Uislamu unaamrisha kumuabudia mwanaadamu kwa sababu:
· Waislamu ni ‘Wafuasi wa Muhammad’
JIBU:
Wasio kuwa Waislamu wa kale ambao walionekana kama kwamba ni watafiti wa Uislamu waliita ‘Dini ya Muhamaadi’, wakimaanisha kwa maana nyengine kwamba Waislamu walimuabudia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo, msingi wa suala hili (la uongo) ni kwamba hakika linatokana na wasiokuwa Waislamu. Hata hivyo, kama ilivyoelezwa hapo juu, ‘Muislamu’ ni “yule anayemnyenyekea Allaah”. Asili ya Uislamu ni kwenye hali ya umoja ulio safi, tena safi, safi kabisa. Allaah Anasema ndani ya Qur-aan (iliyotafsiriwa):
[112:1-4]
[3:144]
Kutokana na Sunnah, hususan ndani ya somo la Sunnah katika Swahiyh al-Bukhaariy, tunaona:
Amesimulia Mu’aadh bin Jabal: Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Ewe Mu’aadh! Je unatambua haki ya Allaah juu ya waja Wake?” Nikasema: “Allaah na Mtume Wake wanajua lililo bora” Mtume akasema: “Kumuabudia Yeye (Allaah) Pekee na bila ya kumshirikisha na chochote pamoja Naye (Allaah) kwenye ibada. Je unatambuwa haki yao juu Yake?” Nikajibu: “Allaah na Mtume Wake wanajua lililo bora” Mtume akasema: “Kutowaadhibu (kama wakimuabudu).” [9:93:470]
Amesimulia ‘Umar: Nimemsikia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Musivuke mpaka katika kunisifu kama Wakristo walivyomsifu mtoto wa Maryam, kwani mimi ni mja. Hivyo, niiteni Mja wa Allaah na Mjumbe Wake.” [4:55:654]
Itaendelea In Shaa Allaah...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni