Aayah Na Mafunzo
Aal-‘Imraan
Allaah Atakughufuria Madhambi Hata Kama Ukikariri Kumuasi
وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٣٥﴾
135. Na wale ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao (kwa maasi), humdhukuru Allaah wakaomba maghfirah kwa madhambi yao. Na nani anayeghufuria madhambi isipokuwa Allaah. Na hawaendelei katika waliyoyafanya na wao wanajua.
أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُم مَّغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَجَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ ﴿١٣٦﴾
136. Hao jazaa yao ni maghfirah kutoka kwa Rabb wao na Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo. Na uzuri ulioje ujira wa watendaji (wema). [Aal-'Imraan 135-136]
Mafunzo:
Hakika fadhila nyingi kabisa zimetajwa katika Qur-aan na Sunnah kuhusu kuomba tawbah, mojawapo: Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Mja alifanya dhambi akasema: Ee Allaah, nighufurie dhambi zangu. Allaah (عزّ وجلّ) Akasema: Mja wangu kafanya dhambi akajua kuwa anaye Rabb wa kumghufuria dhambi na kuziondosha. Kisha akarudia kufanya dhambi tena akasema: Ee Allaah nighufurie dhambi zangu. Allaah (Tabaaraka wa Ta’aala) Akasema: Mja wangu kafanya dhambi akajua kuwa anaye Rabb wa kumghufuria dhambi na kuziondosha. Kisha akarudia kufanya dhambi tena akasema: Ee Allaah nighufurie dhambi zangu. Allaah (عزّ وجلّ) Akasema: Mja wangu kafanya dhambi akajua kuwa anaye Rabb wa kumghufuria dhambi na kuziondosha. Nakushuhudisheni kwamba Nimemghufuria na afanye mja Wangu atakavyo.” [Ahmad].
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni