Translate

Jumapili, 15 Desemba 2019

Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislam - 10

Suala Nambari 10 Linaloeleweka Vibaya

 

Uislamu unazalisha jamii iliyo vivu, isiyoelimika kwasababu:
      • vitu vyote vinatokana na Mungu, na hivyo ni sawa kuamini hakuna hiari ya mwanaadamu-‘fatalism’
      •  
      • teknolojia na sayansi ya sasa haikubaliwi
      •  
Hoja zilizotolewa kwa suala hili linaloeleweka vibaya ni za uongo, na hilo suala wenyewe hakika limekanushwa moja kwa moja na Qur-aan na Sunnah. Wakati ni kweli kwamba Muumba ni chanzo cha kila kitu juu yetu, lakini sio kweli kwamba hili linaweza kutumika kuwa ni udhuru wa binaadamu kujificha kama aya zifuatazo kutoka Qur-aan zinavyoeleza (tafsiri):
 [16:35]

 [43:20]

Allaah Ametufundisha kupitia kwa Qur-aan na Sunnah kwamba sote tuna kiwango fulani cha uhuru. Uhuru huu ni lazima ufanyiwe kazi sawa sawa kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah ili kumridhisha Muumba. Hii ni hamasa iliyo kubwa kwa Waislamu wote kuwasukuma kuwa ni wenye ujuzi ulio bora, wanaweza kuwa Waislamu walio imara kabisa. Kama jamii ya Waisalmu leo hawawezi kusuluhisha matatizo yao, basi sio kwasababu ya uelewa wao wa Uislamu, isipokuwa ni kwasababu ya ujinga wao wa njia hii ya maisha. Umuhimu wa kutafuta elimu na kufanya kazi yanaelezwa wazi ndani ya Sunnah.

Kutokana na Sunnah, hususan ndani ya somo la Sunnah linaloitwa Sunnah ya Abuu-Daawuud, tunaona:
Amesimulia Anas bin Maalik: Mtu wa Answaar alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumuomba, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuuliza: Jee una chochote ndani ya nyumba yako? Akajibu: Ndio, kipande cha nguo, sehemu ambayo tunavaa na sehemu ambayo tunatandika (katika sakafu), na bakuli la mbao ambalo tunakunywia maji. Alisema: Vilete kwangu. Baadaye alivileta vitu hivi kwake na yeye (Mtume) alivichukua kwenye mkono wake na kuuliza: Ni nani atakayevinunua hivi? Mtu mmoja akasema: Mimi nitavinunua kwa dirham moja, Alisema mara mbili au mara tatu: Nani atajitolea zaidi ya dirham moja? Mtu mmoja akasema: Mimi nitanunua kwa dirham mbili. Alimpatia vitu hivi na kuchukua dirham mbili, na kumpatia Answaari, alisema: Nunua chakula kwa moja yake na wafikishie ukoo wako, na nunua shoka na lilete kwangu. Baadaye alilileta kwake. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliliunganisha mpini pamoja nalo kwa mikono yake na kusema: Nenda, tafuta kuni na uziuze, na nisikuone kwa wiki mbili. Mtu yule alikwenda zake na kutafuta kuni na kuuza. Alipopata dirham kumi, alikuja kwake na kumnunulia guo na baadhi yake kwa chakula. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Hili ni bora kwako (kuliko) lile, kuomba kutakuja kama ni alama kwenye uso wako Siku ya Hukumu. Kuomba ni ruhusa kwa watu watatu tu: yule ambaye anakufa kwa njaa, yule ambaye ana deni lililokuwa baya mno, au yule ambaye anahusika na kulipa fidia na anapata tabu kulipa.

Pia kutokana na Sunnah, hususan ndani ya somo la Sunnah linaloitwa Suna ya Ibn Majah, tunaona kwamba Mtume wa Allaah amesema:
Kutafuta elimu ni wajibu kwa kila Muislamu.

Ujuzi wa Qur-aan na Sunnah ndio aina za elimu zilizo bora kabisa, na elimu inayonufaisha binaadamu pia ni nzuri. Qur-aan na Sunnah hazizuii usomaji wa dunia hii na ukweli Muumba Anatuhimiza kuuchunguza ulimwengu tunaoishi kwa mujibu wa aya ifuatayo kutoka kwenye Qur-aan (tafsiri):
 [3:190-191]

Chochote kilicho kizuri ndani ya makala hii kinatokana na Allaah,
na kilicho kibaya ndani yake kinatokana na sisi.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...