Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
24-Ameruhusiwa Kuingiza Jannah Watu Sabiini Elfu Katika Ummah Wake
Hadiyth ifuatayo imethibitisha kwamba Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni Rasuli Pekee ambaye ataruhusiwa kuingiza watu sabiini elfu katika Ummah wake:
Hadiyth maarufu ya ‘Ukaashah kuhusu Ruqyah (kinga na tiba:
عَنْ حُصَيْنِ بْنِ عَبْدِ اَلرَّحْمَنِ قَالَ: كُنْتُ عِنْدَ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ فَقَالَ: أَيُّكُمْ رَأَى الْكَوْكَبَ اَلَّذِي اِنْقَضَّ الْبَارِحَةَ؟ فَقُلْتُ أَنَا. ثُمَّ قُلْتُ: أَمَّا إِنِّي لَمْ أَكُنْ فِي صَلاةٍ وَلَكِنِّي لُدِغْتُ. قَالَ: فَمَا صَنَعْتَ؟ قُلْتُ: اِرْتَقَيْتُ. قَالَ: فَمَا حَمَلكَ عَلَى ذَلِكَ؟ قُلْتُ: حَدِيثٌ حَدَّثَنَاهُ اَلشَّعْبِيُّ. قَالَ: وَمَا حَدَّثَكُمْ؟ قُلْتُ: حَدَّثَنَا عَنْ بُرَيْدَةَ بْنِ الْحُصَيْبِ أَنَّهُ قَالَ: لاَ رُقْيَةَ إِلاَّ مِنْ عَيْنٍ أَوْ حُمَةٍ. قَالَ: قَدْ أَحْسَنَ مَنِ اِنْتَهَى إِلَى مَا سَمِعَ. وَلَكِنْ حَدَّثَنَا اِبْنُ عَبَّاسٍ عَنْ اَلنَّبِيِّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) أَنَّهُ قَالَ: ((عُرِضَتْ عَلَيَّ الأُمَمُ فَرَأَيْتُ اَلنَّبِيَّ وَمَعَهُ اَلرَّهْطُ وَالنَّبِيَّ وَمَعَهُ اَلرَّجُلُ وَالرَّجُلاَنِ، وَالنَّبِيَّ وَلَيْسَ مَعَهُ أَحَدٌ، إِذْ رُفِعَ لِي سَوَادٌ عَظِيمٌ فَظَنَنْتُ أَنَّهُمْ أُمَّتِي، فَقِيلَ لِي هَذَا مُوسَى وَقَوْمُهُ، فَنَظَرْتُ فَإِذَا سَوَادٌ عَظِيمٌ، فَقِيلَ لِي هَذِهِ أُمَّتُكَ، وَمَعَهُمْ سَبْعُونَ أَلْفًا يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ بِغَيْرِ حِسَابٍ وَلاَ عَذَابٍ)) ثُمَّ نَهَضَ فَدَخَلَ مَنْزِلَهُ فَخَاضَ اَلنَّاسُ فِي أُولَئِكَ فَقَالَ بَعْضُهُمْ: فَلَعَلَّهُمْ اَلَّذِينَ صَحِبُوا رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) ، وَقَالَ بَعْضُهُمْ فَلَعَلَّهُمْ اَلَّذِينَ وُلِدُوا فِي الإِسْلامِ فَلَمْ يُشْرِكُوا بِاَللَّهِ شَيْئًا وَذَكَرُوا أَشْيَاءَ. فَخَرَجَ عَلَيْهِمْ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَأَخْبَرُوهُ فَقَالَ: ((هُمُ اَلَّذِينَ لاَ يَسْتَرْقُونَ وَلاَ يَكْتَوُونَ وَلاَ يَتَطَيَّرُونَ وَعَلَى رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ)) فَقَامَ عُكَّاشَةُ بْنُ مُحْصَنٍ فَقَالَ: اُدْعُ اَللَّهَ أَنْ يَجْعَلَنِي مِنْهُمْ. فَقَالَ: ((أَنْتَ مِنْهُمْ)) ثُمَّ قَامَ رَجُلٌ آخَرُ فَقَالَ: اُدْعُ اَللَّهَ أَنْ يَجْعَلَنِي مِنْهُمْ. فَقَالَ: ((سَبَقَكَ بِهَا عُكَّاشَةُ)) البخاري ومسلم
Huswayn bin ‘Abdir-Rahmaan amehadithia: Siku moja nilipokuwa na Sa’iyd bin Jubayr, aliuliza: “Nani miongoni mwenu aliyeona kimondo (nyota inayofukuza shaytwaan) jana usiku?” Nikajibu: “Mimi nimeiona.” Kisha nikaelezea kwamba sikuwa nikiswali wakati ule sababu nilidonelewa na nge mwenye sumu. Akasema: “Kisha ukafanya nini?” Nikajibu: “Nilifanya Ruqyah (kujitibu). Akauliza: “Kitu gani kimekupeleka ufanye hivyo?” Nikasema: “Ni Hadiyth niliyoisikia kutoka kwa Ash-Sha’biyy.” Akauliza: “Amekuhadithieni nini Ash-Sha’biyy?” Nikajibu: “Ameripoti kutoka kwa Buraydah bin Al-Huswayb amesema kwamba Ruqyah hairuhusiwi isipokuwa kwa ajili ya kijicho na kudonelewa (na mdudu sumu).” (Sa’iyd bin Jubayr) akasema: “Amefanya vyema kukomea kwenye aliyosikia (yaani: kufanyia kazi jambo kwa ujuzi kinyume na ujahili). Lakini Ibn ‘Abbaas ametusimulia kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Ummah zote zilipitishwa mbele yangu, nikamuona Nabiy akiwa na kundi dogo la watu, na Nabiy akiwa na mtu mmoja au wawili, na Nabiy akiwa hana mtu yeyote. Kisha nikaoneshwa idadi kubwa ya watu niliodhania ni katika Ummah wangu, lakini nikaambiwa: Huyo ni Muwsaa na watu wake. Kisha nikatazama nikaona kundi kubwa ambalo nikaamibwa: Hawa ni watu wako, miongoni mwao ni watu elfu sabini watakaoingia Jannah bila hesabu wala adhabu)). Kisha akainuka kuingia nyumbani kwake (na nyuma yake) watu wakaanza kujadiliaina ni nani hao watakaoweza kuwa. Wengineo wakasema: “Labda ni Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)” Wengine wakasema: “Labda ni wale waliozaliwa katika Uislamu na hawakumshirikisha Allaah kwa chochote.” (Wakataja mengine kadhaa) Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatoka na kuja na wakamwambia (waliyokuwa wakiyajadili). Akasema: ((Ni wale ambao wasiotafuta kufanyiwa Ruqyah, wala kujichoma chuma cha moto, wala hawaamini twiyaarah (itikadi ya mkosi au nuksi), bali wanamtegemea Rabb wao na kutawakali Kwake Pekee)) ‘Ukaashah bin Mihswan akasimama akasema: “Muombe Allaah niwe mmoja wao.” Akasema: ((Wewe ni mmoja wao)). Kisha mtu mwengine akasimama akasema: Muombe Allaah niwe mmoja wao (pia). Akasema: ((‘Ukaashah amekutangulia))[Al-Bukhaariy (3410) Muslim (220)]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni