Translate
Jumatano, 18 Desemba 2019
Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili
CHAKULA CHA MGONJWA MWENYE KISUKARI AINA YA PILI Chakula bora kabisa kwa mgonjwa wa kisukari ni kile ambacho ni chakula cha asili na si kile ambacho kimetengenezwa kiwandani. Unahitaji chakula ambacho hakijakobolewa, unahitaji zaidi matunda na mboga za majani. Kutumia vyakula hivi naenda kukueleza kwenye hii makala kutakusaidia kupata mahitaji […]
Msikiti Mtakatifu wa al-Aqswa wavamiwa tena
Walowezi wa Kizayuni leo wameuvamia tena Msikiti wa al-Aqswa huko Palestina wakisaidiwa na askari wa jeshi la utawala haramu wa Israel na kuuvunjia heshima msikiti huo ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.
Walowezi hao wa Kizayuni baada ya kuingia katika eneo la ndani la msikiti huo mtakatifu walisikika wakipiga nara dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Vyombo vya habari vya Palestina vimeripoti kwamba, hujuma na uvamizi huo umefanyika kwa msaada na uungaji mkono wa wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel.
Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za kukabiliana na vitendo hivyo.
Kwa mujibu wa duru za Kipalestina, karibu kila siku walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakifanya uvamizi katika msikiti huo lengo likiwa ni kutekeleza njama za kutokomeza utambulisho wa Kiislamu na Kikristo wa Msikiti wa al-Aqswa na badala yake kuweka nembo za Kizayuni.
aqswa
Bakwata wampongeza Rais Wa Tanzania kwa kwasamehe wafungwa 5,000
Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limeadhimisha miaka 51 tangu kuanzishwa kwake kwa mafanikio kadhaa, huku likimpongeza Rais John Pombe Magufuli wa nchi hiyo kwa namna anavyowatumikia wanyonge ikiwamo kuwapatia msamaha zaidi ya wafungwa 5,000 hivi karibuni
Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limetoa wito kwa wafungwa walioachiliwa, kutumia fursa ya maisha yao kutenda mema na kutumikia nchi yao kama nguvu kazi muhimu katika jamii na wasirejee tena katika vitendo vya uhalifu na uovu.
Akihutubia hapo jana jijjini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) Nuhu Mruma alisema kuwa, taasisi hiyo inampongeza sana Rais Magufuli kwa kuwasamehe wafungwa hao ambao bado walikuwa hawajamaliza muda wao wa kukaa gerezani.
Katika maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika mkoani Mwanza Disemba 9 mwaka huu, Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliandika historia mpya kwa mara ya kwanza tangu nchi ipate uhuru kwa kutangaza msamaha kwa wafungwa 5,533.
Wakati Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) likimpongeza Rais Magufuli kwa msamaha wake kwa wafungwa, baadhi ya wafungwa walioachiliwa huru hivi karibuni kwa msamaha wa Rais wameripotiwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu na hata mauaji. Inaarifiwa kuwa, mtu mmoja ambaye aliachiwa huru kwa msamaha wa Rais Dkt. John hivi karibuni aliwavamia na kuwachoma visu watu 6 huku mmoja wao akifariki dunia hapo hapo. Tukio lilitokea katika eneo la Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera. Baada ya mtuhumiwa kutekeleza tukio hilo, wananchi wenye hasira kali walimvamia na kuanza kumshambulia hadi kumuua.
Jumanne, 17 Desemba 2019
Aliyekamilika Iymaan Kwa Tabia Na Kumfanyia Wema Mke
Lu-ulu-un-Manthuwrun
(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)
Hadiyth Ya 29
Aliyekamilika Iymaan Kwa Tabia Na Kumfanyia Wema Mke
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((أَكْمَلُ الْمُؤْمِنِينَ إِيمَانًا أَحْسَنُهُمْ خُلُقًا وَخِيَارُكُمْ خِيَارُكُمْ لِنِسَائِهِمْ خُلُقًا)) الترمذي وقال: حديث حسن صحيح
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Muumin aliyekamilika iymaan ni aliye na tabia njema kabisa, na wabora wenu ni walio bora kwa wake zao kwa tabia)) [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Swahiyh Hasan]
Mafunzo na Mwongozo:
1. Uislamu unasisitiza kuwa na tabia njema kwa kila mtu.
2. Mume anasisitizwa kumfanyia wema mkewe katika maisha ya ndoa, si kumfanyia uovu. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلَا تَنسَوُا الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ ۚ
Na wala msisahau fadhila baina yenu. [Al-Baqarah (2: 237)]
Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ
Na kaeni nao kwa wema. [An-Nisaa (4: 19)]
Pia rejea kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): [Ar-Ruwm 30: 21]
3. Inapasa kuweko subira baina ya mume na mke katika mitihani inayowakabili ya maisha baina yao. [((Na mkisubiri ni kheri kwenu)) [An-Nisaa (4: 25)].
4. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni kigezo bora kabisa katika kuamiliana na wake [Al-Ahzaab (33: 21)].
Pia Hadiyth zifuatazo:
((Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa mke wake, na mimi ni mbora kwa watu wangu wa nyumbani [ahli])) [Ibn Maajah na Ad-Daarimiy].
((Mwanamke ameumbwa kwa ubavu, na sehemu iliyopinda ya ubavu ni juu yake, ukijaribu kuunyoosha utauvunja, na lau utauacha utaendelea kupinda, nakuusieni [kuwafanyia wema]) wake zenu)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
((Allaah, Allaah, kwa wanawake, hao ni wasaidizi wenu walio kwenye mikono yenu, mmewachukuwa kama ni amana kutoka kwa Allaah, na imekuwa halali tupu zao kwenu kwa neno lake Allaah [iyjaab na qubuwl])) [Muslim, Abu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad]
Rejea pia Hadiyth namba (28), (35), (40).
Kuvumiliana Tabia Mbaya Katika Maisha Ya Ndoa Kwa Kukumbuka Tabia Zilizo Nzuri
Lu-ulu-un-Manthuwrun
(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)
Hadiyth Ya 28
Kuvumiliana Tabia Mbaya Katika Maisha Ya Ndoa Kwa Kukumbuka Tabia Zilizo Nzuri
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((لاَ يَفْرَكْ مُؤْمِنٌ مُؤْمِنَةً إِنْ كَرِهَ مِنْهَا خُلُقًا رَضِيَ مِنْهَا آخَرَ)) مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Muumin [mume] asimchukie Muumin [mke]. Asipompendelea kwa tabia fulani ataridhika naye kwa tabia nyingine)) [Muslim]
Mafunzo Na Mwongozo:
1. Hakuna binaadamu aliyekamilika kwa tabia njema. Kila mmoja ana kasoro zake; huenda zikawa ni tabia zinazolingana; nzuri au mbaya.
2. Kuishi pamoja kunadhihirisha tabia baina ya watu.
3. Inapasa kuvumiliana katika maisha ya ndoa, kwani kila mmoja ni mtihani kwa mwenziwe. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَجَعَلْنَا بَعْضَكُمْ لِبَعْضٍ فِتْنَةً أَتَصْبِرُونَ ۗ وَكَانَ رَبُّكَ بَصِيرًا ﴿٢٠﴾
Na Tumejaalia baadhi yenu nyinyi kwa nyinyi kuwa ni majaribio je mtasubiri? Na Rabb wako ni Mwenye kuona daima. [Al-Furqaan: 20]
4. Uislamu unamsisitiza mume kumfanyia wema mke.
Rejea: An-Nisaa (4: 19).
Rejea pia Hadiyth namba (29).
5. Hadiyth hii ni suluhisho mojawapo la kutatua matatizo baina ya mume na mkewe.
Rejea An-Nisaa (4: 128).
6. Inasisitizwa Muislamu kuchagua mke mwema, kwani ndio sababu ya furaha yake duniani na Aakhirah.
Rejea Hadiyth namba (35), (40).
7. Hii Hadiyth inamtaka mume awe makini wala asichukue hatua za haraka kama talaka ambayo huenda ikamletea majuto.
Sheikh wa wilaya ya Kasulu Akanusha habari kuhusu kukatazwa kwa Azana katika swala ya Asubuhi
Baada ya habari kusambaza katika mitandao ya kijamii kuhusu mkuu wa wilaya ya kasulu kutakaza Azan na utumikaji wa spika katika swala ya asubuhi swalat Fajr, Muislamu blog imemtafuta sheikh mkuu wa wilaya ya kasulu bwana masoud swedi kikoba ili kuthibitisha habari hizo.
Sheikh Masoud swedi kikoba amekanusha habari hizo na kusema kuwa hakuna zuio wala katazo lolote kuhusu kutumika kwa spika katika swala ya alfajr ispokuwa mkuu wa wilaya ya kasulu amezuia kuweka mawaidha na adhkaar wakati wa usiku kabla ya swala ya Alfajr ili kuepuka kuwapa usumbufu Raia wengine.
Akithibisha habari hizo amesema sheikh masoud kuwa wenda wasambazaji wa habari hizo hawakumuelewa mkuu wa wilaya hiyo, pia sheikh amesema kuwa yeye kwasasa hayupo katika mji wa kasulu na amewasiliana na maimamu wa msikiti wamemthibitishia hakuna kadhia yeyote kuhusu habari hizo zinazoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii.
Amewataka waislamu kuchunguza habari kabla ya kuieneza wenda wakaingia katika makosa bila ya wao wenyewe kujua.
Sheikh Masoud swedi kikoba amekanusha habari hizo na kusema kuwa hakuna zuio wala katazo lolote kuhusu kutumika kwa spika katika swala ya alfajr ispokuwa mkuu wa wilaya ya kasulu amezuia kuweka mawaidha na adhkaar wakati wa usiku kabla ya swala ya Alfajr ili kuepuka kuwapa usumbufu Raia wengine.
Akithibisha habari hizo amesema sheikh masoud kuwa wenda wasambazaji wa habari hizo hawakumuelewa mkuu wa wilaya hiyo, pia sheikh amesema kuwa yeye kwasasa hayupo katika mji wa kasulu na amewasiliana na maimamu wa msikiti wamemthibitishia hakuna kadhia yeyote kuhusu habari hizo zinazoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii.
Amewataka waislamu kuchunguza habari kabla ya kuieneza wenda wakaingia katika makosa bila ya wao wenyewe kujua.
Palestina yataka walowezi wa Kizayuni watambuliwe rasmi kuwa ni magaidi
Wizara ya Mambo ya Nje ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imetoa wito wa kuwekwa jina la walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina katika orodha ya magaidi.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imelaani hatua za kigaidi za utawala wa Kizayuni wa Israel na kuitaka jamii ya kimataifa kuliweka jina la walowezi wa Kizayuni katika orodha ya magaidi kutokana na jinai zinazofanywa mara kwa mara na walowezi hao.
Taarifa ya wizara hiyo pia imesema kuwa, ripoti za hivi karibuni na matamshi ya maafisa usalama wa Israel vinaonesha kuwa, kuna ongezeko kubwa la mashambulizi na jinai zinazofanywa na walowezi wa Kiyahudi dhidi ya raia wa Palestina. Imeongeza kuwa kiwango cha hasara zilizosababishwa na mashambulizi hayo kimeongezeka mara dufu.
Katika miezi ya karibuni walowezi wa Kizayuni wamezidisha mashambulizi dhidi ya raia wa Palestina, kuvamizi mali na milki zao na kuuvunjia heshima Msikiti wa al Aqsa.
Harakati za mapambano ya ukombozi wa Palestina zikiwemo Hamas na Jihad Islami zimetahadharisha kuhusu mashambulizi hayo na kutangaza kwamba, Msikiti wa al Aqsa ni mstari mwekundu ambao haupaswi kuvukwa.
Jumatatu, 16 Desemba 2019
Kila Mtu Ana Jukumu La Kuchunga Atakaloulizwa
Lu-ulu-un-Manthuwrun
(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)
Hadiyth Ya 27
Kila Mtu Ana Jukumu La Kuchunga Atakaloulizwa
عَنْ ابْنِ عُمَرَ (رضي الله عنهما) عَنْ النَّبِيِّ (صلى الله عليه و آله وسلم) قَالَ: ((كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ، وَالأمِيرُ رَاعٍ، وَالرَّجُلُ رَاعٍ عَلَى أَهْلِ بَيْتِهِ، وَالْمَرْأَةُ رَاعِيَةٌ عَلَى بَيْتِ زَوْجِهَا وَوَلَدِهِ، فَكُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ)) متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (رضي الله عنهما) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Nyote ni wachunga na kila mmoja wenu ataulizwa kuhusu alichokichunga. Kiongozi ni mchunga, na mume ni mchunga juu ya mkewe na mke ni mchunga juu ya nyumba ya mumewe na watoto wake. Kwa hivyo nyote ni wachunga na kila mmoja wenu ataulizwa kuhusu alichokichunga)). [Al-Bukhaariy na Muslim]
Mafunzo Na Mwongozo:
1. Kila Muislamu analo jukumu lake ambalo ni limekuwa ni amana kwake kuichunga. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّا عَرَضْنَا الْأَمَانَةَ عَلَى السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَالْجِبَالِ فَأَبَيْنَ أَن يَحْمِلْنَهَا وَأَشْفَقْنَ مِنْهَا وَحَمَلَهَا الْإِنسَانُ ۖ إِنَّهُ كَانَ ظَلُومًا جَهُولًا ﴿٧٢﴾
Hakika Sisi Tulihudhurisha amana kwa mbingu na ardhi na majabali vikakataa kuibeba na vikaiogopa; lakini insani akaibeba. Hakika yeye amekuwa dhalimu mno, jahili mno. [Al-Ahzaab (33: 72)]
2. Jukumu ni amana na kila Alitochuruzuku Allaah (سبحانه وتعالى) ni neema kwetu, ikiwa ni mali au mke, au mume, au watoto, au elimu, na kila mmoja ataulizwa kuhusu neema hizo. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
ثُمَّ لَتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ ﴿٨﴾
Kisha bila shaka mtaulizwa Siku hiyo kuhusu kuhusu neema. [At-Takaathur: 8]
3. Kutimiza amana ni miongoni mwa sifa zitakazompatia Muislamu Jannah ya Firdaws kama zilivyotajwa katika Suwrah: Al-Muuminuwn (23: 1-11)
4. Mume na mke washirikiane katika malezi ya watoto ili watoto wakuwe na kuinukia katika maadili mazuri ya Kiislamu.
5. Mwanamke wa Kiislamu ana cheo kikubwa kwa kuwa ana jukumu kubwa la ulezi wa nyumba yake, na ameahidiwa kupata Jannah.
Rejea Hadiyth namba (26).
6. Kutimizia amana au jukumu ni jambo mojawapo la kumwezesha mtu kuvuka As-Swiraatw Siku ya Qiyaamah
Hadiyth: ((...na zitatumwa amana na ar-rahm [fuko la uzazi; uungaji udugu], navyo vitasimama pembeni ya Swiraatw kuliani na kushotoni…..))].[Muslim]
03-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa Mahari
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلنِّكَاحِ
Kitabu cha Nikaah (Ndoa)
بَابُ اَلصَّدَاقِ
03-Mlango Wa Mahari
879.
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، عَنِ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {أَنَّهُ أَعْتَقَ صَفِيَّةَ، وَجَعَلَ عِتْقَهَا صَدَاقَهَا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “alimuacha huru Swafiyyah[1] na akafanya kumuacha huru kwake ndio mahari yake.”[2] [Al-Bukhaariy, Muslim]
880.
وَعَنْ أَبِي سَلَمَةَ بْنِ عَبْدِ اَلرَّحْمَنِ، رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّهُ قَالَ: {سَأَلْتُ عَائِشَةَ زَوْجَ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ كَمْ كَانَ صَدَاقُ رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَتْ: كَانَ صَدَاقُهُ لِأَزْوَاجِهِ ثِنْتَيْ عَشْرَةَ أُوقِيَّةً وَنَشًّا. قَالَتْ: أَتَدْرِي مَا اَلنَّشُّ ؟ قَالَ: قُلْتُ: لَا. قَالَتْ: نِصْفُ أُوقِيَّةٍ. فَتِلْكَ خَمْسُمِائَةِ دِرْهَمٍ، فَهَذَا صَدَاقُ رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ لِأَزْوَاجِهِ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Salamah bin ‘Abdir-Rahmaan[3] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nilimuuliza ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) mahari ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ilikuwa kiasi gani?[4] Akasema: Mahari ya wakeze yalikuwa ni wakia kumi na mbili na An-Nash. Akasema: Unajua ni nini An-Nash? Akasema Hapana. Akasema: ni nusu wakia. Kwa hivyo hizo ni dirhamu mia tano (500) haya ndiyo mahari ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kwa wakeze.” [Imetolewa na Muslim]
881.
وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ : {لَمَّا تَزَوَّجَ عَلِيٌّ فَاطِمَةَ عَلَيْهِمَا اَلسَّلَامُ . قَالَ لَهُ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ " أَعْطِهَا شَيْئًا " ، قَالَ: مَا عِنْدِي شَيْءٌ . قَالَ:" فَأَيْنَ دِرْعُكَ الحُطَمِيَّةُ ؟} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “’Aliy alipomuoa Faatwimah عَلَيْهِمَا اَلسَّلَامُ, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuambia: Mpe kitu (kama mahari yake), ‘Aliy akasema: Sina kitu, Rasuli wa Allaah akasema: Iko wapi ile deraya yako ya Al-Hutwamiyyah?.”[5] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy na akaisahihisha Al-Haakim]
882.
وَعَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {أَيُّمَا اِمْرَأَةٍ نَكَحَتْ عَلَى صَدَاقٍ، أَوْ حِبَاءٍ، أَوْ عِدَةٍ، قَبْلَ عِصْمَةِ اَلنِّكَاحِ، فَهُوَ لَهَا، وَمَا كَانَ بَعْدَ عِصْمَةِ اَلنِّكَاحِ، فَهُوَ لِمَنْ أُعْطِيَهُ، وَأَحَقُّ مَا أُكْرِمَ اَلرَّجُلُ عَلَيْهِ اِبْنَتُهُ، أَوْ أُخْتُهُ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةُ إِلَّا اَلتِّرْمِذِيَّ
Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb kutoka kwa baba yake naye kutoka kwa babu yake amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwanamke yeyote anayeolewa kwa mahari, zawadi au kwa ahadi ya kupewa zawadi kabla ya kifungo cha ndoa, basi kitu hicho ni chake.[6] Na kinachotolewa baada ya kifungo cha ndoa hicho ni cha aliyepewa. Na kilicho haki zaidi mtu kukirimiwa kwa sababu yake ni binti yake au dada yake.” [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) isipokuwa At-Tirmidhiy.
883.
وَعَنْ عَلْقَمَةَ، عَنِ ابْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ { أَنَّهُ سُئِلَ عَنْ رَجُلٍ تَزَوَّجَ اِمْرَأَةً، وَلَمْ يَفْرِضْ لَهَا صَدَاقًا، وَلَمْ يَدْخُلْ بِهَا حَتَّى مَاتَ، فَقَالَ اِبْنُ مَسْعُودٍ: لَهَا مِثْلُ صَدَاقِ نِسَائِهَا، لَا وَكْسَ، وَلَا شَطَطَ، وَعَلَيْهَا اَلْعِدَّةُ، وَلَهَا اَلْمِيرَاثُ، فَقَامَ مَعْقِلُ بْنُ سِنَانٍ الْأَشْجَعِيُّ فَقَالَ: قَضَى رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ فِي بِرْوَعَ بِنْتِ وَاشِقٍ اِمْرَأَةٍ مِنَّا مِثْلَ مَا قَضَيْتَ، فَفَرِحَ بِهَا اِبْنُ مَسْعُودٍ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةُ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ وَالْجَمَاعَةُ
Kutoka kwa ‘Alqamah[7] naye kutoka kwa Ibn Mas ‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) aliulizwa: “kuhusu mtu aliyeoa mke, hakumkadiria mahari, wala hakumuingilia hadi akafa. Ibn Mas‘uwd akasema: ana mfano wa mahari ya wanawake wake, hakuna kupunguza wala kuzidisha, naye (mwanamke) itamlazimu akae eda na pia anastahiki kupata mirathi. Ma’qil bin Sinaan Al-Ashja’iyy akasimama na akasema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alihukumu kwa Birwa’[8] bint Waashiq ni mwanamke miongoni mwetu kama hivyo ulivyo hukumu wewe. Ibn Mas-‘uwd akafurahi kwa ushahidi huu.” [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) na akaisahihisha At-Tirmidhiy na ‘Ulamaa
884.
وَعَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: { مَنْ أَعْطَى فِي صَدَاقِ اِمْرَأَةٍ سَوِيقًا، أَوْ تَمْرًا، فَقَدْ اِسْتَحَلَّ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَأَشَارَ إِلَى تَرْجِيحِ وَقْفِهِ
Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kutoa Sawiyq[9] au tende katika mahari ya mwanamke basi amekuwa halaal kwake mwanamke huyo.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd]
885.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَامِرِ بْنِ رَبِيعَةَرَضِيَ اللهُ عَنْهُ ، عَنْ أَبِيهِ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ أَجَازَ نِكَاحَ اِمْرَأَةٍ عَلَى نَعْلَيْنِ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَهُ، وَخُولِفَ فِي ذَلِكَ
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Aamir bin Rabiy’ah[10] kutoka kwa baba yake (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Ameruhusu mwanamke kuolewa kwa (mahari ya) viatu.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na akaisahihisha na amekhalifiwa katika hilo (la kufanya Hadiyth kuwa ni sahihi)
886.
وَعَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: {زَوَّجَ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ رَجُلاً اِمْرَأَةً بِخَاتَمٍ مِنْ حَدِيدٍ} أَخْرَجَهُ اَلْحَاكِمُ.
وَهُوَ طَرَفٌ مِنَ الْحَدِيثِ اَلطَّوِيلِ اَلْمُتَقَدِّمِ فِي أَوَائِلِ اَلنِّكَاحِ
Kutoka kwa Sahl bin Sa’d (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuoza mtu mwanamke kwa (mahari ya) pete ya chuma.” [Imetolewa na Al-Haakim nayo ni sehemu katika Hadiyth ndefu iliyotangulia mwanzo wa Mlango wa Ndoa][11]
887.
وَعَنْ عَلَيٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: {لَا يَكُونُ اَلْمَهْرُ أَقَلَّ مِنْ عَشَرَةِ دَرَاهِمَ} أَخْرَجَهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ مَوْقُوفًا، وَفِي سَنَدِهِ مَقَالٌ
Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Mahari haiwi chini ya dirhamu kumi.” [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniyy ikiwa ni Mawquwf na katika Isnaad yake kuna maelezo]
888.
وَعَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {خَيْرُ اَلصَّدَاقِ أَيْسَرُهُ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
Kutoka kwa ‘Uqbah bin ‘Aamir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mahari yalio na kheri ni yalio mepesi.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na akaisahihisha Al-Haakim]
889.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا {أَنَّ عَمْرَةَ بِنْتَ اَلْجَوْنِ تَعَوَّذَتْ مِنْ رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ حِينَ أُدْخِلَتْ عَلَيْهِ تَعْنِي: لَمَّا تَزَوَّجَهَا فَقَالَ: "لَقَدْ عُذْتِ بِمَعَاذٍ"، فَطَلَّقَهَا، وَأَمَرَ أُسَامَةَ فَمَتَّعَهَا بِثَلَاثَةِ أَثْوَابٍ} أَخْرَجَهُ اِبْنُ مَاجَهْ، وَفِي إِسْنَادِهِ رَاوٍ مَتْرُوكٌ
وَأَصْلُ اَلْقِصَّةِ فِي "اَلصَّحِيحِ" مِنْ حَدِيثِ أَبِي أُسَيْدٍ اَلسَّاعِدِيِّ
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “’Amrah bint Al-Jawn alijilinda dhidi ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) wakati alipoingia kwake (siku aliyomuoa). Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Kwa hakika umejilinda kwa kinga. Akamtaliki na akamuamrisha Usaamah ampe (mwanamke yule) nguo tatu.” [Imetolewa na Ibn Maajah na katika Isnaad yake kuna mpokezi anayeachwa. Asili ya kisa chenyewe kimo katika Swahiyh Al-Bukhaariy kutoka katika Hadiyth ya Abuu Usayd As-Saa’idiy]
[1] Huyu ni Mama wa Waumini Swafiyyah bint Huyai bin Al-Akhtwab, ni kutoka katika kizazi cha Nabiy Haaruwn. Mwanzoni alikuwa ameolewa na Kinaanah bin Abdil-Huqaiq ambaye aliuwawa katika vita vya Khaybar. Swafiyyah alitekwa, kisha Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimchagua kuwa mke wake na akasilimu. Aliachwa huru na uhuru wake ndiyo iliyokuwa mahari yake. Alifariki mwaka 50 Hijriyyah na alizikwa katika makaburi ya Baqi’
[2] Hii ina maana mahari inaweza kuwa kitu kisichokuwa fedha.
[3] Huyu ni Abuu Salamah bin ‘Abdir-Rahmaan bin ‘Awf Az-Zuhri Al-Qurayshiy. Huyu ni mmoja katika Mafuqahaa saba wakubwa katika mji wa Madiynah na ni miongoni mwa Taabii’ wakubwa. Ni madhubuti na amepokea Hadiyth nyingi ambazo alizisikia kutoka katika makundi mbalimbali ya Maswahaba na kutoka kwa waliopokea kutoka kwake. Alifariki mwaka 94 au 104 katika mapokezi mengine akiwa na umri wa miaka 70.
[4] Hakuna kiwango maalumu cha mahari katika Shariy’ah, hata hivyo kuifanya ndogo zaidi kunapendeza, ili kuifanya ndoa kuwa ni nyepesi kwa watu wengi.
[5] Ni deraya iliyotengenezwa na watu wa kabila la Al-Hutwamah, walikuwa mahodari wa kutengeneza maderaya ya kivita. Hadiyth hii ni dalili kuwa bwana arusi anatakiwa ampe mkewe kitu kabla ya kumuingilia.
[6] Hii ina maana kila kilichoamuliwa kabla ya ndoa ni mahari, na yote yanakuwa ni ya muolewa. Ikiwa zawadi hiyo ni ya fedha, dhahabu, nguo, ardhi, nyumba au kitu kingine chochote, yeye ndiye mmiliki kamili wa kitu hicho. Ikiwa kuna kitu chochote watakachopewa jamaa za binti baada ya kuolewa kwake, hilo halitazingatiwa kuwa ni mahari, na si milki ya binti. Ni zawadi aliyopewa mtu tu.
[7] Huyu ni ‘Alqamah bin Qays Abu Shibl bin Maalik katika kabila la Banu Bakr bin An-Nakha, amepokea Hadiyth nyingi kutoka kwa ‘Umar na Ibn Mas-‘uwd. Alikuwa ni Taabi’ mkubwa, alikuwa maarufu kwa Hadiyth ya Abdullaah bin Mas‘uwd na kuwa na usuluba naye, alikuwa ni mjomba wa Al-Aswad bin An-Nakahi alifariki mwaka 61 Hijriyyah.
[8] Jina hili la Birwa’ lina ikhtilafu kwa Wanazuoni wa lugha ambao wao humuita Barwa’ na Wanazuoni wa Hadiyth humuita Birwa’
[9] Sawiyq ni unga wa mtama au wa mahindi au wa shayiri uliokaangwa.
[10] Huyu ni Abuu ‘Imraan ‘Abdillaah bin ‘Aamir bin Rabiy’ah Al-Anzi. Alikuwa ni mwenye umri wa miaka minne au mitano pindi Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipofariki. Alifariki mwaka wa 85 Hijriyyah.
[11] Tazama Hadiyth ya 832.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)
20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh YAFUATAYO NI MAJINA YA MASWAHABA WANAWAKE (RADHI ZA ALLAAH...
-
Dalili 18 zinazoashiria una ujauzito wa mtoto wa kiume Awali ya yote nitoe pongezi kwa mama K na Baba K wote popote walipo kwa kazi nzuri ...
-
Assallaaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Naam, Ndugu zangu katika Imaani, Siku chache zimebaki kwa ajili ya Vijana wetu wanaosoma Elim...