Waislamu wa jamii ya Rohingya wameitaka jamii ya kimataifa isikubali matamshi ya Aung San Suu Kyi, kiongozi wa chama tawala nchini Myanmar aliyoyatoa katika Mahkama ya Kimataifa ya Uadilifu ICJ.
Hii ni baada ya Jumatano ya jana Suu Kyi kujitetea katika mahkama hiyo huko Uholanzi kutokana na hujuma za serikali yake kuwalenga Waislamu wa jamii hiyo nchini Myanmar. Katika utetezi wake Suu Kyi alipinga kujiri aina yoyote ya mauaji dhidi ya Waislamu nchini kwake na kudai kuwa sababu ya mamia ya Waislamu hao kuondoka Myanmar na kuelekea nchi nyingine ilitokana na vita dhidi ya waasi. Aung San Suu Kyi ametoa kauli hiyo katika hali ambayo mwaka 2017 jeshi la nchi hiyo lilifanya mauaji makubwa ya umati kuwalenga Waislamu wa jamii ya Rohingya, kufanya vitendo vya ubakaji na udhalilishaji wa kijinsia na pia kuteketeza kwa moto nyumba zao.Jamii ya Waislamu wa Rohingya inayokandamizwa zaidi nchini Myanmar kutokana na imani yao |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni