Taarifa iliyotolewa na Hamas imesema kuwa, kuhujumu na kuvunjia heshima Msikiti wa al Aqsa ni sawa na kucheza na moto. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, njama za utawala wa Kizayuni wa Israel za kutaka kulazimisha matakwa yake kuhusiana na Msikiti wa Alqsa hazitazaa matunda na Intifadha na mapambano ya wakazi wote wa Quds ni ujumbe wa wazi kwa viongozi wa utawala ghasibu wa Israel.
Harakati ya Hamas pia imewapongeza wakazi wa mji wa Quds kwa kuulinda Msikiti wa al Aqsa na maeneo mengine matakatifu na kusisitiza kuwa, Quds na Msikiti wa al Aqsa na maeneo ya Kiislamu, na taifa la Palestina litaendelea kutetea na kuyalinda maeneo hayo.
Hamas pia imeitaka Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kukabiliana na uhalifu wa wazayuni wa Israel dhidi ya Msikiti wa al Aqsa.
Msikiti huo na maeneo mengine matukufu ya Kiislamu vimekuwa vikishambuliwa na kuvunjiwa heshima mara kwa mara na Wazayuni wa Israel wanaopewa himaya na jeshi la utawala huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni