Swali: Ni yepi maoni yenye nguvu kuhusu ambaye anagusa msahafu ilihali yuko na hadathi?
Jibu: Haijuzu kugusa msahafi ilihali mtu yuko na hadathi. Amesema (Ta´ala):
لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ
“Haigusi isipokuwa waliotwaharishwa kabisa.” (16:79)
Katika Hadiyth ya ´Amr bin Hazm ambaye amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Haigusi Qur-aan isipokuwa yule mwenye twahara.”
Haya ndio maoni ya wale maimamu wane. Haifai kuigusa Qur-aan isipokuwa yule ambaye yuko na wudhuu´.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2RUBFPk
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni