Imefasiriwa na: Naaswir Haamid
Ndani ya makala hii, tutajaribu kusafisha masuala yanayoeleweka vibaya ambayo yamekithiri mno kuhusu Uislamu. Kabla ya kurukia kwenye orodha ya masuala hayo moja kwa moja, ni muhimu kueleza kwa ufupi kuhusu msingi mzuri wa chanzo cha Uislamu.
Uislamu ni jina la njia ya maisha ambayo Muumba Anatuhitaji tuifuate. Tunaepuka jina la dini kwa sababu ndani ya jamii nyingi zisizo kuwa za Kiislamu, kuna mgawanyo wa “dini na taifa”. Mgawanyo huu hautambuliki hata kidogo ndani ya Uislamu: Muumba Anashughulika zaidi kwa yale yote tunayoyafanya, ikiwemo siasa, jamii, uchumi, na nyanja nyenginezo za jamii yetu. Hivyo, Uislamu ni njia kamilifu ya maisha.
Chanzo cha Uislamu ni Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), Muumba wa kila kitu vinavyotambulika na visivyotambulika kwetu. Yeye ni Mmoja, na Asiyefanana na kitu. Allaah Ametufundisha kuhusu Uislamu kwa njia mbili: Qur-aan na Sunnah. Zote mbili; Qur-aan na Sunnah zilifikishwa kwetu, binaadamu, kupitia kwa Mtume wa Allaah: Muhammad bin Abdillaah, (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Mtume wa Allaah hakuwa zaidi na sio pungufu kuliko Mtume aliye na mwisho wa Muumba Asiye na mwisho.
Qur-aan ni kitabu chenye Neno hasa la Allaah. Ilikabidhiwa kutoka kwa Allaah kwa malaika Wake (Jibriyl), na kutoka kwa Malaika huyo kwa Mtume wa Allaah aliyeifikisha kwetu. Qur-aan inagusa mada pana za aina tofauti, zikiwemo ushahidi wa kushinikiza dai lake la kuwa ni Neno la Muumba, simulizi za vizazi vya mwanzo, kanuni ambazo mwanaadamu anatakiwa kuzifuata, na habari kuhusu Siku ya mwisho. Qur-aan inaonyesha kwamba inalindwa kubadilika na yeyote mwengine isipokuwa Allaah, na hili linathibitishwa kwa miaka yake 1400 ya kumbukumbu. Nakala za mwanzo na za mwisho zipo sawa sawa.
Sunnah ni msamiati unaotumika kueleza namna Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyoishi maisha yake. Maisha ya Mtume ni mfano kwa Waislamu wote, au wale waliokubali kuufuata Uislamu. Chochote alichofanya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kuzungumza au alichokikubali, ni chanzo cha Uislamu kama namna ilivyo kwa Qur-aan. Madaraka ya Mtume hayachupi mpaka: maisha yake yalimilikiwa na kile Muumba Alichokitaka, na Mtume hakuongeza au kupunguza kwenye Uislamu kwa yale matakwa yake binafsi. Maisha yake yalikuwa kama vile mkewe alivyomuita: “Qur-aan inayotembea”.
Qur-aan na Sunnah ndio njia mbili pekee ambazo Allaah Ametufundisha moja kwa moja kuhusu Uislamu. Hili linatupeleka kwenye kanuni ya upambanuzi lakini iliyo nyepesi:
Kama mwanamme au mwanamke atajihusisha kwenye imani au tendo ambalo linapingana wazi wazi na Qur-aan au Sunnah, basi imani au tendo hilo haliwezi kutambulika kuwa ni la ‘Kiislamu’.
Kanuni hii inatumika ikiwa ama mwanamme au mwanamke ni Muislamu au asiye Muislamu. Hivyo, hatuwezi kufananisha Uislamu na Waislamu. Uislamu ni njia ya maisha; Waislamu ni watu wanaodai kufuata njia hiyo ya maisha. Muislamu huenda akadai kufuata Uislamu, lakini akawa mkosa. Kwa mnasaba wa masuala yanayoeleweka vibaya, tunaweza kuielezea tena kanuni hiyo hapo juu kwa njia tofauti kidogo:
Baadhi ya masuala yanayoeleweka vibaya kuhusu Uislamu hakika yametokana na imani zisizo sahihi na matendo ya Waislamu, na mengine hakika yametokana na athari ya kukosa elimu na uongo unaorudiwa kila mara 'stereotype' na wasiokuwa Waislamu.
Masuala tofauti yanayoeleweka vibaya yanaorodheshwa chini. Badala ya kutaja masuala hayo kwa wepesi wa namna yalivyo wenyewe, pia tumehusisha ndani yake sababu za kwanini watu mara nyengine wanalichukua suala linaloeleweka vibaya. Hivyo, kila ingizo ndani ya orodha inapewa mtindo ufuatao:
<Maelezo ya Suala Linaloeleweka Vibaya> kwa sababu:
· <hoja 1>
· <hoja 2>
· n.k.
Baada ya kila suala linaloeleweka vibaya na sababu zake zinazoyumkinika, tunaonesha kwa ufupi kwa nini suala hilo ni la uongo kwa kuonesha kwamba yawezekana kuwa ni moja au zaidi ya mambo matatu yafuatayo:
1. Hoja ni ya uongo
2. Hoja haileti mantiki inayopelekea kueleweka vibaya
3. Habari ndogo ndogo zilizo kuu zimedharauliwa
Majibu yetu kwa masuala yanayoeleweka vibaya yamepatikana kutoka Qur-aan na Sunnah. Upatikanaji mwengine wowote hauna mnasaba: Uislamu ni njia ya maisha, ni msingi uliojikita kisawasawa kwenye kujiridhisha kiuwanazuoni, kujiridhisha huko kunaegemezwa katika maarifa.
Suala Nambari 1 Linaloeleweka Vibaya
Uislamu ni ‘dini ya amani’ kwa sababu
· Neno la Kiarabu la Islaam linatokana na neno la Kiarabu ‘As-Salaam’ lenye maana ya amani.
JIBU
Inawezekana kukutana na mshangao kufikiria kwamba suala hili ni miongoni mwa yanayoeleweka vibaya, lakini ukweli ni hivyo. Mzizi wa neno Islaam ni “as-silm” lenye maana ya “kunyenyekea” au “kujisalimisha”. Linaeleweka kuwa na maana ya “kunyenyekea kwa Allaah”. Ingawa kwa azma kuu yeyote iliyosababisha Waislamu walio wengi kudai kwamba Uislamu kimsingi unatokana na amani, hili sio kweli. Allaah Anasema ndani ya Qur-aan (iliyotafsiriwa):
[2:136]
Mzizi unaofuata baada ya hapo unawezekana kuwa ni “As-Salaam” (amani), hata hivyo maandiko ya Qur-aan yanadhihirisha wazi kwamba Allaah Ameshaazimia kwa uwazi shabaha ya maisha haya kuwa ni unyenyekevu Kwake Yeye. Hili linatufanya kuwa na unyenyekevu Kwake wakati wowote, ikiwa ni vipindi vya amani, vita, urahisi au ugumu.
Itaendelea in shaa Allaah...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni