Waislamu wa Afrika ya Mashariki na duniani kwa ujumla wametakiwa wajihusishe na kulingania watu katika dini ya Mwenyezi Mungu.
Wito huo umetolewa na mlinganiaji kutoka nchini Uingereza, Ustadh Adnan Rashid kutoka taasisi ya Elimu na Utafiti (iERA) ya nchini Uingereza.
“Kama hufanyi da’awa, huitendei haki Qur’ an ya Mwenyezi Mungu… Kama hufanyi da’awa hutekelezi Sunna ya Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie),“ Sheikh Adnan aliuambia umati wa watu 5,000 waliohudhuria kongamano hilo katika hotuba aliyoitoa kwa Kiingereza iliyovuta hisia za watu waliokuwa wakimfuatilia.
Kuhusu kufuata Sunna ya Mtume, Sheikh Adnan alitoa mfano wa namna Rasulullah alivyopigwa mawe katika mji wa Taif na jitihada zake za da’awa katika maisha yake yote katika mazingira magumu ya kutengwa, kutukanwa na kadhalika.
Sheikh Adnan alisema Waislamu wa sasa tuna fursa nzuri zaidi ya kufanya da’awa kwa sababu tuna hali nzuri ya kimaisha kuliko walivyokuwa Maswahaba, ambao baadhi yao walikuwa na kipande kimoja tu cha nguo au viwili!
Alisema, hali za Waislamu wa sasa kimaisha ni nzuri lakini hatufanyi da’awa, jambo ambalo linasikitisha. “Mwenyezi Mungu ametuletea kitabu hiki ili nawe uende kukifundisha,” alisema Sheikh Adnan na kisha akanukuu hadithi tukufu ya Mtume isemayo: “Mbora wenu ni mwenye kujifundisha Qur’an kisha naye kuifundisha.” [Bukhari, Abu Dawud na Tirmidhiy].
Sheikh alisisitiza zaidi da’awa kwa wasio Waislamu. “Kufundisha huku Qur’an sio tu kwa Waislamu bali pia kwa wasio Waislamu,” alisema.
Sheikh Adnan alihoji Waislamu waliohudhuria kongamano hilo, vipi kama Mitume wangekuwepo mpaka sasa, je wangekuwa wanafanya da’awa kwa Waislamu pekee au kwa watu wote?
Sheikh Adnan alisema Uislamu ni dini inayokuwa kwa kasi ulimwenguni, na kutoa mfano kwa nchi ya Malawi ambako watu 3,000 walisilimu mwaka jana pekee. Aidha, alisema Uislamu unakua kila mahali duniani, kuanzia Japan, America ya Kusini, Ulaya, Marekani na kwingineko.
Akizungumzia kuhusu “Kitabu Changu” (Qur’an), mada kuu ya kongamano, mlinganiaji huyo wa dini linganifu alisema kitabu hicho kinabadili tabia na maisha, na kama hakitubadilishi basi hatuisomi sawa sawa.
Mfano alioutoa wa namna Qur’an inavyobadili maisha ni namna ilivyobadili maisha ya Waaarabu ambao kabla ya kuja Mtume (zama za ujahili) walikuwa wakiabudu masanamu, wakiua watoto wao wa kike, wakipigana kwa sababu ya vitu vidogo na maasi mengine mengi.
Hata hivyo baada ya kuja kwa Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie), kizazi kile cha Maswahaba na karne kadhaa zilizofuata wakawa watu bora kuwahi kutokea duniani.
Translate
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh YAFUATAYO NI MAJINA YA MASWAHABA WANAWAKE (RADHI ZA ALLAAH...
-
Dalili 18 zinazoashiria una ujauzito wa mtoto wa kiume Awali ya yote nitoe pongezi kwa mama K na Baba K wote popote walipo kwa kazi nzuri ...
-
Assallaaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Naam, Ndugu zangu katika Imaani, Siku chache zimebaki kwa ajili ya Vijana wetu wanaosoma Elim...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni