme maneno machafu wala asitende vitendo vichafu, atarudi akiwa kama siku aliyozaliwa na mama yake.” Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim na wengine.

Amesema pia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “'Umrah hadi 'Umrah ni kafara [kufutiwa dhambi] baina yao, wakati Hajj iliyokubaliwa haina jazaa isipokuwa ni Pepo.” Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim na wengine.

Muislamu hakaribii kukamilisha mmoja katika misimu ya Aakhirah, isipokuwa unakuja mwingine mpya. Hili linaendelea ili awe kila siku ni mwenye kumwabudu Mola Wake Aliyemuumba baada ya kukosekana na Akamjazia neema Zake za dhahiri na zilizojificha.


Na  Allaah  anajua  zaidi

from fisabilillaah.com http://bit.ly/2Vi6tbD
via IFTTT

Msimu katika misimu ya Aakhirah

Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh


Kama jinsi Allaah Amevyofadhilisha baadhi ya watu juu ya wengine na baadhi ya sehemu juu ya zingine, kadhalika Amefadhilisha baadhi ya zama kuliko zingine.

Miongoni mwa hayo Amefadhilisha mwezi wa Ramadhaan uliobarikiwa kuliko miezi mingine. Ameutofautisha na miezi mingine na Kuuchagua kuwa ni mwezi wa wajibu kwa watu kufunga:

 ُ ار َ ت ََيْ َ و ُ َ َشاء ا ي َ م ُ لُق َك ََيْ ُّ ب َ ر َ و

“Na Mola wako Anaumba Atakavyo, na Anachagua (Atakavyo).”28:68


Allaah Ameufadhilisha mwezi huu na Kuufanya kuwa ni msimu bora.

Humo wanashindishana waja katika kumwabu Allaah ili waweze kufikia mafanikio na kujikurubisha kwa Allaah.

Wanajikurubisha kwa Mola Wao kwa kufunga mchana na kusimama usiku na kusoma Kitabu Chake Kitukufu ambacho haitokifikia ubatili mbele yake na wala nyuma yake; ni uteremsho kutoka kwa Mwenye hikmah wa yote daima na Mwenye kustahiki kuhimidiwa. Wanajikurubisha kwa Allaah kupitia hicho na utiifu mwingine wote.

Lakini wakati huo huo wanapofanya hayo, wanajitenga na kujiweka mbali na maasi na madhambi:

 َ ور ُ ب َ ن ت َّ ل ا ة َ ار َ وَن ِتِ ُ ْج ر َ ي ِ ه ِ َ ْضل ِّمن ف م ُ َه ِزيد َ ي َ و ْ م ُ ه َ ور ُ أُج ْ م ُ ه َ ِّ ي ف َ و ُ ي ِ ۚ ل ٌ ٌ َش ُكور ُور َغف ُ ه َّ ن ِ إ

“Wanataraji tijara isiyofilisika. Ili (Allaah) Awalipe ujira wao timilifu na Awazidishie kutokana na fadhila Zake. Hakika Yeye ni Ghafuwrun-Shakuwr (Mwingi wa kusamehe - Mwingi wa kupokea shukurani).”35:29-30



Na  Allaah anajua  zaidi





from fisabilillaah.com http://bit.ly/2s2wTjX
via IFTTT

Dunia ni nyumba ya majaribio na mtihani

Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh


Allaah Ameumba viumbe Wake ili wamwabudu Yeye Mmoja asiyekuwa na mshirika.

Amesema katika Kitabu Chake Titukufu:

 ُونِ د ُ ب ْ ع َ ي ِ َّل ل َِّ إ َ نس اْْلِ َ ن و َّ ُت ا ْْلِ ْ لَق َ ا خ َ م َ و

“Na Sikuumba majini na wanadamu wa isipokuwa waniabudu.”51:56

 Ametuma Mitume Wake watukufu ili wawaoneshe waja njia ya ´ibaadah:

 َ و َ ه َّ ُوا الل د ُ ب ْ اع واَّل أَنِ ُ رس َّ ٍ َّمة ا ِِف ُك ِّل أُ َ ن ْ ث َ ع َ َ ْد ب لَق َ َت و اغُو َّ وا الط ُ ب ِ ن َ ت ْ اج

“Na kwa yakini Tulituma katika kila ummah Rasuli (awaamrishe watu wake) kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na twaaghuwt (miungu ya uongo).”16:36

Amefanya maisha ya dunia kuwa ni sehemu ya majaribio yao na mtihani ili waoneshe ni nani katika wao alie na matendo mazuri:

 ال َ َم ع ُ ن َ ْس أَح ْ ُّ ُكم أَي ْ ُكم َ لُو ْ ب َ ي ِ ل َ اة َ ي َ ا ْْل َ ْ َت و و َ الْم َ لَق َ ي خ ذِ َّ ال

“Ambaye Ameumba mauti na uhai ili Akujaribuni ni nani kati yenu mwenye ‘amali nzuri zaidi.”67:02

Kisha Akasema:

 ُو َف الْغ ُ ِزيز َ الْع َ و ُ ه َ و ُ ر

“Naye ni Al- ‘Aziyzul-Ghafuwr (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwingi wa kusamehe).”67:02


Amesema hivi ili kuonesha kuwa Anawalipa hawa wanaopewa mtihani wanaotenda matendo mema. Malipo haya yametokamana na Jina Lake alGhafuur (Mwingi wa kusamehe).

Upande mwingine Ameonesha pia kuwa wale wasiotenda matendo mazuri wanastahiki kuadhibiwa kutokana na Jina Lake al-´Aziyz (Mwenye enzi ya nguvu asiyeshindika daima). Hili linaenda sambamba na Kauli Yake:

 ُ يم ِ ُب اْْلَل َذا َ الْع َ و ُ َذاِِب ه َ ن ع أَ َّ َ و

“Na kwamba Adhabu Yangu, ndiyo adhabu iumizayo.”15:50


Kwahiyo Ndugu zangu katika Imaani, Tumche Allaah na Tufanye Mema

from fisabilillaah.com http://bit.ly/2SzcPla
via IFTTT

Duaa Sahihi ya Tashahhud

Du'aa za Qunut ni Lazima zisomwe katika Swalah ya Alfajiri?

Kuomba Dua pamoja baada ya Swalah ya Fardh

SWALI

assalam alaykum warahmatullah wabaraqatuh,
katika misikiti mingi tunasoma dua kwa pamoja (imam au mtu mwengine anasoma na wengine tunaitikia) jee hii ni sunna,faradhi au bidaa na kama haifai tuombe vipi baada ya swala.


JIBU

Wa Aleykum  Sallaam  WarahmatulLaah  Wabarakatuh

Naam kwanza kabisa Du'aa ni ‘ibaadah kama alivyosema Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 عن النعمان بن بشير رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم (( الدعاء هو العبادة (( ثم قرأ: ((وَقَالَ  رَبُّكُمُ  ادْعُونِي  أَسْتَجِبْ  لَكُمْ  إِنَّ  الَّذِينَ  يَسْتَكْبِرُونَ  عَنْ  عِبَادَتِي  سَيَدْخُلُونَ  جَهَنَّمَ  دَاخِرِينَ)) رواه الترمذي

Imetoka kwa An-Nu'maan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Du'aa ni ‘ibaadah)) Kisha Akasoma: ((Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni. Hakika wale wanaotakabari na kuniabudu wataingika Jahanam wadhalilike))[Ghaafir:60] [At-Tirmidhiy, na Shaykh Al-Albaaniy kasema kuwa ni Hasan Swahiyh katika Sunan At-Tirmidhiy]

Kwa hivyo inatupasa tuombe kwa kufuata njia iliyo sahihi kama tulivyopata mafunzo kutoka Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

Haikuthibitika kutoka kwa Maswahaba zake kuwa alikuwa akisoma Du'aa pamoja kwa sauti na wao wakiitikia baada ya Swalaah au hata nje ya Swalaah. 

Kwa hiyo kufanya hivyo itakuwa ni bid'ah (uzushi), jambo ambalo linampasa Muislamu ajiepushe nalo ili abakie katika mafunzo Sahihi.


Itambulike kwamba kutenda ‘amali ambayo haimo katika mafunzo sahihi ya Dini yetu itakuwa ni amali isiyo  na thamani yoyote kwa dalili ya kauli ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((من أحدث في أمرنا هذا ما ليس منه فهو رد))  متفق  عليه .
((Yeyote atakayezusha katika mambo yetu haya (ya Dini) ambayo hayamo kwetu basi hakitapokelewa)) [Al-Bukhaariy na Muslim]  

Kuomba Du'aa katika Swalaah au baada ya Swalaah tumeamrishwa katika Qur-aan na Sunnah, lakini kila mtu anatakiwa aombe pekee na sio kwa ujumla kwani hahitaji mtu kuwasiliana na Allaah (‘Azza wa Jalla) kumuomba jambo lake kupitia kwa mtu yeyote, kwa sababu Yeye  Anaitikia maombi ya muombaj na  Yuko karibu na sisi kama Anavyosema:

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ ﴿١٨٦﴾
186. Na watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi); Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka.  [Al-Baqarah:186] 


Vile vile Mtume Muhammad(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kwamba Du'aa huombwa wakati mtu anaposujudu, kama ifuatavyo:

عن ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ : قالرَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ( أَلا وَإِنِّي نُهِيتُ أَنْ أَقْرَأَ الْقُرْآنَ رَاكِعًا أَوْ سَاجِدًا ، فَأَمَّا الرُّكُوعُ فَعَظِّمُوا فِيهِ الرَّبَّ عَزَّ وَجَلَّ ، وَأَمَّا السُّجُودُ فَاجْتَهِدُوا فِي الدُّعَاءِ فَقَمِنٌ – أي جدير وحقيق - أَنْ يُسْتَجَابَ لَكُمْ   .  مسلم
Imetoka kwa ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika mimi nimekatazwa kusoma Qur-aan katika kurukuu au kusujudu. Ama katika kurukuu mtukuzeni Rabb Mwenye Utukufu na Ujalali. Na Ama katika kusujudu jitahidini katika Du'aa kwani ni yakini kuwa Atakutakabalieni)) [Muslim]

Na aliposema tuombe du'aa katika kila baada ya Swalaah ni kuomba kila mtu pekee yake na bila ya kuinua mikono.

Pia baadhi ya ‘Ulamaa wameona kwamba ni baada ya tashahhud na kabla ya kutoa salaam.


Kunyanyuka mikono katika du’aa inakubalika katika hali fulani ya kuomba du’aa kama vile katika Swalaah ya Istisqaa (Swalaah ya kuomba mvua), pia sehemu  kama Swafaa na Marwah, ‘Arafah, Muzdalifah, Jamaraat (baada ya  kurusha vijiwe kwenye nguzo) n.k.  


Na Hadiyth ifuatayo inathibitisha kunyanyua mikono katika du’aa:

عن سَلْمَانَ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ( إِنَّ رَبَّكُمْ تَبَارَكَ وَتَعَالَى حَيِيٌّ كَرِيمٌ يَسْتَحْيِي مِنْ عَبْدِهِ إِذَا رَفَعَ يَدَيْهِ إِلَيْهِ أَنْ يَرُدَّهُمَا صِفْرًا  ((  أبي داود"، وصححه الشيخالألباني   
Kutoka kwa Radhwiys ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Rabb wenu Tabaaraka wa Ta’aalaa Yuhai na Mkarimu Anasitahi kwa mja Wake anapoinua mikono yake (kumuomba) Airudishe sifuri)) (bila ya kumjibu) [Abuu Daawuwd na ameipa daraja ya Swahiyh Shaykh Al-Albaani ]  


‘Ulamaa wameona kwamba pale panapo dalili kwamba inaruhusiwa kunyanyua mikono katika kuomba du’aa basi hakuna kosa.


Na hivyo katika shida zake mtu anazotaka kumuomba Rabb wake, anaweza kunyanyua mikono kutokana na Hadiyth iliyotangulia kutajwa juu.

Kisha vile kutokana na Hadiyth iliyopokelewa na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu):


((Mtu aliyekwenda safarini akachoka na kujaa vumbi, kisha akanyanyua mikono juu na kuomba "Ee Rabb, Ee Rabb” lakini chakula chake ni haramu, kinywaji chake ni haramu na mavazi yake ni haramu, amerutubishwa kwa haramu, vipi atatakabliwa?)) [Muslim]


Hadiyth hii inaonyesha kwamba mtu huyo alikuwa akiomba kwa Allaah ('Azza wa Jalla) shida zake na huku amenyanyua mikono.


Na  Allaah  anajua  zaidi


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2BQakDS
via IFTTT

Inafaa kumuombea Dua Mzazi ambaye si Muislamu?

SWALI:

Je mtoto aweza kumuombea dua gani mzazi wake hali ya kuwa huyo mzazi si muislaam?

JIBU: 

Ikiwa  mzazi  huyo  yuko  haai  unaweza  ukamuombea  Du'aa  ili  Mwenyezi Mungu  amuongoze  na  aulainishe  moyo  wake  ili  aweze  kuingia  kwenye  Uislaam

Na ikiwa  mzazi  huyo  ameshafariki  hali  yakuwa  hakusilimu  na  kafa  kwenye  ukafiri  hapo  tena  haifai  kumuombea  Du'aa na  wala  kumuombea  (Maghufira) msamaha  kwasabubu  ameshakuwa  ni  mtu  wa  motoni  milele  na  ndio  ahadi  ya  Mwenyezi Mungu

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

قَالَ اللهُ تَعَالَى ﴿ اسْتَغْفِرْ لَهُمْ أَوْ لَا تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ إِن تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ سَبْعِينَ مَرَّةً فَلَن يَغْفِرَ اللَّهُ لَهُمْ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ ۗ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ ﴾

Waombee msamaha au usiwaombee. Hata ukiwaombea msamaha mara sabiini, Mwenyezi Mungu hatawasamehe. Hayo ni kwa sababu ya kuwa wao wamemkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotofu.

(Surat At-Tawba Aya-80)

Na  vile  vile  Mwenyezi Mungu  anatuambia  tena  kwa  kututahadharisha  kutokuwaombea  Du'aa  wakati  ambao  wameshafariki

قَالَ اللهُ تَعَالَى ﴿ مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴾

Haimpasii Nabii na wale walio amini kuwatakia msamaha washirikina, ijapo kuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao ni watu wa Motoni.(Surat At-Tawba Aya-113)

Na Allaah anajua zaidi



from fisabilillaah.com http://bit.ly/2BPgWCl
via IFTTT

al-Haa-iyyah 01 – Masjid Manyema Dodoma



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2AnoPPz
via IFTTT

Talkhiysw Swifatu Swalaat-in-Nabiy 05 (B) – Masjid Buhongwa Islamic Mwanza



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2BPy4YL
via IFTTT

Majibu kwa wanaotosheka na Qur-aan peke yake 03 – Radd kwa Abdi John



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2CHVJfa
via IFTTT

´Umdat-ul-Ahkaam 07



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2TpGlKb
via IFTTT

´Umdat-ul-Ahkaam 08



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2SweWpG
via IFTTT

Athar-ul-Adhkaar ash-Shar´iyyah 06



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2F1yI8q
via IFTTT

Athar-ul-Adhkaar ash-Shar´iyyah 05



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2QdB1Hr
via IFTTT

Photo - مكة المكرمة...



مكة المكرمة...

from FB-RSS feed for مكة المكرمة http://bit.ly/2EZiZYG
via IFTTT

Photo - رزقنا الله و إياكم صلاة فجر قريبا فى المسجد النبوى



رزقنا الله و إياكم صلاة فجر قريبا فى المسجد النبوى

from FB-RSS feed for مكة المكرمة http://bit.ly/2EYsC90
via IFTTT

Video



اللهم ارزقنا الصلاة فى المسجد الحرام قريبا

from FB-RSS feed for مكة المكرمة http://bit.ly/2EVHNRj
via IFTTT

Photo - اللهم ارزقنا الصلاة فى ساحات المسجد النبوى الشريف



اللهم ارزقنا الصلاة فى ساحات المسجد النبوى الشريف

from FB-RSS feed for مكة المكرمة http://bit.ly/2EYsB4W
via IFTTT

Photo - اللهم ارزق كل مشتاق الحج والعمرة يارب العالمين



اللهم ارزق كل مشتاق الحج والعمرة يارب العالمين

from FB-RSS feed for مكة المكرمة http://bit.ly/2EX9vNj
via IFTTT

السلام عليكم ورحمة الله وبركاتة متابعى صفحة مكة المكرمة الاعزاء استفتاء.. البلد الاكثر تفاعلا معنا لعام 2018 وسيتم اعلان اسم البلد الفائزغداا.. تحياتى للجميع.. مكة المكرمة..

السلام عليكم ورحمة الله وبركاتة
متابعى صفحة مكة المكرمة الاعزاء
استفتاء..
البلد الاكثر تفاعلا معنا لعام 2018
وسيتم اعلان اسم البلد الفائزغداا..
تحياتى للجميع.. مكة المكرمة..

from FB-RSS feed for مكة المكرمة http://bit.ly/2F1WW2L
via IFTTT

Photo - اللهم ارزقنا زيارة الحبيب المصطفى علية الصلاة والسلام



اللهم ارزقنا زيارة الحبيب المصطفى علية الصلاة والسلام

from FB-RSS feed for مكة المكرمة http://bit.ly/2EZiYnA
via IFTTT

Photo - اللهم اسقينا من ماء زمزم



اللهم اسقينا من ماء زمزم

from FB-RSS feed for مكة المكرمة http://bit.ly/2EZoDsX
via IFTTT

New video by Daarul I'LM TZ on YouTube

Shikamana na vitu hivi viwili-Sheikh Abuu 'Umayr Adam



View on YouTube

Jumapili, 30 Desemba 2018

kuondosha chakula kilichobaki kati ya meno kabla ya kutawadha?

Swali: 

Ni wajibu kwa mtu kuondosha chakula kilichobaki kati ya meno kabla ya kutawadha?


Jibu: 


Kilicho dhahiri kwangu ni kwamba sio wajibu kukiondosha kabla ya kutawadha. Lakini hapana shaka kuwa kusafisha meno ndio kamilifu, safi zaidi na mtu anaepuka maradhi ya meno. 


Kwa sababu uchafu huu ukibaki unaweza kusababisha harufu na kuleta magonjwa kwenye meno na fizi.
Mtu anatakiwa anapomaliza kula atumie mjiti kwenye meno yake ili kile chakula kilichobaki kwenye meno kiondoke. Vilevile atumie Siwaak. Kwa kuwa chakula kinabadilisha harufu ya kinywa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu Siwaak:
“Unasafisha kinywa na unamridhisha Mola.”
Hii ni dalili inayofahamisha kuwa kila pale ambapo kinywa kinahitajia kusafishwa basi kunasafishwa kwa Siwaak. 

Ndio maana wanachuoni wakasema kuwa imekokotezwa zaidi kutumia Siwaak wakati inapobadilika harufu ya kinywa kwa sababu ya kunywa au kwa sababu nyingine.


Marejeo : Majmuu´-ul-Fataawaa (11/140)


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2F14Ie3
via IFTTT

Nyaki za kutumia Mswaki

Swali: 

Ni lini imekokotezwa zaidi kutumia Siwaak? Ni ipi hukumu ya kutumia Siwaak wakati wa Khutbah?


Jibu: 


Imekokotezwa zaidi kutumia Siwaak wakati mtu anapoamka kutoka usingizini, mara ya kwanza mtu anapotaka kuingia nyumbani, wakati wa kutawadha katika kusukutua na mtu anaposimama kwa ajili ya kuswali.

Ni sawa kwa yule mwenye kusubiri swalah kutumia Siwaak. Lakini asitumie Siwaak wakati wa Khutbah. Kwani kufanya hivo kunamshughulisha. Isipokuwa ikiwa kama atakuwa na miayo. Katika hali hii atumie Siwaak ili kufukuza usingizi.


Marejeo : Majmuu´-ul-Fataawaa (11/115)


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2RnWhyV
via IFTTT

Kutumia sabuni wakati wa Wudhuu

Swali: 


Ni ipi hukumu ya kuosha mikono na uso kwa sabuni wakati wa kutawadha?


Jibu: 


Kuosha mikono na uso kwa sabuni wakati wa kutawadha sio jambo lililowekwa katika Shari´ah. Bali ni kupetuka mpaka na kupindukia. Imethibiti ya kwamba Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Wameangamia wale wenye kuvuka mipaka. Wameangamia wale wenye kuvuka mipaka.”
Alisema hivo mara tatu.
Lau tuseme kuwa kwenye mikono ya mtu kuna uchafu usiotoka isipokuwa kwa kutumia sabuni au kitu kingine kinachosafisha, katika hali hiyo hakuna ubaya.

Ama ikiwa ndio mazowea ya mtu basi kutumia sabuni kutazingatiwa kuwa ni kuvuka mipaka na Bid´ah. Mtu asifanye hivo.


Marejeo : Majmuu´-ul-Fataawaa (11/151)


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2GPuNyd
via IFTTT

Hukumu ya Wudhuu kwa mwaamke aliyepaka kucha rangi

Swali: 

Ni ipi hukumu ya wudhuu´ kwa yule ambaye kwenye kucha zake amepaka rangi ya kucha?



Jibu: 


Rangi ya kucha ni kitu anachopaka mwanamke juu ya kucha na ni kitu kilicho na ukoko. 


Kwahiyo haijuzu kwa mwanamke kuitumia kipindi ambapo anaswali kwa kuwa inazuia maji kufika kwenye ngozi wakati wa kutawadha. 


Kila kitu kinachozuia maji kufika kwenye ngozi haijuzu kwa mwenye kutawadha kukitumia. Kwa kuwa Allaah amesema:
فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ
“Hivyo basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi.” (05:06)
Mwanamke huyu ambaye amepaka juu ya kucha zake rangi ya kucha yanazuia maji kufika kwenye ngozi. 


Kwa hivyo hawezi kusadikishwa ya kwamba ameosha mikono. Katika hali hiyo anakuwa ameacha kiungo cha faradhi wakati wa kutawadha au wakati wa kuoga.
Kuhusu wale wasioswali, kama mfano wa mwanamke mwenye hedhi, hakuna neno kuitumia. Isipokuwa ikiwa kama rangi hii ni katika mambo maalum ya makafiri. Katika hali hiyo itakuwa haijuzu kwa kuwa itakuwa ni kujifananisha.
Nimewasikia baadhi ya watu waliotoa fatwa ya kwamba rangi hii inaingia katika aina ya kuvaa soksi na kwamba inajuzu kwa mwanamke kuitumia kwa muda wa mchana mmoja na usiku wake kwa yule ambaye ni mkazi na kwa muda wa michana mitatu na nyusiku zake kwa yule amabaye ni msafiri. Fatwa hii ni ya kimakosa. 


Sio kila kitu kinachofunika miili ya watu kinaingizwa katika soksi. Shari´ah imekuja kufahamisha kuwa mtu anatakiwa kufuta juu ya khofu pindi mtu anapohitajia kufanya hivo. Mguu unahitajia kufunikwa na kusitiriwa kwa kuwa unagusa chini katika ardhi kwenye changarawe, baridi na mengineyo. 


Ndipo Shari´ah ikaja kusunisha kufuta juu yake. Mtu anaweza kutumia kipimo juu ya kilemba vilevile. Si sahihi kwamba kilemba mahala pake ni kichwani. 


Kimsingi ni kwamba ufutaji wa kwenye kichwa ni mwepesi. Ufaradhi wa kwenye kichwa ni kufuta tofauti na mkono ambao unatakiwa kuoshwa. 


Kwa ajili hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumpa ruhusa mwanamke kufuta vifuniko vyake vya mikono (gloves) pamoja na kuwa vinafunika mikono. Hii ni dalili inayofahamisha kuwa haijuzu kwa mtu kutumia kipimo kwa kila kizuizi kinachozuia maji kufika na kikalinganishwa na kilemba na soksi.
Ni wajibu kwa muislamu kutumia juhudi zake katika kuitambua haki na wala asitoe fatwa yoyote isipokuwa atambue kuwa Allaah atamuuliza juu yake. Kwa kuwa mtu anaelezea kuhusu Shari´ah ya Allaah (´Azza wa Jall).


Marejeo : Majmuu´-ul-Fataawaa (11/147-148)


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2Ruf2AK
via IFTTT

Hukumu ya Kuacha mabega wazi kwa mwanamke

Swali: 

Ni ipi hukumu ya mwanamke kuswali na huku ameweka ´Abaa´ah yake juu ya mabega yake? Imenifikia kutoka kwako kwamba katika hali hii swalah yake inabatilika kwa kuwa imefanana na vazi la mwanaume.


Jibu: 


Allaah ndiye Mwenye kutakwa msaada. Mwanamke huyu imepokelewa vilevile kinyume chake katika yale yaliyoenezwa na wanawake kwamba sisi tunasema kwamba ni sawa kwa mwanamke kuvaa ´Abaa´ah juu ya mabega hata kama hilo litafanywa sokoni na madukani. Yote mawili ni makosa.
Sisi tunasema mwanamke kuweka ´Abaa´ah juu ya mabega yake wakati wa swalah hakuna neno. Kwa sababu hili ni jambo lililozoeleka kwa wanawake. Si jambo maalum kwa wanaume peke yao mpaka tuseme kuwa huku ni kujifananisha na wanaume.
Kuhusu mwanamke kuweka ´Abaa´ah yake juu ya mabega masokoni na mbele za watu asifanye hivo. Kwa sababu kule kuweka kwake ´Abaa´ah yake juu ya mabega kunapelekea kufichukua fomu ya mabega yake na shingo yake na kuonyesha kama shingo yake ni ndefu au ni fupi, jambo ambalo ni fitina. 


Iwapo wanawake wataruhusiwa kuweka ´Abaa´ah zao masokoni ni nani ambaye ana uhakika kama mambo hayatokuwa na wanawake wakaanza kutoka masokoni wakiwa na kanzu pasi na ´Abaa´ah? Kwa sababu wanawake mara nyingi wakifunguliwa mlango kidogo basi mlango unakuwa mkubwa. Huenda wakafikia mpaka kuufungua mlango wote na wakaingia kusikokuwa mlango.
Kwa hiyo tunasema kuweka ´Abaa´ah juu ya mabega wakati wa swalah hakuna neno. Hakubatilishi swalah. Ama kutembea nayo masokoni hapana. Kwa sababu kunapelekea katika fitina. Ni njia inayopelekea wanawake kupanuka zaidi katika mavazi.


Marejeo : Al-Liqaa' ash-Shahriy (42) 


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2EX60FQ
via IFTTT

Hukumu ya Mwanamke kuvaa nguo nyeupe

Swali: 


Hadiyth ambayo imependekeza kuvaa mavazi meupe, je, ni kwa wanaume na wanawake? Na je, ni jambo lililopendekezwa hata kwa wanaume?


Jibu


Lilio la dhahiri ni kuwa ni kwa wanaume. 


Kwa dalili ya Hadiyth ya ´Aaishah, ya kwamba aliona wanawake wa Answaar wametoka kwa ajili ya Swalah ya Fajr na walikuwa wamevaa mavazi meusi. Pamoja na haya, sio Haramu kwa mwanamke kuvaa mavazi meupe. Jambo lililo la Haramu kwake ni kujifananisha na wanaume. Kama ilivyokuja katika Swahiyh:
“Allaah Anamlaani mwanaume anayejifananisha na mwanamke; na mwanamke anayejifananisha na mwanaume.”


Na  Allaah  anajua  zaidi


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2EYqqz0
via IFTTT

Hukumu ya Mwanamke Kuvaa Jilbaab na suruali

Swali: 


Ni ipi hukumu ya mwanamke kuvaa ´Abaa´ah ya mapambo, anaweka ´Abaa´ah mabegani na kuvaa suruwali?


Jibu: 


Naam, kwanza kabisa Suruwali haijuzu kwa mwanamke. 


Kwasababu Suruwali sio vazi la mwanamke. 

Mwanamke anatakiwa kuvaa vazi pana, lenye kusitiri na lililo la wasaa. 


Kwahiyo haijuzu kwake kuvaa mavazi ya kubana. 


Suruwali ni vazi la kubana. Haijuzu kwake.
´Abaa´ah la mapambo halijuzu. ´Abaa´ah ni kwa ajili ya kujisitiri. Sio kwa ajili ya kujipamba. ´Abaa´ah halitakiwi kuwa na mapambo na michoro.
Wakati anapotoka ´Abaa´ah anatatakiwa kuliweka juu ya kichwa. Hata hivyo hakuna neno akaliweka mabegani mwake anapokuwa nyumbani au pamoja na wanawake wenzake.


Marejeo : Liqaa'-ul-Jumu´ah bit-Twaa'if

Na  Allaah anajua  zaidi


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2EX5WWC
via IFTTT

Hukumu ya Kula Tonge lilioanguka

Swali: 

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Linapoanguka tonge la mmoja wenu, basi aliondoshe uchafu na alile na wala asimwachie shaytwaan.”At-Tirmidhiy (1862).
Nifanye nini ikiwa  tonge hilo siwezi kuliondosha uchafu?


Jibu: 


Naam, Ikiwa huwezi kuliondosha uchafu na limechanganyikana na uchafu, hakuna la kufanya. 


Lakini hata hivyo liweke sehemu ambayo ni safi kwa ajili ya kuitukuza neema.


Marejeo : Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (58) 


Na Allaah  anajua  zaidi


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2F0ZvTa
via IFTTT

kunyamaza wakati wa kula ni Sunnah?

Swali: 

Je, ni adabu kunyamaza wakati wa kula?


Jibu: 


Hakuna msingi juu ya hilo. Msingi wakati wa kula na mambo mengine yote ni:
“Yule anayemuamini Allaah na siku ya Mwisho aseme yaliyo na kheri au anyamaze.”
Mambo yanatakiwa kuwa hivyo.


Marejeo : Fataawaa Raabigh (3)


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2SoPL8t
via IFTTT

Hukumu ya kutoelekea Qibla wakati wa kuchinja

Swali: 

Je, inatosha kusema “Bismillaah” bila ya kuelekea Qiblah, au ni lazima kufanya yote mawili (kusema Bismillaah na kuelekea Qiblah)? Kwa kuwa mahala ambapo nafanya kazi ni pafinyu na wala siwezi kuelekea Qiblah wakati wa kuchinja.
Jibu: 

Kusema “Bismillaah” wakati wa kuchinja ni jambo la wajibu, kwa kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) Kaamrisha hilo, na namna hii ndivyo alivyoamrisah Mtume (´alayhis-Swalaat was-Salaam). 

Haijuzu mtu kukusudia kuacha kusema “Bismillaah”. 


Mtu anatakiwa kusema wakati wa kuchinja “Bismillaah Allaahu Akbar”. Hii ndio Sunnah. Na lau atasema “Bismillaah” yatosha. 

Haifai kwake kukusudia kuacha kusema “Bismillaah”. Akiiacha kwa kusahau au kwa ujinga wa kutokujua, hakuna neno kwa hilo na kichinjo kitakuwa ni Halali. 

Lakini haifai kwake kuiacha kwa kukusudia. Ama kuelekea Qiblah ni jambo limependekezwa na wala sio la wajibu

Lau atachinja bila ya kuelekea Qiblah, ni sahihi na inajuzu. Lakini kuelekea kwake Qiblah wakati wa kuchinja ndio bora zaidi.


Mhusika : Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

Marejeo : Nuur ´alaad-Darb


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2ApSLuj
via IFTTT

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...