Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
38-Nabiy Pekee Aliyetakwa Afuate Mwongozo Na Vigezo Vya Manabii Wengineo
Allaah (سبحانه وتعالى) Alimuamrisha Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) afuate mwongozo na vigezo vya Manabii wengineo; jambo ambalo hakuna Nabiy mwengine aliyeamrishwa kufanya hivyo. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى) baada ya kuwataja Manabii kumi na nane katika Aayah zilizofuatana za Suwrah Al-An’aam:
وَتِلْكَ حُجَّتُنَا آتَيْنَاهَا إِبْرَاهِيمَ عَلَىٰ قَوْمِهِ ۚ نَرْفَعُ دَرَجَاتٍ مَّن نَّشَاءُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿٨٣﴾
Na hiyo ndio hoja Yetu Tuliyompa Ibraahiym juu ya watu wake. Tunampandisha cheo Tumtakaye. Hakika Rabb wako ni Mwenye hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.
وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۚ كُلًّا هَدَيْنَا ۚ وَنُوحًا هَدَيْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِ دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَارُونَ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٤﴾
Na Tukamtunukia Is-haaq, na Ya’quwb. Wote Tukawahidi. Na Nuwh Tulimhidi kabla. Na katika dhuria wake Daawuwd, na Sulaymaan, na Ayyuwb, na Yuwsuf, na Muwsaa, na Haaruwn. Na hivyo ndivyo Tulipavyo wafanyao ihsaan.
وَزَكَرِيَّا وَيَحْيَىٰ وَعِيسَىٰ وَإِلْيَاسَ ۖ كُلٌّ مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٨٥﴾
Na Zakariyyaa, na Yahyaa, na ‘Iysaa, na Ilyaas. Wote ni miongoni mwa Swalihina.
وَإِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطًا ۚ وَكُلًّا فَضَّلْنَا عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٨٦﴾
Na Ismaa’iyl, na Al-Yasa’a na Yuwnus, na Luwtw. Na wote Tuliwafadhilisha juu ya walimwengu.
وَمِنْ آبَائِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ وَإِخْوَانِهِمْ ۖ وَاجْتَبَيْنَاهُمْ وَهَدَيْنَاهُمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٨٧﴾
Na katika baba zao, na dhuriya wao, na ndugu zao. Na Tukawateua na Tukawaongoza kuelekea njia iliyonyooka.
ذَٰلِكَ هُدَى اللَّـهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚ وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٨﴾
Hiyo ndiyo hidaaya ya Allaah, kwa hiyo, Humwongoza Amtakaye kati ya waja Wake. Na kama wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda. [Al-An’aam: 83-88]
Na hii ni dalili ya kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Amemfadhilisha kuliko Manabii wengineo kama alivyosema Imaam As-Sa’dy (رحمه الله):
“Inamaanisha: Fuata nyuma ee Rasuli Mkarimu mwendo wa hawa Manabii waliokhitariwa, na fuata millah zao. Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akafuata vigezo vyao akaongoka kwa hidaaya ya Rusuli (wote) wa kabla yake, na akakusanya kila aina ya mazuri yao. Ikamkusanyikia kwake fadhila na khulqa zikawapita walimwengu wote. Akawa Sayyid wa Rusuli wote, na Imaam wa wenye kumcha Allaah, basi Swalaah za Allaah ziwe juu yake pamoja na Manabii wote wengineo. Na kutokana na hivyo, Maswahaba wakatoa dalili kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Rasuli mbora kabilsa kuliko wote. [Tafsiyr As-Sa’dy (Uk 263)]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni