Translate

Jumatatu, 1 Julai 2019

Hukmu ya Muislamu Anayejiua

                                                     Hukmu ya Muislamu Anayejiua





Uislamu umetukataza kujiua na yeyote mwenye kujiua atakuwa ametenda madhambi makubwa na yatakayomsababishia kuingia motoni na kuharamishiwa pepo. Isitoshe, ataadhibiwa kwa chombo kilekile alichotumia kujiulia. Allaah Aliyetukuka Atuepushe kabisa na balaa hilo la kujinyonga au kujiua kwa njia yoyote ile.

Anasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutoka katika Hadiyth iliyosimuliwa na Abu Hurayrah,
"Yeyote atakayejitupa kutoka mlimani na kujiua, atatupwa ndani ya moto milele. Atakayekunywa sumu na kujiua, basi atatupwa motoni na huko atakuwa akiinywa hiyo sumu milele. Atakayejiua kwa kipande cha chuma, atatiwamotoni akiwa na kipande hicho cha chuma akijitwanga nacho tumboni kwake humo motoni milele." Al-Bukhaariy na Muslim

Kadhaalika, mtu anayejiua, au jambazi, au aliyefariki kwa kutumia madawa ya kulevya au kuuza, mlevi n.k. wote hao watatengwa kuswaliwa na Viongozi wa Dini ili iwe funzo kwa wale wenye tabia hizo waweze kujiepusha na maovu hayo. Lakini, hata hivyo, wanaweza kuswaliwa na watu wa kawaida.


HUKUMU  YA  KUJIUA KWA SABABU YA MATESO NA MITIHANI YA KIDUNIA


Tufahamu kuwa mitihani katika hii dunia na haswa kwa Muumini ni lazima. Na kila mmoja anapimwa na Allaah Aliyetukuka kwa kiasi cha Imani yake. Allaah Aliyetukuka Anasema:
Je! Wanadhani watu wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao wasijaribiwe? Hakika Tuliwajaribu waliokuwa kabla yao, na kwa yakini Allaah Atawatambulisha walio wa kweli na Atawatambulisha walio waongo” [Al-Ankabut [29]: 2 – 3].
Na tena:
Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, bila ya kukujieni kama yaliyo wajia wale waliopita kabla yenu? Iliwapata shida na madhara na wakatikiswa hata Mtume na walio amini pamoja naye wakasema: Lini nusura ya Allaah itakuja? Jueni kuwa nusura ya Allaah ipo karibu” [Al-Baqarah [2]: 214].

Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) anatuelezea kuwaMuislamu mzuri ni yule anaponeemeshwa hushukuru na hiyo ikawa ni kheri kwake na anapopata mitihani husubiri, na hiyo pia ikawa ni kheri kwake. [Muslim].

Kujiua kwa sababu ya mateso ni miongoni mwa madhambi makubwa inayompeleka mwenye kufanya kitendo hicho motoni. Kwa hivyo, mwenye kujiua makaazi yake siku ya Kiyama ni Motoni.  Dalili kutoka Hadiyth zifuatazo:

Kutoka kwa Jundab kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mtu alifikwa na maafa ya majeraha akajiua, hivyo Allaah Amesema: Mja wangu amejisababisha kufa mwenyewe kwa kuharakiza, hivyo Nimemharamisha Pepo.” [Al-Bukhaary]

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:  “Yeyote atakayejitupa kutoka mlimani na kujiua ataingia motoni akiuangukia ambako ataishi humo milele. Na yeyote atakayekunywa sumu na kujiua nafsi yake, atabeba sumu yake mkononi mwake huku anainywa motoni ambako ataishi milele. Na yeyote atakayejiua kwa silaha ya chuma, atabeba silaha yake mkononi mwake na huku anajichinja tumbo lake motoni ambako ataishi milele.” [Al-Bukhaariy]


Anas bin Maalik ameripoti kuwaMtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Asiombe mmoja wenu kufa kwa sababu ya shida iliyomfika, bali ikiwa hakupata msaada aombe (du’aa) “Ee Allaah, nijaalie niishi ikiwa uhai kwangu ni kheri na nipe mauti ikiwa mauti kwangu ni kheri kwangu” [Muslim]

Kadhaalika, mtu anayejiua, au jambazi, au aliyefariki kwa kutumia madawa ya kulevya au kuuza, mlevi n.k. wote hao watatengwa kuswaliwa na Viongozi wa Dini ili iwe funzo kwa wale wenye tabia hizo waweze kujiepusha na maovu hayo. Lakini, hata hivyo, wanaweza kuswaliwa na watu wa kawaida.


Allaah Aliyetukuka Atuepushe na balaa la kujiua na mabalaa mengine kama hayo.


Na Allaah Anajua zaidi.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...