Translate

Jumatano, 3 Julai 2019

Hukumu ya Mabachela kutumia dawa za kupunguza matamanio

Swali


Ni ipi hukumu ya kutumia madawa yanayopunguza kuja kwa matamanio pamoja na kuzingatia kwamba yanakuwa mengi kwa wale ambao ni mabachala wasiokuwa na uwezo wa kuoa?


Jibu



Hili linategemea ushauri wa daktari. Ikiwa kuyatumia madawa haya hayamdhuru mtu katika siku za huko mbeleni, hakuna neno. Ama ikiwa yanamdhuru hayafai. Kila kitu kinachomdhuru mtu basi kimekatazwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna madhara wala kudhuriana.”
Mtu anahitajia nguvu hizi huko mbeleni. Mtu atakapooa atazihitajia na atatamani abaki nayo hali ya kuyachunga mpaka pale utapokuja wakati ambao Allaah atamsahilishia mke na mambo yakawa mepesi. Isitoshe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewaelekeza vijana katika jambo pindi aliposema:
“Enyi kongamano la mabarobaro! Yule miongoni atakayeweza kuoa basi na aoe. Kwani hilo litamfanya kuteremsha macho na kuhidhi utupu. Asiyeweza basi afunge. Kwani hiyo kwake ni kinga”



Rejea Kitaab Al-Liqaa' Ash-Shahriy (51)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...