Translate

Ijumaa, 1 Novemba 2019

Hiswnul-Muslim: Fadhila Za Kumdhukuru Allaah

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُوا لِي وَلَا تَكْفُرُونِ ﴿١٥٢﴾
((Basi nidhukuruni na Mimi Nitakukumbukeni; na nishukuruni wala msinikufuru.))[1]  



 Na Anasema:
 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّـهَ ذِكْرًا كَثِيرًا ﴿٤١﴾ وَسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا ﴿٤٢﴾
((Enyi mlioamini! Mdhukuruni Allaah kwa dhikri ya wingi. Na Msabbihini asubuhi na jioni))[2]   


Na Anasema:
   وَالذَّاكِرِينَ اللَّـهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا ﴿٣٥﴾
((na Wanaume wanaomdhukuru Allaah kwa wingi na Wanawake wanaomdhukuru Allaah (kwa wingi); Allaah Amewaandalia maghfirah na ujira adhimu))[3]  


Na Anasema:

 وَاذْكُر‌ رَّبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعًا وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ‌ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ الْغَافِلِينَ ﴿٢٠٥﴾  
((Na mdhukuru Rabb wako katika nafsi yako kwa unyenyekevu na kwa khofu na si kwa jahara (kunyanyua sauti) katika kauli asubuhi na jioni; na wala usiwe miongoni mwa walioghafilika.))[4] 


 وقال صلى الله عليه وسلم: ((مَثَـــلُ الـــذي يَـــذكُرُ ربَّـــهُ وَالـــذي لا يـــذكُرُهُ، مَثَـــل الحـــيِّ والمَيِّــتِ))
Na amesema  (صلى الله عليه وسلم): ((Mfano wa anayemdhukuru Rabb wake na asiyemdhukuru ni mfano wa aliye hai na maiti))[5]


وقال صلى الله عليه وسلم: ((أَلَا أُنَبِّئُكُمْ بِخَيْرِ أَعْمَالِكُمْ وَأَزْكَاهَا عِنْدَ مَلِيكِكُمْ وَأَرْفَعِهَا فِي دَرَجَاتِكُمْ وَخَيْرٌ لَكُمْ مِنْ إِنْفَاقِ الذَّهَبِ وَالْوَرِقِ وَخَيْرٌ لَكُمْ مِنْ أَنْ تَلْقَوْا عَدُوَّكُمْ فَتَضْرِبُوا أَعْنَاقَهُمْ وَيَضْرِبُوا أَعْنَاقَكُمْ؟)) قَالُوابَلَىقَالَ: ((ذِكْرُ اللَّهِ تَعَالَى))
Na amesema (صلى الله عليه وسلم): ((Hivi niwaambieni khabari ya matendo yenu bora, na ambayo ni masafi mno, mbele ya Rabb wenu, na ambayo ni ya juu mno katika daraja zenu, na ambayo ni bora kwenu kuliko kutoa dhahabu na fedha, na ambayo ni bora kuliko kukutana na adui zenu, mkawapiga shingo zao, nao wakakupigeni shingo zenu?)) Wakasema: [Maswahaba]: Ndio. Akasema: ((Ni kumdhukuru Allaah Ta’aalaa))[6]      


وقال صلى الله عليه وسلم: ((يَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى أَنَا عِنْدَ ظَنِّ عَبْدِي بِي وَأَنَا مَعَهُ إِذَا ذَكَرَنِي فَإِنْ ذَكَرَنِي فِي نَفْسِهِ ذَكَرْتُهُ فِي نَفْسِي وَإِنْ ذَكَرَنِي فِي مَلَإٍ ذَكَرْتُهُ فِي مَلَإٍ خَيْرٍ مِنْهُمْ وَإِنْ تَقَرَّبَ إِلَيَّ بِشِبْرٍ تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ ذِرَاعًا وَإِنْ تَقَرَّبَ إِلَيَّ ذِرَاعًا تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ بَاعًا وَإِنْ أَتَانِي يَمْشِي أَتَيْتُهُ هَرْوَلَةً)) البخاري، مسلم، الترمذي و ابن ماجه
Na amesema (صلى الله عليه وسلم): ((Allaah Ta’aalaa Anasema: Mimi ni vile mja Wangu anavyonidhania. Niko pamoja naye anaponikumbuka. Anaponikumbuka katika nafsi yake, Nitamkumbuka katika nafsi Yangu, anapokumbuka katika hadhara, Nitamkumbuka katika hadhara bora zaidi. Na anaponikaribia shibiri Ninamkaribia dhiraa; anaponikaribia dhiraa, Ninamkaribia pima, anaponijia kwa mwendo (wa kawaida) ninamwendea mbio))[7] 


وعن عبد الله بن بسرٍ رضي الله عنهُ أنّ رجُلًا قاليَا رَسُولَ اللهِ، إِنَّ شَرَائِعَ الإِسْلَامِ قَدْ كَثُرَتْ عَلَيَّ، فَأَخْبِرْنِي بِشَيْءٍ أَتَشَبَّثُ بِهِ. قَالَ: ((لَا يَزَالُ لِسَانُكَ رَطْبًا مِنْ ذِكْرِ الله))  
Imepokewa kutoka kwa kwa ‘Abdullaah Bin Busr  (رضي الله عنه)kwamba mtu mmoja alisema: Ee Rasuli wa Allaah! ‘Ibaadah za Dini zimekuwa nyingi kwangu, basi nieleze kitu ambacho nitaweza kudumu nacho. Akasema: ((Ulimi wako utaendelea kuwa laini kwa kumdhukuru Allaah))[8] 


وقال صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ قَرَأَ حَرْفًا مِنْ كِتَابِ اللَّهِ فَلَهُ بِهِ حَسَنَةٌ وَالْحَسَنَةُ بِعَشْرِ أَمْثَالِهَا لَا أَقُولُ الم حَرْفٌ وَلَكِنْ أَلِفٌ حَرْفٌ وَلَامٌ حَرْفٌ وَمِيمٌ حَرْفٌ))
Na amesema (صلى الله عليه وسلم): ((Anayesoma herufi moja katika kitabu cha Allaah basi anapata thawabu za jema moja na jema ni kwa mema kumi, sisemi kuwa ‘Alif Laam Miym’ ni herufi moja lakini ni kwamba ‘Alif’ peke yake ni herufi moja, na ‘Laam’ ni herufi, na ‘Miym’ ni herufi))[9]


وَعَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ قَالَ خَرَجَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَنَحْنُ فِي الصُّفَّةِ فَقَالَ: ((أَيُّكُمْ يُحِبُّ أَنْ يَغْدُوَ كُلَّ يَوْمٍ إِلَى بُطْحَانَ أَوْ إِلَى الْعَقِيقِ فَيَأْتِيَ مِنْهُ بِنَاقَتَيْنِ كَوْمَاوَيْنِ فِي غَيْرِ إِثْمٍ وَلَا قَطْعِ رَحِمٍ؟)) فَقُلْنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ نُحِبُّ ذَلِكَ قَالَ: ((أَفَلَا يَغْدُو أَحَدُكُمْ إِلَى الْمَسْجِدِ فَيَعْلَمُ أَوْ يَقْرَأُ آيَتَيْنِ مِنْ كِتَابِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ خَيْرٌ لَهُ مِنْ نَاقَتَيْنِ وَثَلَاثٌ خَيْرٌ لَهُ مِنْ ثَلَاثٍ وَأَرْبَعٌ خَيْرٌ لَهُ مِنْ أَرْبَعٍ وَمِنْ أَعْدَادِهِنَّ مِنْ الْإِبِلِ))
Na imepokewa kutoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir(رضي الله عنه  ambaye amesema, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) alitujia tukiwa katika Swuffah akauliza: ((Kuna yeyote miongoni mwenu anayetaka kwenda  soko la Butw-haan au Al-'Aqiyq na akapata humo ngamia wawili (wa thamani kabisa wa kike) bila ya kutenda dhambi au kukata undugu?)) Tukajibu kwamba sote tunapenda kufanya na kupata hivyo. Kisha akasema: ((Basi aende mmoja wenu Msikitini akajifunze au asome Aayah mbili katika kitabu cha Allaah عزوجل basi akifanya hivyo ni bora kuliko ngamia (wa thamani kabisa wa kike).  Na Aayah tatu ni bora kuliko ngamia watatu, na Aayah nne ni bora kuliko ngamia wanne, na mfano wa hivyo hivyo wa Aayah kwa ngamia))[10]


وقال صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ قَعَدَ مَقْعَدًا لَمْ يَذْكُرِ اللَّهَ فِيهِ، كَانَتْ عَلَيْهِ مِنَ اللَّهِ تِرَةٌوَمَنِ اضْطَجَعَ مَضْجَعًا لَمْ يَذْكُرِ اللَّهَ فِيهِ ، كَانَتْ عَلَيْهِ مِنَ اللَّهِ تِرَةٌ))
Na amesema (صلى الله عليه وسلم): ((Anayekaa kikao chochote kile asimdhukuru Allaah katika kikao hicho basi ana dhambi kutoka kwa Allaah, na anayelala sehemu yeyote ile kisha asimdhukuru Allaah wakati wakuinuka sehemu hiyo basi ana dhambi kwa Allaah))[11] 


وقال صلى الله عليه وسلم: ((مَا جَلَسَ قَوْمٌ مَجْلِسًا لَمْ يَذْكُرُوا اللَّهَ فِيهِ وَلَمْ يُصَلُّوا عَلَى نَبِيِّهِمْ إِلَّا كَانَ عَلَيْهِمْ تِرَةً فَإِنْ شَاءَ عَذَّبَهُمْ وَإِنْ شَاءَ غَفَرَ لَهُمْ))  
Na amesema (صلى الله عليه وسلم): ((Hapana watu wowote wale, wanaokaa kikao kisha wasimdhukuru Allaah humo, wala wasimswalie Nabiy wao ila watakuwa wana dhambi. Akipenda Atawaadhibu na Akipenda Atawaghufuria))[12]  

وقال صلى الله عليه وسلم: ((مَا مِنْ قَوْمٍ يَقُومُونَ مِنْ مَجْلِسٍ لَا يَذْكُرُونَ اللَّهَ فِيهِ إِلَّا قَامُوا عَنْ مِثْلِ جِيفَةِ حِمَارٍ وَكَانَ لَهُمْ حَسْرَةً))
Na amesema  (صلى الله عليه وسلم): ((Hapana watu wowote wale wanaosimama katika kikao walichokaa, kisha wasimdhukuru Allaah ila watakuwa wanasimama kama mzoga wa punda, na watakuja juta [kwa kutokumdhukuru Allaah]))[13]





[1] Al-Baqarah (2:152).
[2] Al-Ahzaab (33:41-42).
[3] Al-Ahzaab (33:35).
[4] Al-A’raaf (7:205).
[5] Hadiyth ya Abu Muwsaa Al-Ash’ariyy(رضي الله عنه)   -Al-Bukhaariy  pamoja Al-Fat-h (11/208) au namba [6407] na Muslim kwa tamshi kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:  

((مَثَلُ البَيْتِ الذي يُذكَرُ اللهُ فيه، والبيت الذي لا يذكرُ الله فيه مَثَلُ الحيِّ والميِّت))
((Mfano wa nyumba ambayo Allaah Anatajwa na ambayo hatajwi humo ni kama aliye hai na maiti)) (1-539) [779].
[6] Hadiyth ya ‘Abu Dardaa ‘Uwaymir bin ‘Aamir (رضي الله عنه) - At-Tirmidhiy (5/459) [3377], Ibn Maajah (2/1246) [3790], na angalia Swahiyh Ibn Maajah (2/316) na Swahiyh At-Tirmidhiy (3/139).
[7] Hadiyth ya Abu Hurayrah(رضي الله عنه)   - Al-Bukhaariy (8/171) [7405], Muslim (4/2061) [2675] na tamshi la Al-Bukhaariy.
[8] At-Tirmidhiy (5/458) [3375], Ibn Maajah (2/1246) [3793], na taz. Swahiyh At-Tirmidhiy (3/139) na Swahiyh Ibn Maajah (2/317).
[9] Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd - (رضي الله عنه - At-Tirmidhiy (5/175) [2910] na taz. Swahiyh At-Tirmidhiy (3/9) na Swahiyh Al-Jaami’ Asw-Swaghiyr (5/340) [6469].
[10] Muslim (1/553) [803].
[11] Hadiyth ya Abu Hurayrah(رضي الله عنه)   - Abu Daawuwd (4/264) [4856] na wengineo na taz. Swahiyh Al-Jaami’ (5/342) [6477].
[12] Hadiyth ya Abu Hurayrah(رضي الله عنه)   - At-Tirmidhiy [3380] na taz. Swahiyh At-Tirmidhiy (3/140).
[13] Hadiyth ya Abu Hurayrah(رضي الله عنه)   - Abu Daawuwd (4/264) [4855], Ahmad (2/389) na taz Swahiyh Al-Jaami’ (5/176) [5750].


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...