SWALI LA KWANZA:
Bismillah rahmani rahim.
Namshukuru Allah Muumba wa ulimwengu kwa kunikubalia kujiunga na mtandao huu (Allhamdullillahi Rabill allamina)
Swali: Katika kusoma FisabililLaah Blog nimesoma kuwa "Ukila nyama ya Ngamia kama umetia "udhu" basi udhu unatenguka. Kwa nini
Nitafurahi sana ikiwa utanielezea na Hadith za maswahaba
Shukran. Allhamdullillahi Rabill allamina.
Nitafurahi sana ikiwa utanielezea na Hadith za maswahaba
Shukran. Allhamdullillahi Rabill allamina.
SWALI LA PILI:
Assalam Aalaykum: Allah Awabariki kwa jitihada zenu Amin.
Nina Swali kuhusu Ngamia. niliingia katika web hii nikatafuta katika sehemu ya kujifinza au namna ya kutia wudhuu. Nikaangalia Step baada ya Step. Mwisho Mukaweka Mambo yanayotengua Wudhuu. Na mukatoa mifano. Kama Kujamba. kwenda haja kubwa. Mkojo. Na kula Nyama ya ngamia. Sasa Naomba Hadith zinazoelezea kuhusu kutokwa na Wudhuu Unapokula Nyama ya Ngamia.
Niliingia vivile sehemu kusachi au kutafuta Mambo yanayotengua Udhu Mukaweka tu. Kama kwenda chooni. Kukojoa. Usingizi Mnono. kujamba. Nk. Lakini Hamjaweka Ngamia na hili ni moja wapo mambo yanotengua Udhu. Kwa hiyo nilikua Naomba tu Munifahamishe Kuhusu Huyu Ngamia Kwa ushahidi wa Hadithi kwa sababu watu wengi sana halijui Jambo hili.
JIBU
Wa Aleykum Sallaam WarahmatulLaah Wabarakatuh
AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Naam katika suala hilo zipo Hadiyth zinazozungumzia ambazo zipo wazi. Hadiyth zenyewe ni:
Jaabir bin Samurah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema kuwa alikuja mtu akamuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Je, tutawadhe kwa kula nyama ya mbuzi?” Akasema: “Ukitaka tawadha, na ukitaka usitawadhe”. Akauliza: “Je, tutawadhe kwa nyama ya ngamia (yaani kwa kula)?” Akasema: “Ndio, tawadheni kwa nyama ya ngamia” [Muslim na Ibn Maajah].
Imepokewa na Al-Baraa’ bin ‘Aazib (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Tawadheni kwa nyama ya ngamia, wala msitawadhe kwa nyama ya mbuzi” [Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah]
Hii ya kutawadha baada ya kula nyama ya ngamia ndio rai iliyo sahihi zaidi kwa kila hali. Kwa ajili hiyo amesema Imaam an-Nawawiy katika Sharh yake ya Swahiyh Muslim: “Na madhehebu haya ndio yenye dalili yenye nguvu zaidi japokuwa jamhuri ya ‘Ulamaa wanakwenda kinyume chake.”
Ama kuhusu nini hekima ya kutawadha baada ya kula nyama ya ngamia Hadiyth hazikutaja hilo. Kwa hiyo, Mjuzi wa hikma hiyo ni Allaah ('Azza wa Jalla) Peke Yake nasi tunahitajika tuwe ni wenye kufuata. Kwa kufanya hivyo ni dalili ya Iymaan nzuri ya Muislamu.
Na Allaah Anajua zaidi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni