أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
058-Suwrah Al-Mujaadalah: Aayah 8
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ نُهُوا عَنِ النَّجْوَىٰ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا نُهُوا عَنْهُ وَيَتَنَاجَوْنَ بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَمَعْصِيَتِ الرَّسُولِ وَإِذَا جَاءُوكَ حَيَّوْكَ بِمَا لَمْ يُحَيِّكَ بِهِ اللَّـهُ وَيَقُولُونَ فِي أَنفُسِهِمْ لَوْلَا يُعَذِّبُنَا اللَّـهُ بِمَا نَقُولُ ۚ حَسْبُهُمْ جَهَنَّمُ يَصْلَوْنَهَا ۖ فَبِئْسَ الْمَصِيرُ﴿٨﴾
8. Je, huwaoni wale waliokatazwa kunong’ona, kisha wanarudia yale waliyokatazwa nayo, na wananong’onezana kuhusu dhambi na uadui na kumuasi Rasuli na wanapokujia wanakuamkia kwa maamkizi Asiyokuamkia kwayo Allaah; na wanasema katika nafsi zao: Mbona Allaah Hatuadhibu kwa yale tunayoyasema? Jahannam inawatosheleza, wataingia waungue, basi ubaya ulioje mahali pa kuishia.
Sababun-Nuzuwl:
حدثنا عبد الصمد ثنا حماد عن عطاء بن السائب عن أبيه عن عبد الله بن عمرو أن اليهود كانوا يقولون لرسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم: سام عليك، ثم يقولون في أنفسهم، لولا يعذبنا الله بما نقول، فنزلت هذه الآية: ((وَإِذَا جَاءُوكَ حَيَّوْكَ بِمَا لَمْ يُحَيِّكَ بِهِ اللَّهُ)) إلى آخر الآية. .
Ametuhadithia ‘Abdu As Swamad, ametuhadithia Hammaad toka kwa ‘Atwaa bin As Saaib toka kwa baba yake toka kwa ‘Abdillaah bin ‘Amri ya kuwa Mayahudi walikuwa wakimwambia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Saam ‘alayka” (Mauti yawe juu yako), kisha wanajiambia wenyewe: “Kwa nini basi Allaah hatuadhibu kwa haya tuyasemayo?’ Hapo ikateremka Aayah hii:
وَإِذَا جَاءُوكَ حَيَّوْكَ بِمَا لَمْ يُحَيِّكَ بِهِ اللَّـهُ وَيَقُولُونَ فِي أَنفُسِهِمْ لَوْلَا يُعَذِّبُنَا اللَّـهُ بِمَا نَقُولُ ۚ حَسْبُهُمْ جَهَنَّمُ يَصْلَوْنَهَا ۖ فَبِئْسَ الْمَصِيرُ﴿٨﴾
Na wanapokujia wanakuamkia kwa maamkizi Asiyokuamkia kwayo Allaah; na wanasema katika nafsi zao: Mbona Allaah Hatuadhibu kwa yale tunayoyasema? Jahannam inawatosheleza, wataingia waungue, basi ubaya ulioje mahali pa kuishia.
[Al-Haythamiy kaitaja Hadiyth hii katika mjeledi wa saba ukurasa wa 122. Imesimuliwa na Ahmad, Al-Bazzaar na At-Twabaraaniy, na Isnaad yake ni nzuri haina shaka, kwa kuwa Hammaad aliisikia toka kwa ‘Atwaa bin As-Saaib katika hali ya uswahiyh, Muslim ameikhariji Hadiyth ya ‘Aaishah katika mjeledi wa 14 ukurasa 147, Ahmad katika mjeledi wa sita ukurasa 229, na Ibn Jariyj mjeledi wa 28 ukurasa wa 14].
حَدَّثَنَاهُ إِسْحَاقُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، أَخْبَرَنَا يَعْلَى بْنُ عُبَيْدٍ، حَدَّثَنَا الأَعْمَشُ، بِهَذَا الإِسْنَادِ غَيْرَ أَنَّهُ قَالَ فَفَطِنَتْ بِهِمْ عَائِشَةُ فَسَبَّتْهُمْ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم “ مَهْ يَا عَائِشَةُ فَإِنَّ اللَّهَ لاَ يُحِبُّ الْفُحْشَ وَالتَّفَحُّشَ ” . وَزَادَ فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ ((وَإِذَا جَاءُوكَ حَيَّوْكَ بِمَا لَمْ يُحَيِّكَ بِهِ اللَّهُ)) إِلَى آخِرِ الآيَةِ .
Ametuhadithia Is-haaq bin Ibraahiym, ametueleza Ya’alaa bin ‘Ubayd, ametuhadithia Al-A’amash kwa Isnaad hii isipokuwa amesema: ‘Aaishah akawagundua (makusudio yao), akawatukana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: ((Wacha ee ‘Aaishah, hakika Allaah Hapendi maneno machafu na tabia ya ulimi mchafu.” Akaongeza: Allaah (عزّ وجلّ Akateremsha:
وَإِذَا جَاءُوكَ حَيَّوْكَ بِمَا لَمْ يُحَيِّكَ بِهِ اللَّـهُ وَيَقُولُونَ فِي أَنفُسِهِمْ لَوْلَا يُعَذِّبُنَا اللَّـهُ بِمَا نَقُولُ ۚ حَسْبُهُمْ جَهَنَّمُ يَصْلَوْنَهَا ۖ فَبِئْسَ الْمَصِيرُ﴿٨﴾
Na wanapokujia wanakuamkia kwa maamkizi Asiyokuamkia kwayo Allaah; na wanasema katika nafsi zao: Mbona Allaah Hatuadhibu kwa yale tunayoyasema? Jahannam inawatosheleza, wataingia waungue, basi ubaya ulioje mahali pa kuishia.
Na pia,
دَّثَنَا عَبْدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا يُونُسُ، عَنْ شَيْبَانَ، عَنْ قَتَادَةَ، حَدَّثَنَا أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ، أَنَّ يَهُودِيًّا، أَتَى عَلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم وَأَصْحَابِهِ فَقَالَ السَّامُ عَلَيْكُمْ فَرَدَّ عَلَيْهِ الْقَوْمُ فَقَالَ نَبِيُّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " هَلْ تَدْرُونَ مَا قَالَ هَذَا " . قَالُوا اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ سَلَّمَ يَا نَبِيَّ اللَّهِ . قَالَ " لاَ وَلَكِنَّهُ قَالَ كَذَا وَكَذَا رُدُّوهُ عَلَىَّ " . فَرَدُّوهُ قَالَ "قُلْتَ السَّامُ عَلَيْكُمْ" . قَالَ نَعَمْ . قَالَ نَبِيُّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عِنْدَ ذَلِكَ "إِذَا سَلَّمَ عَلَيْكُمْ أَحَدٌ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ فَقُولُوا عَلَيْكَ" . قَالَ "عَلَيْكَ مَا قُلْتَ" . قَالَ : ((وإِذَا جَاءُوكَ حَيَّوْكَ بِمَا لَمْ يُحَيِّكَ بِهِ اللَّهُ)) . قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ .
Ametuhadithia ‘Abdu bin Humayd, ametuhadithia Yuwnus toka kwa Shaybaan toka kwa Qataadah, ametuhadithia Anas bin Maalik ya kwamba Myahudi mmoja alimjia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa na Maswahaba wake akasema: “As-Saamu ‘alaykum”, na watu wakamjibu. Nabiy wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Akawauliza: ((Je, mnajua kasema nini huyu?)) Wakasema: ((Allaah na Rasuli Wake Wanajua zaidi, yeye amesalimia tu ee Nabiy wa Allaah))?. Akasema: ((Hapana, lakini yeye amesema kadha na kadha, basi nijibishieni)). Wakamjibu. Akasema (Rasuli kumwambia Myahudi): Umesema: “As Saam ‘alaykum”. Akasema: ((Naam)). Na hapo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema wakati huo: ((Akiwasalimieni yeyote katika Ahlul-Kitaab, basi mwambieni “alayka”)). Akasema: “Yawe juu yako uliyoyasema”. Akasema:
وَإِذَا جَاءُوكَ حَيَّوْكَ بِمَا لَمْ يُحَيِّكَ بِهِ اللَّـهُ
Na wanapokujia wanakuamkia kwa maamkizi Asiyokuamkia kwayo Allaah;
[Jaami’ At-Tirmidhiy amesema Abuu ‘Iysaa Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh].
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni