Suala Nambari 7 Linaloeleweka Vibaya
Uislamu unakubali kuwaua watu wasio na hatia kwa sababu:
· Waislamu wanaweza kuwa ni magaidi
· Waislamu wanashiriki kwenye ‘vita tukufu’ (jihaad)
· Uislamu umeenea kwa panga
· Ni mfumo wa kisheria ulio katili na dhalimu
Siku hizi, suala hili linaloeleweka vibaya ni miongoni mwa lililoenezwa mno kabisa kuhusu Uislamu. Lakini bado ndani ya Qur-aan, Muumba Anaeleza bila ya utata (tafsiri):
[17:33]
Tukiegemea kwenye aya hii, hairuhusiki kwa Uislamu kuua mtu yeyote asiye na kosa kwa baadhi ya makosa ya jinai. Ni vyema tukakumbuka katika nukta hii, tofauti iliyofanywa hapo juu baina ya Qur-aan na Sunnah, na Waislamu; ni Qur-aan na Sunnah pekee ndizo zilizoafikiwa kuwa zinaendana pamoja na matakwa ya Muumba, wakati Waislamu wanaweza sana kutetereka. Hivyo, kama Muislamu yeyote ataua mtu asiye na hatia, Muislamu huyo ametenda dhambi mbaya kabisa, na hakika tendo hilo haliwezi kudaiwa kuwa limefanywa “kwa jina la Uislamu”.
Na itambulike wazi basi, kwamba “Gaidi Muislamu” inafanana na maneno mawili yenye kupewa maana tofauti ili kutoa msemo mmoja oxymoron: kwa kuua watu wasio na hatia, Muislamu anatenda dhambi kubwa, na Allaah ni anayefanywa kuwa Muadilifu personified. Msemo huu ni wa kukosa nidhamu na kuushushia hadhi Uislamu, na ni lazima uepukwe. Inategemewa kwamba; kwa vile uelewa na hamasa ya Uislamu inapanda juu kwa jamii iliyo ya kawaida ya watu, basi watu watayatenganisha mbali mbali maneno ya “ugaidi” na “Uislamu”, yasitumike ndani ya msemo mmoja.
Sababu nyingine inayokuzwa ili kukubaliana na suala hilo linaloeleweka vibaya ni kwamba Muumba Ameweka “jihaad” juu yetu. Tamko la “vita tukufu” linatokana na enzi za Vita vya Msalaba Crusades na limechimbuka ndani ya Uingereza kama ni kilio cha kasi dhidi ya Waislamu huko Jerusalem. Jihaad ni neno la Kiarabu lenye maana ya kupambana, lakini kwa mujibu wa maelezo ya aya nyingi ndani ya Qur-aan, linabeba maana ya mpambano wa kijeshi, au vita. Allaah Amewasilisha hatua kwa hatua wajibu wa mpambano wa kijeshi kwa jamii ya Waislamu wakati wa kipindi cha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Aya ya mwanzo iliyoshushwa kwa mnasaba huo ni kama ifuatayo (tafsiri):
[22:39]
Aya hii inaweka bayana masharti kabla ya kupigana vita vyovyote ndani ya Uislamu; ni lazima kuwepo masharti ya kuwepo unyanyasaji kwa watu. Muumba Ameweka wazi amri juu yetu ya kupigana dhidi ya unyanyasaji na udhalimu, hata kama ikiwa kwa gharama ya kumwaga damu kama aya ifuatayo inavyoonesha (tafsiri):
[2:190-192]
Kama ambavyo mtu anaweza kufikiria, taratibu za mpambano wa vita umetafsiriwa wazi na kwa upana ndani ya Qur-aan na Sunnah. Kwa vile hili ni somo moja lililo kubwa mno, tunafupisha kwa urahisi sehemu moja wapo kwa kutanabahisa kwamba haifai kuua wanawake, watoto, walemavu, wazee, na walio waadilifu. Kutokana na Sunnah, hususan ndani ya somo la Sunnah linaloitwa Sahih al-Bukhaariy, tunaona:
Imesimuliwa na ‘AbduLlaah: Wakati wa kipindi fulani cha vita Ghazawat enzi za Mtume, mwanamke alikutikana ameuawa. Mtume wa Allaah hakukubaliana na kuuawa kwa wanawake na watoto.
Suala (jengine) linaloeleweka vibaya ambalo linahusiana na jihaad, kawaida linatangazwa na Waislamu wanaosema kwamba “Jihaad ni kwa kuhami mipaka.” Qur-aan na Sunnah inakataa kabisa dhana hii. Kama aya iliyonukuliwa hapo juu inavyoonesha, jihaad ni wajibu wakati wote panapotokezea dhulma (na sio tu wakati wa kuhami mipaka), na Waislamu hawahitajii matamshi ya uongo yanayotolewa duniani pale inapokuja kusimamisha wajibu huu. Kutokana na Sunnah, hususan ndani ya somo la Sunnah linaloitwa Sahih al-Bukhaariy, tunaona:
Imesimuliwa na Abuu Mussa: Mtu mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kuuliza, “Mtu anapigana vita kwa ngawira; mwengine anapigana kwa umaarufu na wa tatu anapigana kwa kujionesha, ni yupi miongoni mwao anayepigana kwa ajili ya Allaah?” Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema, “Yule anayepigana kwa Neno la Allaah (yaani Uislamu) atakuwa bora, anayepigana kwa ajili ya Allaah.” [4:52:65]
Hivyo, Muumba Anatuwajibisha kupigana vita wakati wowote pale watu wanapokandamizwa vibaya hata kukosa uhuru wa kumsikiliza au kumfanyia kazi Mjumbe wa Allaah kama ilivyo ndani ya Qur-aan na Sunnah.
Sababu ya tatu ambayo kawaida huwa inanukuliwa kuhusu suala hili linaloeleweka vibaya katika Uislamu inasema kwamba njia hii ya maisha inakubaliana na kuuwa watu wasio na hatia kwasababu mfumo wake wa sheria ya Uislamu ni wenye ukatili usio na maana. Hoja hii ni nyepesi kwa namna mbili. Kwanza, inawafanya wanaadamu kuwa ni waadilifu na waliotakasika kuliko Muumba, na hivyo tunaweza kubadili Shariah. Pili, mara nyingi imeegemezwa kuidhania Shariah za Kiislamu ni zenye kutekelezeka kiulaini, kama vile kusema “wizi wote wanapata kukatwa mikono yao.”
Qur-aan na Sunnah imeweka wazi kwamba sheria ya kisasi, ni juu yetu kwa mauaji na jeraha la mwili, lakini msamaha ni bora kama aya zifuatazo kutoka Qur-aan zinavyoonesha (tafsiri):
[2:178]
[42:40-43]
Muumba Ameamrisha sheria ya kisasi juu yetu Akitambuwa vilivyo kwamba tunaweza kuijadili. Ndani ya jamii nyingi za leo zisizokuwa za Waislamu, kuna majadiliano yanayoendelea kuhusu adhabu ya kifo. Kwa Uislamu, mjadala huu ni butu, Muumba Amekwishalitolea maamuzi suala hilo kwa ajili yetu. Hata hivyo, Ametupatia aya ya ajabu ndani ya Qur-aan ambayo inatushauri kufikiria vyema suala hilo vizuri kama tunahitaji kuielewa (tafsiri inafuata):
[2:179]
Watu wengi pia hawapo na uelewa wa sharti zilizo kali ambazo ni lazima zitimizwe kwa sheria ya kisasi kufanyiwa kazi. Sunnah imejaa mifano ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ikituonesha pale sharti za sheria ya kisasi zinapotimizwa kabla ya kufanyiwa kazi. Kwa mfano, mwizi atawajibika tu kukosa mkono wake kama bidhaa aliyoiba imevuka kiwango fulani, na kama ikithibitishwa kwamba bidhaa hiyo imehamishwa kutoka sehemu yake ya awali. Wizi wa chakula hauna adhabu ya mtu kukosa mkono wake, na bidhaa nyengine pia zimesameheka. Huu ni mfano tu wa namna sheria zinavyofanyiwa kazi kwa hadhari sana ndani ya Uislamu.
Mwisho, hoja nyengine inayokuzwa kwa suala hili linaloeleweka vibaya mno ni kwamba Uislamu ‘umeenea kwa panga’. Ni lazima ieleweke kwa sasa kwamba ni lazima daima tutofautishe baina ya Qur-aan na Sunnah na Waislamu pale inapofika hatua ya kutambua nini Muumba Ametuhitajia (sisi kufanya). Allaah Ameeleza wazi ndani ya Qur-aan (tafsiri),
[2:256]
Hivyo, HAIWEZEKANI kukubali Uislamu kwa nguvu. Hata kama Waislamu wasio na uongofu watajaribu ‘kulazimisha’ Uislamu namna fulani kwa wengine, haitokubaliwa na Muumba kwa mujibu wa aya hii.
Mijadala ya taariykh ambayo inajaribu kufafanua kwamba Waislamu ‘hawajawabadili wengine kwa nguvu’ hakika ni hoja ndogo kwa mjadala uliopo hapo juu. Hata hivyo, ni vyema kubainisha kwamba (kwa mujibu wa) taariykh, Uislamu umeenea kwa njia za amani. Ujumbe wa Muumba ulifikishwa Afrika na kusini mwa mashariki ya Asia kwa wafanyabiashara walio Waislamu, na leo nchi kubwa kabisa yenye Waislamu duniani ni Indonesia. Safari za kijeshi zilizopelekea kuteka nyara kwa kuzungushia mipaka ya Ulaya na Asia ya kati, zote zilifanikiwa kwa (Uislamu) kustahamilia imani na kanuni (za dini) nyengine.
Kwa mara nyengine, ni muhimu kukumbuka kwamba Allaah Anatamka kwamba HAIWEZEKANI Uislamu kulazimishwa kwa mtu, hivyo Waislamu hawaoni haja ya kujaribu!
Itaendelea In Shaa Allaah...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni