Translate

Alhamisi, 14 Novemba 2019

39-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyenyekevu Wake: Akichukia Kusimamiwa

 

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

39-Unyenyekevu Wake Akichukia Kusimamiwa

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ ، قَالَ لَمْ يَكُنْ شَخْصٌ أَحَبَّ إِلَيْهِمْ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ وَكَانُوا إِذَا رَأَوْهُ لَمْ يَقُومُوا لِمَا يَعْلَمُونَ مِنْ كَرَاهِيَتِهِ لِذَلِكَ ‏.‏ قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ غَرِيبٌ مِنْ هَذَا الْوَجْهِ

Kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه) amesema:  “Hakuweko mtu aliyekuwa kipenzi zaidi kwao kuliko Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).” Akasema:  Lakini hawakuwa wakimsimamia pindi wanapomuona kwa sababu walijua jinsi gani alivyokuwa akichukia hivyo (kusimamiwa). [Adab Al-Mufrad, At-Tirmidhiy, ameisahihisha Al-Albaaniy – Swahiyh At-Tirmidhiy (2754),

 

Shaykhul-Islaam ibn Taymiyyah  (حمه الله)  amesema:  “Maswahaba (رضي الله عنهم) hawakuwa wakimsimamia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa vile walijua kuchukiwa kwake hivyo, wala hawakuwa wakisimamiana wao kwa wao.” [Mukhtaswar Al-Fataawaa Al-Miswriyyah (2/26-27)]

 

Imaam Ibn Baaz (حمه الله) amesema:   “Maswaahaba walikuwa wanapokutana naye Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) walikuwa wakimwamkia kwa kumpa mikono na hawakuwa wakibusu mkono wake…” [Fataawaa Nuwr Alad-Darb ukanda 488)]

 

 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...