Translate

Alhamisi, 11 Julai 2019

058-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Mujaadalah: Aayah 1 - 4

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

058-Al-Mujaadalah: Aayah 1-4

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

قَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا وَتَشْتَكِي إِلَى اللَّـهِ وَاللَّـهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَا ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ﴿١﴾

Allaah Amekwishasikia kauli ya yule mwanamke anayejadiliana nawe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mumewe, na anamshitakia Allaah; na Allaah Anayasikia majibizano yenu. Hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.

 

الَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِنكُم مِّن نِّسَائِهِم مَّا هُنَّ أُمَّهَاتِهِمْ ۖ إِنْ أُمَّهَاتُهُمْ إِلَّا اللَّائِي وَلَدْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَيَقُولُونَ مُنكَرًا مِّنَ الْقَوْلِ وَزُورًا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٌ﴿٢﴾

Wale miongoni mwenu wanaowatamkia wake zao dhwihaar: Nyinyi kwetu kama migongo ya mama zetu.  Hao wake zao si mama zao. Hawakuwa mama zao isipokuwa wale waliowazaa. Na hakika wao bila shaka wanasema yasiyokubalika na kauli ya kuchukiza na uongo. Na hakika Allaah bila shaka ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kughufuria.

 

وَالَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِن نِّسَائِهِمْ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا قَالُوا فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مِّن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا ۚ ذَٰلِكُمْ تُوعَظُونَ بِهِ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ﴿٣﴾

Na wale wanaowatamkia wake zao dhwihaar, kisha wakarudi katika waliyoyasema (kuitengua dhwihaar), basi ni kuacha huru mtumwa kabla ya kugusana. Hayo mnawaidhiwa kwayo. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.

 

فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ مِن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا ۖ فَمَن لَّمْ يَسْتَطِعْ فَإِطْعَامُ سِتِّينَ مِسْكِينًا ۚ ذَٰلِكَ لِتُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۚ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ ۗ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٤﴾

Na yule asiyepata uwezo, basi afunge Swiyaam miezi miwili mfululuzo kabla ya kugusana. Na yule asiyeweza, basi alishe chakula masikini sitini. Hivyo ili mumuamini Allaah na Rasuli Wake. Na hiyo ni mipaka ya Allaah. Na makafiri watapata adhabu iumizayo. [Al-Mujaadalah: 1-4]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو مُعَاوِيَةَ، حَدَّثَنَا الأَعْمَشُ، عَنْ تَمِيمِ بْنِ سَلَمَةَ، عَنْ عُرْوَةَ بْنِ الزُّبَيْرِ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتِ الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي وَسِعَ سَمْعُهُ الأَصْوَاتَ، لَقَدْ جَاءَتِ الْمُجَادِلَةُ إِلَى النَّبِيِّ ـ صلى الله عليه وسلم ـ وَأَنَا فِي نَاحِيَةِ الْبَيْتِ تَشْكُو زَوْجَهَا وَمَا أَسْمَعُ مَا تَقُولُ فَأَنْزَلَ اللَّهُ ((قَدْ سَمِعَ اللَّهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا)) إلى آخر الآية.

Ametuhadithia ‘Aliy bin Muhammad, ametuhadithia Abuu Mu’aawiyah, ametuhadithia Al-A’amash kutoka kwa Tamiym bin Salamah kutoka kwa ‘Urwah bin Zubayr kutoka kwa ‘Aaishah amesema: Himdi ni Yake Allaah Ambaye Usikivu Wake umezienea sauti zote. Hakika alikuja mwanamke aliyeleta mashtaka yake kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  na kuzungumza naye, nami nilikuwa pembezoni mwa nyumba sisikii anayoyasema. Allaah (عزّ وجلّ)  Akateremsha:

 

قَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا وَتَشْتَكِي إِلَى اللَّـهِ وَاللَّـهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَا ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ﴿١﴾

Allaah Amekwishasikia kauli ya yule mwanamke anayejadiliana nawe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mumewe, na anamshitakia Allaah; na Allaah Anayasikia majibizano yenu. Hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.

 

[Hadiyth hii ameikhariji Al-Bukhaariy ikiwa Mu’allaq katika mjeledi wa 17 ukurasa wa 143, An-Nasaaiy katika mjeledi wa 6 ukurasa 137, Ibn Maajah nambari 188 na nambari 2063, na Ibn Jurayj katika mjeledi wa 28 ukurasa wa 5 na 6, na Al-Haakim katika mjeledi wa pili ukurasa wa 481. Amesema Isnadi yake ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy ameikubali]

 

 

Pia,

 

حَدَّثَنَا الْحَسَنُ بْنُ عَلِيٍّ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ آدَمَ، حَدَّثَنَا ابْنُ إِدْرِيسَ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِسْحَاقَ، عَنْ مَعْمَرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ حَنْظَلَةَ، عَنْ يُوسُفَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ سَلاَمٍ، عَنْ خُوَيْلَةَ بِنْتِ مَالِكِ بْنِ ثَعْلَبَةَ، قَالَتْ ظَاهَرَ مِنِّي زَوْجِي أَوْسُ بْنُ الصَّامِتِ فَجِئْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَشْكُو إِلَيْهِ وَرَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُجَادِلُنِي فِيهِ وَيَقُولُ: "‏اتَّقِي اللَّهَ فَإِنَّهُ ابْنُ عَمِّكِ‏.‏ فَمَا بَرِحْتُ حَتَّى نَزَلَ الْقُرْآنُ: ((قَدْ سَمِعَ اللَّهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا))‏ إِلَى الْفَرْضِ فَقَالَ: "‏يُعْتِقُ رَقَبَةً "‏.‏ قَالَتْ لاَ يَجِدُ قَالَ:  ‏"‏فَيَصُومُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ‏"‏ ‏.‏ قَالَتْ يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّهُ شَيْخٌ كَبِيرٌ مَا بِهِ مِنْ صِيَامٍ ‏.‏ قَالَ: ‏"‏فَلْيُطْعِمْ سِتِّينَ مِسْكِينًا"‏ ‏.‏ قَالَتْ مَا عِنْدَهُ مِنْ شَىْءٍ يَتَصَدَّقُ بِهِ، قَالَتْ: فَأُتِيَ سَاعَتَئِذٍ بِعَرَقٍ مِنْ تَمْرٍ، قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ فَإِنِّي أُعِينُهُ بِعَرَقٍ آخَرَ ‏.‏ قَالَ: ‏"‏قَدْ أَحْسَنْتِ اذْهَبِي فَأَطْعِمِي بِهَا عَنْهُ سِتِّينَ مِسْكِينًا وَارْجِعِي إِلَى ابْنِ عَمِّكِ‏"‏ ‏.‏ قَالَ: وَالْعَرَقُ سِتُّونَ صَاعًا.

 قَالَ أَبُو دَاوُدَ فِي هَذَا إِنَّهَا كَفَّرَتْ عَنْهُ مِنْ غَيْرِ أَنْ تَسْتَأْمِرَهُ ‏.‏ وَقَالَ أَبُو دَاوُدَ وَهَذَا أَخُو عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ.

Ametuhadithia Al-Hasan bin ‘Aliy, ametuhadithia Yahyaa bin Aadam, ametuhadithia Ibn Idriys kutoka kwa Muhammad bin Is-haaq kutoka kwa Ma’amar bin ‘Abdillaah bin Handhwalah kutoka kwa Yuwsuf bin ‘Abdillaah bin Salaam kutoka kwa Khuwaylah bint Maalik bin Tha’alabah amesema: Mume wangu Aws bin Swaamit alinitamkia “dhwihaar” (kuwa mimi ni kama mgongo wa mama yake). Nikamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلمili kumshtakia, na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  ananihoji kuhusiana naye akiniambia: ((Mche Allaah. Yeye ni bin 'ami wako)). Sikuacha kwenda mpaka ikateremka Qur-aan:

 

قَدْ سَمِعَ اللَّهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا

Allaah Amekwishasikia kauli ya yule mwanamke anayejadiliana nawe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mumewe..  

 

Akasema (Rasuli): (((Amwache huru mtumwa)). Akasema (Khuwaylah): Hana (mtumwa). Akasema: ((Basi afunge Swawm ya miezi miwili mfululizo)). Akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Yeye ni mtu mzima sana, hana Swiyaam. Akasema: ((Basi alishe masikini sitini)). Akasema: Hana chochote cha kutoa Swadaqah. Akasema: Na wakati ule lililetwa kapu la tende, nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Na mimi nitamsaidia kwa kapu jingine. Akasema: ((Hakika umefanya vizuri. Nenda ukamlishie kwayo mumeo masikini sitini, na urejee kwa bin 'ami wako)). Amesema: Kapu moja ni pishi sitini. Abuu Daawuwd amesema kuhusiana na hili: Hakika yeye alimtolea kafara bila kumtaka rukhsa. Na Abuu Daawuwd amesema: Na huyu (Aws) ni nduguye ‘Ubaadah bin As-Swaamit. [Abuu Daawuwd, Kitaab Atw-Twalaaq]

  

Na pia,

 

أَخْبَرَنَا إِسْحَاقُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ أَنْبَأَنَا جَرِيرٌ، عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ تَمِيمِ بْنِ سَلَمَةَ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، أَنَّهَا قَالَتِ الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي وَسِعَ سَمْعُهُ الأَصْوَاتَ لَقَدْ جَاءَتْ خَوْلَةُ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم تَشْكُو زَوْجَهَا فَكَانَ يَخْفَى عَلَىَّ كَلاَمُهَا فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ : ((قَدْ سَمِعَ اللَّهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا وَتَشْتَكِي إِلَى اللَّهِ وَاللَّهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَا))‏ الآيَةَ ‏.‏

Ametueleza Is-haaq bin Ibraahiym, amesema, ametueleza Jariyj kutoka kwa Al-A’amash, kutoka kwa Tamiym bin Salamah kutoka kwa ‘Urwah kutoka kwa ‘Aaishah kuwa amesema: Himdi ni Yake Allaah Ambaye Usikivu Wake umezienea sauti zote. Hakika alikuja Khawlah kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akimshitaki mumewe. Maneno yake nilikuwa siyasikii. Na hapo Allaah (عزّ وجلّ)  Akateremsha:

قَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا وَتَشْتَكِي إِلَى اللَّـهِ وَاللَّـهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَا ۚ  

Allaah Amekwishasikia kauli ya yule mwanamke anayejadiliana nawe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mumewe, na anamshitakia Allaah; na Allaah Anayasikia majibizano yenu. [An-Nasaaiy, Kitaab Atw-Twalaaq]

 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...