Translate

Ijumaa, 1 Novemba 2019

009-Asbaabun-Nuzuwl: At-Tawbah: Aayah 34 - 35

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

At-Tawbah: Aayah 34 - 35

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ كَثِيرًا مِّنَ الْأَحْبَارِ وَالرُّهْبَانِ لَيَأْكُلُونَ أَمْوَالَ النَّاسِ بِالْبَاطِلِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۗ وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣٤﴾

Enyi walioamini! Hakika wengi katika Wanachuoni Marabai wa dini (zao) na Wamonaki wanakula mali za watu kwa batili, na wanazuia njia ya Allaah. Na wale wanaorundika dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika njia ya Allaah, basi wabashirie adhabu iumizayo. 

 

 

يَوْمَ يُحْمَىٰ عَلَيْهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكْوَىٰ بِهَا جِبَاهُهُمْ وَجُنُوبُهُمْ وَظُهُورُهُمْ ۖ هَـٰذَا مَا كَنَزْتُمْ لِأَنفُسِكُمْ فَذُوقُوا مَا كُنتُمْ تَكْنِزُونَ﴿٣٥﴾

Siku zitakapopashwa katika Jahannam, na kwazo vikachomwa moto vipaji vyao, na mbavu zao, na migongo yao (wakiambiwa): Haya ndiyo mliyoyarundika kwa ajili ya nafsi zenu. Basi onjeni yale mliyokuwa mkiyarundika. [At-Tawbah: 34-35]

 

 

حَدَّثَنَا عَلِيٌّ، سَمِعَ هُشَيْمًا، أَخْبَرَنَا حُصَيْنٌ، عَنْ زَيْدِ بْنِ وَهْبٍ، قَالَ مَرَرْتُ بِالرَّبَذَةِ فَإِذَا أَنَا بِأَبِي، ذَرٍّ رضى الله عنه فَقُلْتُ لَهُ، مَا أَنْزَلَكَ مَنْزِلَكَ هَذَا، قَالَ:  كُنْتُ بِالشَّأْمِ، فَاخْتَلَفْتُ أَنَا وَمُعَاوِيَةُ فِي: ((الَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلاَ يُنْفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ))‏.‏ قَالَ مُعَاوِيَةُ: نَزَلَتْ فِي أَهْلِ الْكِتَابِ‏،‏ فَقُلْتُ: نَزَلَتْ فِينَا وَفِيهِمْ‏، فَكَانَ بَيْنِي وَبَيْنَهُ فِي ذَاكَ، وَكَتَبَ إِلَى عُثْمَانَ رضى الله عنه يَشْكُونِي، فَكَتَبَ إِلَىَّ عُثْمَانُ أَنِ اقْدَمِ الْمَدِينَةَ‏‏، فَقَدِمْتُهَا، فَكَثُرَ عَلَىَّ النَّاسُ حَتَّى كَأَنَّهُمْ لَمْ يَرَوْنِي قَبْلَ ذَلِكَ، فَذَكَرْتُ ذَاكَ لِعُثْمَانَ فَقَالَ لِي: إِنْ شِئْتَ تَنَحَّيْتَ، فَكُنْتَ قَرِيبًا‏ فَذَاكَ الَّذِي أَنْزَلَنِي هَذَا الْمَنْزِلَ، وَلَوْ أَمَّرُوا عَلَىَّ حَبَشِيًّا لَسَمِعْتُ وَأَطَعْتُ‏.‏

 

Ametuhadithia ‘Aliy, amemsikia Hushaym, ametusimulia Huswayn toka kwa Zayd bin Wahb amesema: Nilipita Ar-Rabadhah na mara ghafla nikamwona Abuu Dharr (رضي الله عنه)  Nikamuuliza: Nini kimekuleta kuja kuishi huku? Akasema: Nilikuwa Sham, nikazozana mimi na Mu’aawiyah kuhusiana

((وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلاَ يُنْفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ‏))‏

((Na wale wanaorundika dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika njia ya Allaah)). Mu’aawiyah akasema: Imeteremka kwa Ahlul-Kitaab tu. Nikasema: Imeteremka kwetu na kwao pia. Ukakasi ukawepo kati yangu na yeye katika hilo. Akamwandikia barua ‘Uthmaan (رضي الله عنه)  akimlalamikia kuhusu mimi. Naye ‘Uthmaan akaniandikia na kuniamuru niende Madiynah. Nikaenda, na watu wakanizonga (kuniuliza sababu ya kuondoka Sham) kana kwamba hawajawahi kuniona kamwe. Nikamweleza ‘Uthmaan hilo naye akaniambia: Ukitaka achana (na rai yako) uwe karibu. Basi hili ndilo lililonifikisha kuishi hapa, na lau watampa madaraka Mhabeshi (mtumwa) awe kiongozi wangu, basi nitamsikiliza na kumtii. [Al-Bukhaariy]

 

Na pia,

 

قَالَ أَحْمَدُ بْنُ شَبِيبِ بْنِ سَعِيدٍ حَدَّثَنَا أَبِي، عَنْ يُونُسَ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ خَالِدِ بْنِ أَسْلَمَ، قَالَ خَرَجْنَا مَعَ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ ـ رضى الله عنهما ـ فَقَالَ أَعْرَابِيٌّ أَخْبِرْنِي قَوْلَ اللَّهِ: ((وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلاَ يُنْفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ‏))‏ قَالَ ابْنُ عُمَرَ ـ رضى الله عنهما ـ مَنْ كَنَزَهَا فَلَمْ يُؤَدِّ زَكَاتَهَا فَوَيْلٌ لَهُ، إِنَّمَا كَانَ هَذَا قَبْلَ أَنْ تُنْزَلَ الزَّكَاةُ فَلَمَّا أُنْزِلَتْ جَعَلَهَا اللَّهُ طُهْرًا لِلأَمْوَالِ‏.‏

Ahmad bin Shabiyb bin Sa’iyd amesema, baba yangu ametuhadithia toka kwa Yuwnus toka kwa Ibn Shihaab toka kwa Khaalid bin Aslam. Amesema: Tulitoka pamoja na ‘Abdullaah bin ‘Umar (رضي الله عنهما) na bedui mmoja akasema: Nielezee Kauli ya Allaah:

((وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلاَ يُنْفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ‏))‏

((Na wale wanaorundika dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika njia ya Allaah))

 

Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما)  akasema: Mwenye kuzirundika na asitoe Zakaah yake, basi ole wake na adhabu kali. Na hili lilikuwa kabla ya kufaradhishwa Zakaah, na ilipofaradhishwa, Allaah Ameifanya kuwa utakaso kwa mali.  [Al-Bukhaari]

 

 

Na pia,

 

حَدَّثَنَا قُتَيْبَةُ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ حُصَيْنٍ، عَنْ زَيْدِ بْنِ وَهْبٍ، قَالَ مَرَرْتُ عَلَى أَبِي ذَرٍّ بِالرَّبَذَةِ فَقُلْتُ:  مَا أَنْزَلَكَ بِهَذِهِ الأَرْضِ؟ قَالَ:  كُنَّا بِالشَّأْمِ فَقَرَأْتُ: ((‏وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلاَ يُنْفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَبَشِّرْهُمْ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ‏))  قَالَ مُعَاوِيَةُ مَا هَذِهِ فِينَا، مَا هَذِهِ إِلاَّ فِي أَهْلِ الْكِتَابِ‏.‏ قَالَ قُلْتُ إِنَّهَا لَفِينَا وَفِيهِمْ‏.‏

Ametuhadithia Qutaybah bin Sa’iyd, ametuhadithia Jariyr toka kwa Huswayn toka kwa Zayd bin Wahab amesema: Nilimpitia Abuu Dharr huko Ar-Rabadhah nikamuuliza: Kitu gani kimekuleta ardhi hii? Akasema: Tulikuwa Sham, nikasoma:

 

‏‏ وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣٤﴾

Enyi walioamini! Hakika wengi katika Wanachuoni Marabai wa dini (zao) na Wamonaki wanakula mali za watu kwa batili, na wanazuia njia ya Allaah. Na wale wanaorundika dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika njia ya Allaah, basi wabashirie adhabu iumizayo. 

Na Mu’aawiyah akasema: Hili halituhusu sisi, hili haliwahusu wengine isipokuwa Ahlul-Kitaab. Akasema: Nikasema hakika hili bila shaka linatuhusu sisi na wao pia.  [Al-Bukhaariy]

 

 

 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...