Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
39-Amepewa Al-Kawthar (Mto Uliko Jannah) Ulio Na Kheri Nyingi
عَنْ أَنَسٍ (رضي الله عنه) : ((إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ)) أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: ((هُوَ نَهْرٌ فِي الْجَنَّةِ))
Anas (رضي الله عنه) amehadithia (kuhusu kauli yake Allaah): “Hakika Sisi Tumekupa Al-Kawthar”; kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Huo ni Mto katika Jannah.” [Al-Bukhaariy, At-Tirmidhiy]
عَنْ أَنَسٍ، قَالَ بَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ذَاتَ يَوْمٍ بَيْنَ أَظْهُرِنَا إِذْ أَغْفَى إِغْفَاءَةً ثُمَّ رَفَعَ رَأْسَهُ مُتَبَسِّمًا فَقُلْنَا مَا أَضْحَكَكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ قَالَ: " أُنْزِلَتْ عَلَىَّ آنِفًا سُورَةٌ " . فَقَرَأَ: ((بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ * إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ * فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ * إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الأَبْتَرُ)) . ثُمَّ قَالَ: "أَتَدْرُونَ مَا الْكَوْثَرُ؟" فَقُلْنَا اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ . قَالَ: "فَإِنَّهُ نَهْرٌ وَعَدَنِيهِ رَبِّي عَزَّ وَجَلَّ عَلَيْهِ خَيْرٌ كَثِيرٌ هُوَ حَوْضٌ تَرِدُ عَلَيْهِ أُمَّتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ آنِيَتُهُ عَدَدُ النُّجُومِ فَيُخْتَلَجُ الْعَبْدُ مِنْهُمْ فَأَقُولُ: رَبِّ إِنَّهُ مِنْ أُمَّتِي. فَيَقُولُ مَا تَدْرِي مَا أَحْدَثَتْ بَعْدَكَ " . زَادَ ابْنُ حُجْرٍ فِي حَدِيثِهِ بَيْنَ أَظْهُرِنَا فِي الْمَسْجِدِ . وَقَالَ "مَا أَحْدَثَ بَعْدَكَ"
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه) ambaye amesema: Siku moja Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa amekaa na sisi usingizi ukamchukua. Kisha akainua kichwa chake akiwa anatabasamu. Tukasema: Nini kilichokuchekesha ee Rasuli wa Allaah? Akasema: “Nimeteremshiwa Suwrah sasa hivi! Akasoma:
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ ﴿١﴾
Hakika Sisi Tumekupa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Al-Kawthar (Mto katika Jannah).
فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ ﴿٢﴾
Basi swali kwa ajili ya Rabb wako na chinja kwa ajili Yake.
إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الْأَبْتَرُ ﴿٣﴾
Hakika mbaya wako, yeye ndiye atakayekatiliwa mbali (kizazi na kila kheri) [Al-Kawthar: 108]
Kisha akasema: “Je mnajua nini Al-Kawthar?” Tukasema: Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi. Akasema: “Huo ni mto Ameniahidi Rabb wangu Allaah (عزَّ وجلّ) nao una kheri nyingi; ni hodhi na Ummah wangu wataufikia Siku ya Qiyaamah. Bilauri zake ni sawa na idadi ya nyota. (Baadhi ya) waja watafukuzwa waondoke. Hapo nitasema: Ee Rabb wangu hakika hao ni katika Ummah wangu! Atasema (Allaah): Hujui waliyoyazusha (katika Dini) baada yako.”
Ibn Hujri amezidisha katika Hadiyth yake: “Alikuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameketi pamoja nasi Msikitini. Na (Allaah) Akasema: “Hujui walichokizusha baada yako!” [Swahiyh Muslim]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni